Abd El Nasser na Mauritania
Maandishi ya : Amr Sabih
Kituo cha kiutamaduni cha kimisri huko Mauritania ndio vituo vya kiarabu kongwe zaidi huko Mauritania, na hadithi ya kuanzishwa kwake ilirejea ujumbe kutoka kwa Rais wa kwanza wa Mauritania baada ya Uhuru Bwana Al-Mukhtar Ould Daddah - aliutumia mnamo 1963 kwa Rais Gamal Abd El Nasser, kuomba kutoka kwake aingilie ili kuokoa utambulisho wa kiarabu kwa Mauritania unaokabili hatari ya kuondoa, ikiwa Misri haichukui hatua kulingana na nafasi yake ya kitamaduni na kistaarabu ili kuhifadhi Uarabu wa Mauritania.
Gamal Abd El Nasser alijibu na kuamuru kuanzishwa kwa jukuwa kubwa la kitamaduni la kimisri huko Mauritania kutetea Uarabu wa Mauritania, na kituo hicho kilipewa maktaba ya vitabu 20,000 katika taaluma tofauti ambapo ilikuwa maktaba kubwa zaidi katika nchini Mauritania.
Mnamo Februari 6, 1964, Rais wa Mauritania, Mukhtar Ould Daddah, akazindua Kituo cha kiutamaduni cha kimisiri, na mshairi mkubwa wa Mauritania Ahmadou Ould Abdel Qader Qaida alitoa shairi lililoitwa "Nuru ya Mashariki" kwa ajili ya kukisifu kituo hicho na lengo la kuwepo kwake.
Kituo hicho kilikuwa na shauku ya kuwapa wanafunzi wa Mauritania shahada ya kwanza sawa na cheti cha kimisri, na Misri iliendelea kupokea kila mwaka kundi la kielimu kutoka Mauritania, na wakati mshairi mkubwa wa Mauritania "Shagali Ahmed Mahmoud" aliandika shairi akiisifu Misri, na Rais Abd El Nasser akaisoma, akamwita mshairi huyo mchanga kuja Misri, na akatoa nafasi ya kusoma nchini Misri kwake, na kwa kweli Shaghali alisoma huko Misri kwa miaka miwili katika Kitivo cha Mafunzo, Chuo Kikuu cha Ain Shams.
Baada ya Rais El Sadat kutia saini Mkataba wa Amani na Wazayuni ,Kituo cha kiutamaduni cha kimisri kilifungwa kwa miaka kadhaa kisha kufunguliwa tena wakati wa Rais Mubarak.
Kituo cha kitamaduni cha kimisri kiliendelea kutoa mafunzo kwa watu wa Mauritania katika nyanja zote na kuwapa Ruzuku za kielimu nchini Misri, hadi jambo hilo mnamo miaka ya themanini iliyopita lilifikia kwa kuunda serikali ya Mauritania ambapo mawaziri wake wote walikuwa wahitimu kutoka vyuo vikuu vya Misri.
Miaka 55 baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha kiutamaduni cha kimisiri nchini Mauritania kwa amri ya Rais Gamal Abd El Nasser, serikali ya kisasa ya Mauritania iliamua kurudisha chema hicho kwa Misri, kwa hivyo katika mitaa ya mji mkuu wa Mauritania Nouakchott hakukuwepo mtaa ambao jina lake linaweza kubadilishwa isipokuwa Barabara ya Gamal Abd El Nasser .
Pamoja na kila kitu, Gamal Abd El Nasser bado ana macho mbali na anajua umuhimu wa ushawishi wa kimisri katika uwanja wake muhimu kwa ulimwengu wake wa Kiarabu, bara lake la Afrika na ulimwengu wake wa Kiisilamu, na hakufanya makosa wakati alipoitikia mwito wa Mauritania wa kuhifadhi kitambulisho cha kiarabu cha Mauritania, na kwa hakika hakuwa akingojea au kutafuta kuita mtaa kwa jina lake.
wazungu na wafuasi wao hawasahau maadui yao, na Abd El Nasser kama alama ya mradi wa kitaifa na piganaji mkali zaidi wa ukoloni wa zamani na mpya wa Magharibi, baada ya karibu nusu karne ya kifo chake bado kuna jaribio la kuangamiza na kutokomeza yote yanayomwakilisha, kwa sababu kuwepo kwake tu, hata jina la mitaani, linaweza kuhamasisha wengine kwa dhana ya kupinga Na kudharauliwa na kupambana ukoloni.
Gamal Abd El Nasser alikuwa akisoma siku za usoni wakati alisema mnamo 1968:
"Wamarekani na wafuasi wao hawatanisamehe kwa kile nilichofanya nao ... nikiwa hai au maiti."
Baada ya zaidi ya miaka 50 ... hawajasahau ... hawajasamehe ... wala hawatasamehe.
Mkusanyiko wa picha nadra sana kutoka kwa matembezi ya kiongozi wa Mauritania Mukhtar Ould Daddah kwenda Kairo mnamo Machi 1967 na kupokea Uzamivu wa heshima kutoka Al-Azhar tukufu na mahudhurio yake kwa mikutano pamoja na Rais Gamal Abd El Nasser, na kikundi kingine wakati wa mapokezi ya Rais Nasser kwake kwenye uwanja wa ndege ili kuhudhuria Mkutano wa kutopendelea Oktoba 3, 1964, na Ziara ya Oktoba 1967. , Na matembezi ya Novemba 7, 1968.