Tarehe Agosti 10, 1809 ... Kilio cha kwanza kwa uhuru wa Jamhuri ya Ekuador

Tarehe Agosti 10, 1809 ... Kilio cha kwanza kwa uhuru wa Jamhuri ya Ekuador

Imetafsiriwa na/ Abdelrhman Mohamed
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Mnamo tarehe Agosti 10, Baraza la Kijeshi la Libertarian ya Quito lilisaini sheria inayotangaza kwamba Ecuador sio tena ya Dola ya Hispania.

Mnamo Agosti 11, Baraza la Kijeshi lilikutana, siku tano baadaye, mnamo Agosti 16, na likatangaza rasmi hatua zinazodai uhuru wa Jamhuri ya Ecuador. Wakati "Mapinduzi ya Quito" yalipoanza kukua na kuanza kuwa na athari, viongozi wote wa Baraza walikamatwa hatua kwa hatua na kuondolewa.

Baada ya mwaka mmoja, mnamo Agosti 2, 1810, wanajeshi na wafuasi wa Baraza lililotajwa hapo juu waliingia katika kambi za kijeshi kutafuta makamanda waliokamatwa, na kusababisha mauaji ambayo mateka wote waliuawa, wakati huo iliyoitwa "Mauaji ya Agosti 10".

"Mapinduzi ya Quito" mnamo Agosti 10 kwa hivyo yalijulikana kama "Kilio cha Kwanza cha Uhuru" kama hatua ya awali iliyosababisha uhuru kamili.

Mwishowe, tunapaswa kuwashukuru wale ambao hawakusita kujitolea kwa uhuru na kuangazia njia ya uhuru kwa kutoa roho zao.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy