Shughuli za Siku ya Pili ya Ziara ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Jamhuri ya Tanzania mnamo mwaka 1966

Shughuli za Siku ya Pili ya Ziara ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Jamhuri ya Tanzania mnamo mwaka 1966
Shughuli za Siku ya Pili ya Ziara ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Jamhuri ya Tanzania mnamo mwaka 1966
Shughuli za Siku ya Pili ya Ziara ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Jamhuri ya Tanzania mnamo mwaka 1966
Shughuli za Siku ya Pili ya Ziara ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Jamhuri ya Tanzania mnamo mwaka 1966
Shughuli za Siku ya Pili ya Ziara ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Jamhuri ya Tanzania mnamo mwaka 1966

Imetafsiriwa na: Engy Mohammed
Imehaririwa na:  Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Asubuhi ya Ijumaa, tarehe Septemba 23, 1966, majadiliano rasmi yalianza kati ya Rais Abdel Nasser na Rais Julius Nyerere kuhusu uhuru wa wakati huo pamoja na njia za kuimarisha Umoja wa Afrika. 


Majira ya mchana, Rais Julius Nyerere alifuatana na Rais Gamal Abdel Nasser hadi Makao Makuu ya Chama cha TANU (Tanganyika African National Union), chama cha umoja wa kitaifa wa Tanzania, kuhudhuria sherehe za kumkaribisha Mheshimiwa Rais Nasser. Wanachama wa chama hicho walimpokea kwa shangwe na vifijo, huku wakazi wa mji mkuu, Dar es Salaam, wakiwa wamekusanyika mbele ya makao makuu ya chama. 

Marais hao wawili waliposhika nafasi zao kwenye jukwaa kuu, wananchi walianza kucheza ngoma za jadi wakiwa wamevalia mavazi ya kitaifa kwa mwendo wa muziki huo. Viongozi wa chama walimkaribisha Rais Nasser kama mpiganaji shujaa aliyepambana na ukoloni na kutetea haki za watu waliodhulumiwa kwa ujasiri. 

Kisha, wanachama wa chama walimkabidhi Rais Nasser ngao, mkuki, na vazi la kitamaduni kama ukumbusho wa watu wa Tanzania.

Marais hao wawili walielekea katika Chuo Kikuu Kipya kilichoanzishwa jijini Dar es Salaam. Walipofika, walipokelewa kwa uchangamfu na ufasaha na rais wa chuo kikuu pamoja na washiriki wa kitivo. Wakati wa ziara yao, walifahamu vyuo na idara mbalimbali za chuo hicho. Rais Gamal Abdel Nasser alitoa hotuba, ambayo maudhui yake yalikuwa kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Rais... Mabwana:

Ni fursa adhimu leo tunapokiona chuo hiki kipya cha Dar es Salaam, na ninaamini kuwa tangu muda mfupi tuliokuwa hapa, ni msingi imara wa elimu ya juu nchini Tanzania. Ninaamini kuwa hiki ni njia ya haki na sahihi, kwa sababu katika kazi zetu za maendeleo, tutahitaji idadi kubwa ya mafundi. Tumeingia katika uzoefu huu katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, na kila mwaka tunaamini na tunapanga kwamba tutaridhika na wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini baada ya miaka mitano tunagundua kwamba tunahitaji kuongeza fani kwa wanafunzi wengi zaidi. 

Nakaribisha mwaliko wa ushirikiano kati ya vyuo vikuu vyetu na Chuo Kikuu chenu cha Dar es Salaam, na nachukua fursa hii kuwaalika wajumbe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutembelea vyuo vyetu vya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu. 

Ama Chuo Kikuu cha Al-Azhar, tulikiendeleza miaka minne iliyopita. Hapo awali, kilikuwa kikizingatia mafundisho ya sayansi za kidini tu, lakini tulikiendeleza ili mwanafunzi aweze kusoma dini na uhandisi, au dini na tiba, na sayansi nyingine mbalimbali. Tulitenga vyuo viwili; Chuo cha Sharia na Chuo cha Lugha ya Kiarabu. Hivyo basi, wanafunzi wanapata fursa ya kufanya kazi katika nyanja mbalimbali badala ya kuwa wasomaji wa misikitini au wataalamu wa masuala ya kidini pekee kama mashekhe.

Katika Msikiti wa Al-Azhar, kuna idadi kubwa ya wanafunzi kutoka nchi mbalimbali, na wanaporudi katika nchi zao, hakuna faida kamili kwa nchi zao, kwa sababu walikuwa wataalamu wa dini, wakati ambapo nchi zao zilihitaji wataalamu wa shirika, usimamizi, uhandisi, na matawi mengine. Sasa hawa wanafunzi wanasomea udaktari, uhandisi, usimamizi na mambo haya yote. Vyuo vikuu vyetu mbalimbali vina wanafunzi 25,000 kutoka nchi za Afrika, Asia, na Kiarabu, na hii inasaidia kubadilishana utamaduni na ushirikiano kati ya nchi za Kiarabu, Asia, na Afrika.

Kuhusu ushirikiano na Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ninathibitisha kwamba Chuo Kikuu cha Al-Azhar kiko tayari kushirikiana katika masomo ya Kiislamu na kukupatia vitabu vyote utakavyohitaji. 

Nakushukuru kwa ukarimu nilioupokea, na ninakitakia chuo kikuu chako kipya kila la heri katika maendeleo.

Kwa picha zaidi, bonyeza hapa.