Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika kikao cha kufunga Mkutano wa Bandung mwaka 1955

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika kikao cha kufunga Mkutano wa Bandung mwaka 1955

 

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky

Mkutano wetu unafikia mwisho baada ya majadiliano ya karibu yenye manufaa ambayo yalidumu kwa muda wa siku nane, siku hizi nane zilitanguliwa na maandalizi na juhudi kubwa zilizofanywa na sekretarieti ya pamoja ya mkutano huo, kwa kweli zilikuwa na manufaa makubwa. 

Hakuna shaka kwamba mkutano wetu umepata mafanikio makubwa; kwani Amani na Ushirikiano wa kimataifa utafaidika sana na mshikamano na maelewano yanayodhihirishwa na maamuzi yake, na kwamba sababu ya Amani itapata msukumo mkubwa kutokana na kujali kikubwa na uungaji mkono kamili unaooneshwa na nchi zote za Asia na Afrika kuhusiana na suala la haki za binadamu, na haki ya kuweka hatima.

 Sifa nyingi za mafanikio ya mkutano huo ni kutokana na juhudi binafsi za Mkuu wa Mkutano huo, Mheshimiwa “Ali Sastro Amidjogo”,  pamoja na uzoefu na ustahimilivu  wake mrefu,  vilevile roho ya wanachama wote wa ujumbe - iliyokuwa na sifa za ustahimilivu  mrefu,  na hamu ya upatanisho ilisaidia kufanya majadiliano yetu kuchukua njia ya kujenga katika nyakati ambazo ilionekana kuepukika kwamba kutokubaliana kungetokea.

Naishukuru serikali ya Indonesia kwa ukarimu wake ambao imeuonesha, na nchi zinazoalika mkutano huo kwa kuchukua hatua ya kwanza kuelekea kuufanya.