Kumbukumbu ya Kifo cha Mpiganaji Shujaa na Mwanamapinduzi "Che Guevara"

Kumbukumbu ya Kifo cha Mpiganaji Shujaa na Mwanamapinduzi "Che Guevara"

Imetafsiriwa na/ Malak Hazem
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

"Maisha ni neno na mtazamo... Wazungu hawaandiki historia... Historia imeandikwa na wale wanaopenda nchi, waliongoza mapinduzi ya ukweli na waliwapenda maskini" (Che Guevara) 

Miaka 55 iliyopita, mnamo tarehe Oktoba 8, 1967, Che Guevara alikamatwa na CIA kwa msaada wa majeshi ya Bolivia katika misitu ya Bolivia, ambapo aliongoza wanamapinduzi wa Bolivia na Cuba katika mapambano ya kuikomboa nchi kutoka kwa unyonyaji wa kibepari na kibeberu... Siku iliyofuata, mnamo tarehe Oktoba 9, 1967, aliuawa. 

Neno la Kihispania "Guerillero Heroico" linamaanisha picha ya ishara ya Guevara, iliyochukuliwa na Alberto Corda mnamo mwaka 1960, inayomaanisha kwa Kiarabu "Mwanamapinduzi Shujaa" na imechukuliwa kuwa picha maarufu zaidi ulimwenguni. 

Ni vyema kutajwa kuwa Hayati Rais Gamal Abdel Nasser alikutana mara mbili na shujaa wa Mwanamapinduzi Shujaa Guevara, na katika barua ya Guevara kwa Gamal Abdel Nasser, alisema kwamba alivutiwa na ujasiri na uthabiti wa askari wa Misri katika kufukuza Uingereza, Ufaransa na Israeli wakati wa uchokozi wa tatu dhidi ya Misri, na kwamba hii iliathiri vyema Wacuba walioasi dhidi ya "Batista" mnamo mwaka 1956, kwani uzoefu wa Misri ulikuwa nguvu ya kiroho kwa wacuba kukabiliana na vikwazo katika vita vya msituni  walivyopigana vilimani...

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy