Urithi wa Gamal Abd El Nasser ulikwenda wapi? Na nani aliyeuharibu?

Urithi wa Gamal Abd El Nasser ulikwenda wapi? Na nani aliyeuharibu?

Na/ Amr Sabeh

 Mapinduzi ya Julai 23, 1952 yamezinduliwa  na Kiongozi Gamal Abd El Nasser katika mazingira ya kitaifa, kiarabu na kikanda yenye hali ya hatari sana.

Misri ilikuwa jamii inaongozwa na mahusiano ya nusu kikabaila na ubepari nyuma, na mkoloni Mwingereza alikuwa akitawala uwezo wote wa nchi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, akiungwa mkono na jeshi lake yenye askari elfu themanini wa Uingereza, kundi la wakala jasusi anayoyaunda kutoka kwa Wamisri,  jamii ya nje lililovamia Misri ili kunyonya rasilimali zake na uporaji wa mali zao, na familia ya kifalme ya kigeni imezama katika rushwa na kuoza, na fedheha zake za kisiasa, kiuchumi na kijamii zilikuwa hadithi ya wote.

Chama cha Al-Wafd kilikuwa kuondoka uongozi wa harakati ya kitaifa tangu msimamo wake mbovu mnamo Februari 4, 1942, na kikawa chama kwa watu tajiri sana, na itikadi yake ya Yemen ya maadui kwa maslahi ya wengi yalionekana.

Mradi wa kitaifa wa serikali ya mwisho ya Al-Wafd kabla ya mapinduzi ni kupambana furaha !!

Je, kuna unyonge kama hivyo?

Na nguvu nyingine ya kisiasa kama jamaa wa Al-Ekhwan Waislamu, wakomunisti na wajamaa walikuwa kuhamia kwenye eneo la tukio, lakini wote walikuwa hawawezi kusogea kwa umakini ili kuwasha mapinduzi yaliyokamata mfumo mgumu wa kisiasa na usiotulia.

Moto huko Kairo mnamo Januari 26, 1952 ulikuwa  kama tangazo la kufilisika kwa kile kinachoitwa enzi ya huria katika historia ya Misri ya kisasa kuanzia 1923 hadi 1952.

Na kwenye uwanja wa Kiarabu, ulimwengu wa Kiarabu iligawanyika kwa nchi na majimbo madogo chini ya udhibiti wa ukoloni mpya wa Uingereza, Ufaransa na Marekani uliopo katika eneo hilo baada ya Vita vya pili vya Dunia.

Israel ilikuwa imewekwa kwa nguvu kati ya ulimwengu wa Kiarabu ,ndani ya Palestina, ili kutenganisha ulimwengu wa Kiarabu kwa Mashariki na Magharibi, na kutumika kama ubeberu wa kulinda maslahi ya nchi za Magharibi katika eneo muhimu ya kimkakati kwa Wamagharibi, wenye akiba ya mafuta ya kwanza Duniani, na kuficha kwa mradi wowote wa maendeleo wa kisasa wa kitaifa katika ulimwengu wa Kiarabu.

Kwa kiwango cha kimataifa, vita baridi vilikuwa vikiendelea kati ya kambi za kibepari na kijamaa kwenye nyanja za cheo na kuweka udhibiti.

Katika mazingira hayo, Gamal Abd El Nasser alivunja mapinduzi ya Misri, alipopokea Abd El Nasser alitawala Misri, Misri ilikuwa nchi maskini iliyo nyuma ya viwanda, na mazao yake ya kilimo ya msingi ni pamba iliyokuwa ukiritimba wa kundi la mabwana, walanguzi na wageni.

Uchumi wa Misri ulikuwa nyuma, ukifuatilia  ukiritimba wa ubepari wa kigeni.

Kulikuwa na watu 960 tu waliotawala kazi zote za msingi za Baraza ya idara za makampuni ya viwanda,  kati yao tunakuta Wamisri 265 pekee, na Benki ya Barclize ya Kiingereza ilikuwa kudhibiti 56% tu ya amana, na Benki ya Misri imetawaliwa na mali za Waingereza na Marekani.

Uchumi wa Misri ulikuwa bure na kusitishwa kwa sababu ya uhusiano wake na maslahi ya nje kwa kupitia mabenki, makampuni ya bima na biashara ya nje katika mauzo na maduhuli, na huduma zote za uchumi wa Misri zilikuwa kuzitawaliwa na Wageni na Wayahudi.

Jambo lililofanywa mwanauchumi mkuu wa Misri Dkt. Abdul Jalil Al-Omari kuelezea uchumi wa Misri akisema: "uchumi wa Misri ulikuwa kama ng'ombe aliyezunguka katika nchi ya Misri, lakini sehemu zake zote za maziwa kamuliwa nje ya Misri).

Nyaraka za kihistoria zinatupa ukweli wa giza juu ya hali ya mambo ya ndani kabla ya mapinduzi.  Misri ilikuwa bajeti ya mwisho ya serikali mwaka wa 1952, ikionesha kasoro la paundi milioni 39.

Mgao wa uwekezaji katika miradi mipya kulingana na bajeti, iwe na serikali au sekta binafsi, ulikuwa sifuri. 

 Pia, salio la paundi la Misri ilidaiwa nalo badala ya bidhaa, huduma na njia zote za usafirishaji ilizotoa kwa ajili ya juhudi za vita vya Washirika mnamo wa Vita vya Pili vya Dunia, na paundi milioni 400 zimekuwa kufujwa, na haikubakia isipokuwa paundi milioni 80 pekee.

Mnamo miaka ya themanini ya karne iliyopita, gazeti la Al-Wafd liliibua suala hili linilohusu ukweli kwamba Misri ilikuwa mkopeshaji wa Uingereza kabla ya mapinduzi, na nyaraka zinathibitisha kuwa kiasi kilichobaki cha deni, ambacho ni paundi milioni 80, Uingereza ilikataa kuwapa Misri mnamo wa kipindi cha utawala wa Rais Gamal Abd El Nasser, ukisumbuka Nasser na sera zake dhidi yake, na haikutolewa hadi katikati ya miaka ya sabini ya karne iliyopita mnamo wa utawala wa Sadat. Uporaji uliofanyika kwenye ardhi ya kilimo, huko Misri katika karne yote ya kumi na tisa na nusu ya kwanza ya karne ya ishirini, iliporwa na familia ya Muhammad Ali hapo mwanzo na kisha ikaruhusu hisa yake kwa wanunuzi wa kigeni, na tabaka la Wamisri wachache sana, ulifanya kazi katika kuliunda ili kuwa chanzo chake kuunga mkono mbele ya wengi wa Wamisri maskini.

Waingereza walipoivamia Misri mwaka wa 1882, walifanya kazi ya kuunda tabaka lililokuwa na uaminifu kwao, na wakafuata mtindo wao wa kiustaarabu, na wakagawanya miongoni mwa wanachama wake maelfu ya ekari, chini ya hali ya kutiliwa shaka na kali kwa mkulima wa Misri aliyedhulumiwa, aliyeachwa mawindo kwa ujinga, umasikini na maradhi, ambaye ana kanzu moja tu, hapati chakula cha siku yake, na anachukuliwa kama watumwa wa kuwatumikia mabwana wake wa kifalme.

Kampuni ya Suez Canal ilikuwa kuhusisha mateso ya Wamisri katika vipimo vyake vyote. Mfereji uliochimbwa katika ardhi ya Misri na makumi ya maelfu ya Wamisri waliotoa damu zao kwa ajili maji yake, ulichukuliwa, na kampuni ya Suez Canal ilikuwa kama nchi ndani ya nchi, ina bendera yake yenyewe, kodi, vyombo vya dola na mtaa wa kipekee ambao Wamisri walizuia kuuingia.

Mwenyekiti wa kampuni alichukuliwa kama Marais wa nchi, akizungukwa na sherehe zote za heshima na shukurani, na hakuna afisa wa Misri anayemshtaki kwa chochote.  Na nyaraka za Amerika, Ufaransa na Israeli zinathibitisha kuwa kampuni hii ililipa paundi milioni 400 kutoka kwa pesa za Misri kusaidia juhudi za kijeshi za washirika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Pia, ililipa mali nyingi ya fedha, yaliyokadiriwa kwa milioni kumi kwa Harakati ya kizayuni nchini Palastina, kama misaada yanayounga mkono mradi wa kitaifa wa Wayahudi.

 Baada ya kuanzishwa kwa Israel usimamizi wa Kampuni ya Suez Canal ilianzisha ofisi za uratibu wa habari na ujasusi ili kuwasiliana na chombo cha Mossad, na pia iliendelea kulipa fedha za Misri kwa taasisi ya kizayuni ili kuiunga mkono.

Mipango yote ya mustakabali ya kampuni hiyo  ilijikita katika kurefusha mkataba wa makubaliano kwa kipindi kipya cha miaka 99. 

Ubora na utajiri wa Misri uliibiwa kutoka kwa watu wake, ukafyonzwa na tabaka za wateja, familia tawala inayoingilia kati, wanunuzi wa kigeni na Wayahudi walionyonywa.

Misri haikuwa miliki ya watu wake. Misri haikuwa na sera huru ya mambo ya nje, bali sera yake ilijikita kwenye mzunguko wa wanasiasa wa Uingereza.  Mfalme Farouk alipoamua kuingia katika Vita vya Palestina, jeshi la Misri lilishindwa katika vita hivyo kutokana na usaliti wa majeshi mengine ya Waarabu, ukosefu wa maandalizi, silaha duni, uzembe wa viongozi, na mipango mibovu, na kutokana na kushindwa, 78% kutoka maeneo ya kihistoria ya Palastina na kuanzisha nchi iliyoharibika. Gamal Abd El Nasser aliposhika utawala wa Misri wakati hali yake ilikuwa mbaya, na baada ya kufukuzwa kwa Mfalme Farouk mnamo Julai 26, 1952.

Sheria ya kwanza ya mageuzi ya kilimo ilitolewa Septemba 9, mwaka wa 1952. 

Sheria hiyo ina sura 6 zinazojumuisha vifungu 40.

 Kifungu cha kwanza kilibainisha kima cha juu cha umiliki wa kilimo kwa ekari 200 kwa kila mtu, na kifungu cha nne kiliruhusu mmiliki kutoa ekari mia kwa watoto wake.

Sheria iliwaruhusu wamiliki kuuza ardhi yao ya ziada kwa yeyote waliyemtaka, na iliwapa haki ya kuepuka kuuzwa kwa ardhi za watu wengine.

Pia, sheria iliamua kulipa fidia kwa wamiliki, kwani bei za ardhi zilikadiriwa mara kumi ya thamani ya kukodisha, na mali na vifaa vingine (miti na vifaa) kulingana na ardhi viliongezwa kwa viwango vya juu.

Sheria ilidhibiti utoaji wa fidia kwa kuchora hati kutoka kwa serikali ili kulipwa kwa muda wa miaka thelathini, kwa kiwango cha riba cha kila mwaka.

Sheria iliamua kusambaza ardhi ya ziada kwa wakulima wadogo kwa kadri ya (ekari 2 hadi 5), kwa sharti la kulipa bei ya ardhi hizi kwa miaka 30, na kwa ziada ya 3% kila mwaka, na kuongeza asilimia 1.5 ya bei ya jumla ya ardhi; wafa kwa mali ambazo zilikuwa duniani (miti, vifaa ... nk).

Sura ya pili ya sheria iligusia mpangilio wa vyama vya ushirika katika ardhi zilizogawiwa.  Ama sura ya nne, ilibainisha idadi ya hatua za kuzuia kugawanyika kwa ardhi iliyosambazwa, pamoja na kodi mpya ya ardhi.  Sura ya tano iligusia uhusiano kati ya wamiliki na wapangaji.  Sura ya sita na ya mwisho inahusiana na kuweka kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa kilimo, na kuwapa haki ya kuandaa vyama vyao vya kilimo.

Jumla ya ardhi ambayo sheria ya Septemba ilitumika mnamo wa mwaka wa 1952 ilifikia eneo la ekari 653,736,000 za wamiliki wakubwa 1,789, lakini ardhi ambayo sheria ilitumika kwa kweli ilifikia ekari elfu 372,305. Ama yaliyobaki, ambayo ni karibu nusu, wamiliki waliiuza kwa mbinu zao wenyewe hadi Oktoba, mwaka wa 1953, wakati serikali ilifuta maandishi yaliyowaruhusu wamiliki kuziuza kwa njia yao wenyewe.

Sheria ya pili ya mageuzi ya kilimo ilitolewa mwaka wa 1961, ambayo ni Sheria (Na. 127 ya mwaka 1380 AH = 1961 AD), na jambo muhimu zaidi katika sheria hii ni kwamba kufanya kiwango cha juu cha umiliki wa mtu binafsi ni ekari 100, pamoja na ekari 50 kwa ajili ya familia iliyobaki (watoto) kwa ajili ya manufaa tu, na mauzo yoyote ya ardhi yamepigwa marufuku kutoka mmiliki wa watoto wake, na pia sheria ilifuta ubaguzi wa awali wa ardhi yenye rutuba.

Ardhi iliyohamishiwa kwa "mageuzi ya kilimo" kama matokeo ya sheria hii inakadiriwa kuwa ekari 214,132,000.  Kisha sheria ya tatu ya mageuzi ya kilimo ilitolewa mwaka wa 1969, ambayo ni Sheria ya 50 ya 1969, iliyofanya kikomo cha juu cha umiliki wa mtu binafsi wa ekari 50.

Takwimu rasmi zinasema kwamba hadi 1969, ekari elfu 989,184 ziligawanywa kwa wakulima, ambapo ekari elfu 775,018 zilikamatwa kwa mujibu wa sheria za mageuzi ya kilimo, na ekari 184,411,000 zilihusishwa na taasisi mbalimbali, na wengine, ekari elfu 29,755. ilikuwa mapato ya ardhi kwa Nili. Kulingana na takwimu rasmi zilezile, ardhi hizi ziligawiwa kwa familia 325,670,000, na vyama vya kilimo vilianzishwa katika vijiji vyote vya Misri, na serikali, kupitia vyama hivyo, iliunda mfumo wa kupanga kwa kilimo nchini kote. Jamhuri ilibainisha aina za mimea, na ilitoa kwa wakulima mbegu, dawa na mbolea, pamoja na kununua mazao kutoka kwa wakulima. Mgawanyiko wa umiliki wa kilimo kwa kuzingatia mipango ya kina ya kilimo kupitia mzunguko wa kilimo, huondoa tatizo la ukosefu wa ajira, na kuinua kiwango cha kiuchumi cha mkulima wa Misri katika mfumo sambamba na mpango wa uchumi wa serikali kufikia kujitosheleza kwa mimea ya kilimo.

Jambo muhimu na kubwa kuliko hayo yote lilikuwa ni mabadiliko yaliyotokea katika hali ya mkulima mmisri na familia yake, ambapo shule na vitengo vya afya viliingia vijijini, na viwango vya mwamko na elimu viliongezeka, na hali ya afya na kiuchumi katika vijijini iliiboresha kwa sababu ya mapinduzi.

Bwawa la Juu lilikuwa mradi mkubwa,  na muhimu zaidi wa miradi ya mapinduzi, ambayo ni kilimo kwanza, kwani ilitoa kiasi cha maji kinachohitajika ili kubadilisha Umwagiliaji wa hayd kuwa Umwagiliaji wa kudumu, na kutokana na hilo, karibu ekari milioni 2 zilirejeshwa. Misri, wakati wa enzi ya Abd El Nasser, iliweza kujitosheleza kutokana na mazao yake yote ya kilimo isipokuwa ngano,  ambapo ilikidhi 80% kutoka mahitaji yake.

Mnamo  1969, uzalishaji wa pamba nchini Misri ulifikia kantari milioni 10 na 800 elfu, ambayo ni idadi kubwa zaidi ya uzalishaji wa pamba katika historia ya kilimo cha Misri hata kidogo.  Eneo linalolimwa la mpunga nchini Misri limefikia zaidi ya ekari milioni moja, ambalo ni eneo la juu zaidi kupandwa katika historia ya Misri.

Kulima kwa aina mpya za ngano kulijaribiwa, kama vile ngano ya Mexico na ngano ya Giza 155.  Katika uwanja wa viwanda, baraza la kudumu la maendeleo ya uzalishaji wa kitaifa lilianzishwa mnamo wa mwezi wa Septemba, na baraza lilitoa mpango wa uwekezaji wa umma mnamo wa Julai, mpango kabambe kwa miaka 4, kulingana nayo urekebishaji wa ardhi ulianza, kujenga miradi mikubwa ya tasnia kama vile chuma na chuma, Kampuni ya Mbolea ya Kima, viwanda vya matairi ya mpira, viwanda vya mabehewa ya reli ya SEAF,  na viwanda vya kebo za umeme.

Na mnamo miaka ya sitini, njia za umeme zilipanuliwa kutoka Aswan hadi Aleskandaria, pia migodi iliyojengwa huko Aswan na Oasis ya Bahariya, miradi hiyo yote ilikuwa ya kujifadhili.  Mnamo wa Julai 26, 1956, Rais Gamal Abd El Nasser alitaifisha Kampuni ya Suez Canal, na kuirudisha Misri.

Baada ya kushindwa kwa uchokozi wa pande tatu, fedha za Waingereza na Wafaransa nchini Misri zilifanywa Misri, zikataifishwa na kunyang'anywa.  Na Shirika la Uchumi lilianzishwa mwaka wa 1957, linalochukuliwa kuwa kiini cha kwanza cha sekta ya umma ya Misri, na taasisi zote za kigeni za Misri zilikuja kwake.  Mnamo wa Februari 13, 1960, Rais Abd El Nasser alitaifisha benki ya Misri, benki kubwa zaidi ya biashara nchini, na kampuni zote za viwanda zilizohusika, baada ya Uingereza na Marekani wakitawala jengo hilo kubwa, Abd El Nasser alilirejesha kwa Misri.

Mnamo Julai 1961, maamuzi ya ujamaa yalitolewa, na ilionekana wazi kuwa mfumo huo ulikuwa unaelekea aina ya uchumi uliopangwa chini ya usimamizi wa serikali na kuongozwa na sekta ya umma.  Kupitia hatua hizi, Misri iliweza kufikia kiwango cha ukuaji kutoka mwaka wa 1957 hadi 1967, kilichofikia takriban asilimia 7 kila mwaka. Chanzo cha takwimu hii ni ripoti ya Benki ya Dunia Nambari [870-A] kuhusu Misri iliyotolewa Washington mnamo wa Januari 5 , mwaka wa 1976.  Hii ina maana kwamba Misri iliweza, katika miaka kumi ya enzi ya Abd El Nasser, kujiendeleza mara nne zaidi ya kile ilichoweza kufikia katika miaka arobaini iliyotangulia enzi ya Abd El Nasser.

Haya yalikuwa ni matokeo yasiyo ya kifani katika ulimwengu mzima unaoendelea, ambapo kiwango cha maendeleo ya kila mwaka katika nchi zake zilizo huru zaidi katika kipindi hicho hakikuzidi 2.5%. Bali asilimia hii ilikuwa kubwa kuliko ile ya nchi zilizoendelea, isipokuwa tu Japan, Ujerumani Magharibi, na kundi la nchi za kikomunisti.  Kwa mfano, Italia, ambayo ni nchi ya viwanda iliyoendelea, na mojawapo ya nchi kubwa za viwanda imepata kiwango cha ukuaji wa takriban 4.5% inayokadiriwa tu katika muda huo huo.  Misri, pamoja na India na Yugoslavia, ilianza mapema miaka ya sitini mradi kabambe wa kutengeneza ndege, makombora, injini za ndege na silaha.

Hadi mwaka wa 1967, Misri ilikuwa bora kuliko India katika utengenezaji wa ndege na injini za ndege, na ndege ya jet ya Misri ilitengenezwa Kairo 300. Na Misri ilitengeneza makombora mawili ya kwanza yaliyotengenezwa kwa msaada wa wanasayansi wa kombora wa Ujerumani, lakini yaliharibiwa na kasoro katika vifaa vya uelekezi mnamo wa mwaka wa 1966. Tofauti kati ya mpango wa nyuklia wa Misri na mwenzake wa Israeli ilikuwa mwaka mmoja na nusu Kwa kupendelea mpango wa nyuklia wa Israeli, na licha ya kurudi nyuma, Misri ilikuwa karibu ya kufikia usawa wa nguvu katika uwanja wa nyuklia. kati yake na Israel ifikapo mwaka wa 1971.

Kwa bahati mbaya, baada ya Vita vya Oktoba vya 1973, Rais Sadat alisitisha miradi yote hii na kumaliza uwepo wake, na sasa tuangalie India imefikia wapi katika uwanja wa makombora, ndege na silaha za nyuklia huko Misri ili kutambua ukubwa wa Gamal Abd El Nasser katika kuona mbali na hatari ya mradi wake wa kufufua upya mradi wa kizayuni wa Marekani katika eneo mwaka wa 1965 na baada ya Kukamilisha mpango wake wa kwanza wa miaka mitano. Pato la taifa la Misri lilifikia takriban dola bilioni 5.1, wakati mwenzake wa Saudia alikuwa karibu dola bilioni 2.3 katika mwaka huo huo.

Ama kuhusu Emarates, ilikuwa bado haijaanzishwa.  Pato la taifa la Thailand, Indonesia, Malaysia, Korea Kusini na Singapore, mtawalia, lilifikia takriban dola milioni 4,390, 3,840, 3130, 3000 na 970 milioni katika mwaka uliotajwa. Yaani, kila moja ya nchi hizi ilikuwa nyuma ya Misri katika suala la Pato la Taifa.

Mnamo  Juni 5, mwaka wa 1967, siku ya hesabu ilifika kwa uzoefu wa mradi wa Gamal Abd El Nasser katika vita, ambao Rais wa Ufaransa Charles de Gaulle alivielezea kama (vita vya Amerika na utendaji wa Israeli).  Licha ya vurugu za mgomo na ukubwa wa kushindwa kijeshi.  Je, Misri imeporomoka na kuisha, kama baadhi ya waraibu wakijaribu kuendeleza kushindwa, ili kutuaminisha kwamba vita vya 1967 ndio chanzo cha matatizo yote ya Misri?  !!

Tukitazama hali ya Misri baada ya kushindwa, inatubainikia yafuatayo: Uchumi wa Misri ulilipa gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa Bwawa la Juu, na ujenzi wa bwawa hili haukukamilika isipokuwa mwaka wa 1970, kabla kifo cha Rais Abd El Nasser.

Mkusanyiko wa kiwanda wa alumini pia kilijengwa huko Nagaa Hammadi, ambao ni mradi mkubwa uliogharimu karibu pauni bilioni 3. Kwa kuzingatia kurudi nyuma, Misri ilidumisha kiwango cha ukuaji wa uchumi kabla ya kudorora. Badala yake, asilimia hii iliongezeka mnamo wa mwaka wa 1969 na 1970 na ilifikia asilimia 8 kila mwaka, na uchumi wa Misri uliweza, katika mwaka wa 1969, kufikia ongezeko la usawa wa biashara yake kwa mara ya kwanza na ya mwisho katika historia ya Misri, na ziada ya paundi milioni 46.9 kwa bei za wakati huo.

Uchumi wa Misri ulibeba mzigo wa kujenga upya jeshi la Misri tangu mwanzo, bila madeni ya nje.  Maduka ya Misri yalikuwa yakionyesha na kuuza bidhaa za Misri kama vile chakula, nguo, samani na vifaa vya umeme. Rais Abdel Nasser alijivunia kuwa alivaa suti na mashati ya uzi wa Mahalla, na alitumia vifaa vya umeme vya Misri (Ideal).

Ripoti ya Benki ya Dunia inafuatilia baadhi ya vipengele vya mabadiliko ya kina ya kijamii ambayo Misri ilishuhudia kati ya miaka (1952-1970): Eneo la ardhi ya kilimo liliongezeka kwa zaidi ya maraba, kwa mara ya kwanza, ongezeko la eneo la ardhi ya kilimo ilitangulia ongezeko la idadi ya watu.

Tangu nyakati za zamani, Gamal Abd El Nasser alikuwa kiongozi wa kwanza wa Misri kupanua eneo la Bonde la Nile.  Idadi ya vijana mashuleni, vyuo vikuu na vyuo vya juu imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 300.  Eneo la ardhi linalomilikiwa na kundi la wakulima wadogo liliongezeka kwa ekari milioni 2.1 hadi ekari milioni 4 hivi. Maendeleo ya ajabu yamefanywa katika uwanja wa usawa na haki ya kijamii katika miji pia kupitia ushuru.

 

Viwango duni na vya juu viliwekwa kwa mishahara, na hakuna mtu anayeishi na anasa na wala mtu yeyote anayeishi chini ya kiwango na kabla ya kifo cha Rais Abd El Nasser ulikamilishwa ujenzi wa roketi maarufu wa Misri, mipango ya usafiri na kuhariri ardhi yote ya Kiarabu na si kusonga hali, na kutokana na Rais Abd El Nasser alikubali kwa Mpango wa Rogers, mashujaa wa vikosi vya jeshi waliweza kusonga ukuta wa makombora makubwa mpaka makali ya  Suez Canal na ndege ya Israeli, mkono wake mrefu, ilifutwa katika shambulio la Misri katika Canal ya Magharibi Suez.

Kuzuka kwa vita vya ukombozi, na kuvuka kwa jeshi la Misri hadi Ukingo wa Mashariki ikawa suala la muda.  Rais Abd El Nasser alikadiria kabla ya Aprili mwaka wa 1971.  Kabla ya kifo cha Rais, aliidhinisha mpango wa Granit, ambao ni mpango wa kuvuka, ambao sehemu yake ya kwanza ilitekelezwa saa sita mchana mnamo Oktoba 6, pamoja na mpango wa 200, ambao ni mpango wa ulinzi uliohesabiwa ili kusababisha pengo katika ushirikiano muhimu kati ya jeshi la pili na la tatu la Misri.

Ni muujiza wa hatima, kuwa uvunjaji huo ulitokea kama vile mpango 200 ilivyotarajiwa, baada ya uamuzi wa kuchelewa wa Rais Sadat kuendeleza mashambulizi ya Misri.

Oktoba 14, 1973 roho yenye nguvu ambayo ni Rais Abd El Nasser ilipanda kwa muumba wake, na uchumi wa Misri ni kutoka kwa Korea Kusini, na Misri ina ziada ya sarafu ngumu inayozidi dola milioni mia mbili na hamsini, kulingana na dalili ya Benki ya Dunia. 

Na thamani ya sekta ya umma iliyojengwa na Wamisri wakati wa enzi ya Rais Abd El Nasser, kulingana na makadirio ya Benki ya Dunia, ilifikia dola bilioni 1400.

Misri ndiyo yenye msingi mkubwa wa viwanda katika Ulimwengu wa Tatu. Na idadi ya viwanda vilivyoanzishwa wakati wa enzi ya Abdel Nasser vilikuwa 1200, vikiwemo viwanda vizito, vya kuleta mabadiliko na kimkakati. Bwawa la Juu lilijengwa mradi mkubwa wa uhandisi na maendeleo katika karne ya ishirini na uteuzi wa Umoja wa Mataifa, ambao katika ujenzi wake ni sawa na piramidi 17 zilizoigwa kwa piramidi ya Khufu.  Kiwango cha wasiojua kusoma na kuandika kilipunguzwa kutoka asilimia 80 kabla ya mwaka wa 1952 hadi asilimia 50 mnamo mwaka wa 1973.

Kutokana na matumizi ya elimu  bure katika hatua zote za masomo ya bure yaliyozaa wasomi wa mfano (Ahmed Zewail, Muhammad Al-Mashad, Saeed Al-Nashai, Magdy Yaqoub, Mustafa Al-Sayed, Yahya Badir), na wengi wengine licha ya porojo zote za wapinzani wa Nasser na sera zake kabambe, na anayetaka kusoma kumbukumbu wataalamu hawa ndio bora kwa mamlaka ya Rais Abd El Nasser na enzi yake.  Umeme, maji safi, shule, vitengo vya afya na vyama vya kilimo vimeingizwa katika idadi kubwa ya vijiji vya Misri.  Na bima ya afya na kijamii na pensheni zimehakikishwa kwa karibu kila raia wa Misri.  Haya yote bila madeni, ambapo Misri, usiku wa kifo cha Rais Abdel Nasser, ilikuwa na deni la takriban dola bilioni moja, bei ya silaha zilizonunuliwa kutoka Umoja wa Kisovieti.

Sarafu ya Misri haikuunganishwa kwa dola ya Marekani, lakini Paundi ya Misri ilikuwa sawa na dola tatu na nusu, na sawa na riyal kumi na nne za Saudi kwa viwango vya Benki Kuu ya Misri.  Rais Abd El Nasser aliondoka, na paundi ya dhahabu inagharimu paundi 4 za Misri, na baada ya kuondoka kwa kiongozi huyo, Misri iliingia katika vita vya Oktoba na inatawaliwa na mifumo yote ya utawala wa Nasser.  Sekta ya umma inayoongoza maendeleo ya jeshi la Misri lililojengwa na Abd El Nasser baada ya kushindwa.  Ukuta wa kombora ambao Abd El Nasser alihamia kwenye ukingo wa mfereji kabla ya kifo chake na mipango ya kijeshi iliyowekwa tangu utawala wake.

Alichokifanya Rais Gamal Abd El Nasser hakikuwa muujiza au kitu cha ajabu.  Badala yake, hilo ni jambo la kawaida kwa nchi kama Misri, na Mungu aijaalie faida, uwezo na mali zote kuwa nchi kubwa.  Nafasi ya fikra, uwezo na mali ya Misri ilichanganyikana na uzalendo, nia na maoni ya Rais Gamal Abd El Nasser ya mustakabali kwa ajili ya Misri, jambo lililopelekea mafanikio hayo yote yaliyotokea mnamo kipindi kifupi, kisichozidi miaka 18, kilichogubikwa na njama na vita vingi ili kukomesha mradi wa Nasserist.

Kwa kifo cha Rais Abd El Nasser, na mapinduzi yaliyotokea katika sera za Misri baada ya Vita vya Oktoba 1973, majembe ya ubomoaji yalianza kupiga jengo kubwa la urithi wa Rais Gamal Abd El Nasser nchini Misri.

Marejeleo:

Kitabu cha (Abd El Nasser aliihukumuje Misri) Abdullah Imam.

Kitabu cha (Kwa Misri si kwa Abd El Nasser) Muhamed Hasanein Hekal.

Kitabu cha ( Faili za Suez) Muhamed Hasanein Hekal.

Kitabu cha (Wizi ya tatu kwa Misri) Saad El Din Wahba.

Kitabu cha (Abd El Nasser) Robert Stephnes.. Muhamed Uda.

Kitabu cha (Gamal Abd El Nasser) Agrashif.

Kitabu cha (Binadamu ni Msimamo...) Mahmoud Amin El Alem.

Kitabu cha (Kumbukumbu ya Sami Sharaf) Sehemu ya 1,2.

Kitabu cha ( kwanini kuanguka baada ya Abd El Nasser)Adel Hussen.

Kitabu cha (Nini kilichotokea pamoja na Wamisri) Galal Amin.

Ripoti za Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia zilizotajwa hapo juu.

Sura moja ya kitabu cha (Vita vya Naseria.... Utafiti mpya katika Historia ya kisasa): Amr Sabeh,Chapisho la kwanza 2011.