Kumbukumbu ya miaka 54 ya Uhuru wa Ufalme wa Uswazi

Mnamo siku kama hii – Septemba 6, 1968 - Uswazi ilipata uhuru wake kutoka kwa Uingereza.
Basi, tangu miaka ya thamanini ya karne ya kumi na tisa, Matarajio ya Uingereza na Uholanzi kudhibiti Uswazi na Tamaa yao ya kupata Maadini na dhahabu nchini humo yalikuwa yameanza. Mnamo 1902, vita vilitokea kati ya Waingereza na Waholanzi, ambapo Waingereza walishinda na waliweza kudhibiti Uswazi peke yao.
Hatua ya Uswazi kuelekea Uhuru ilianza wakati wa kupitishwa kwa katiba ya kwanza ya nchi hiyo mnamo 1964, wakati ambapo Uingereza ilikabidhi mamlaka kwa watu wa Uswazi mnamo 1967 na Uswazi ilipata Uhuru wake mnamo Septemba 6, 1968.
Ikumbukwe kuwa Mfalme wa Uswazi, Miswati wa tatu mnamo 2018, aliamua kubadilisha jina la nchi yake kuwa "E Swatini" pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya hamsini, ambayo pia ni kumbukumbu ya Uswazi ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru.