Hitimisho la Ziara ya Rais "Gamal Abdel Nasser" kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mnamo mwaka 1966
Imetafsiriwa na: Alaa Yaheia
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Asubuhi ya tarehe Septemba 29, 1966, Rais "Nyerere" aliandamana na Rais "Gamal Abdel Nasser" kwenda kwenye Taasisi ya Kitaifa na Bunge. Wanachama wa taasisi hiyo waliwakaribisha viongozi hao wawili kwa makofi makubwa walipowasili kwenye jukwaa. Rais "Gamal Abdel Nasser" alitoa hotuba iliyogusia masuala ya kitaifa na ya Afrika, akizungumzia pia juhudi za bara la Afrika kupata uhuru. Alisema:
"Mheshimiwa Rais",
Nataka kutoa shukrani zangu za dhati kwa fursa hii iliyotolewa na Bunge lenu tukufu katika hitimisho la ziara yangu. Nimefurahishwa sana na ziara hii nchini Tanzania, ambako nimepata nafasi ya kukutana na idadi kubwa ya raia wenu. Nimeona kwa macho yangu juhudi zenu za dhati za kujenga maisha mapya bora, yenye uhuru wa kweli katika Afrika."
Enyi Ndugu:
Leo nilijivunia kusimama mbele ya viongozi wakuu, waheshimiwa wa Watanzania, wanaoakisi matumaini na azma yao ya kufikia uhuru wa kisiasa na kijamii, pamoja na umoja katika uwanja wa kimataifa na Afrika. Uhuru wa kisiasa na kijamii kwa kila nchi ya Afrika na umoja wake katika kimataifa na kifikra ni nguzo muhimu za maandalizi mazuri na misingi ya ulinzi ili kuchukua hatua kwa uhuru mkubwa zaidi na umoja mkubwa kwa ajili ya Afrika kubwa inayokabiliwa na changamoto. Daima, katika Muungano wa Jamhuri ya Misri, tumekuwa tukithamini juhudi zenu za kufanikisha uhuru wa kila upande na umoja kwa misingi ya dharura.
Ninawahakikishia kwamba ziara hii inatupa furaha kubwa na inaimarisha imani yetu katika uwezo wenu wa kuhakikisha malengo yenu chini ya uongozi wa mpiganiaji na kiongozi shupavu, "Julius Nyerere." Huyu ni mwanamapinduzi mwaminifu kwa Tanzania, Afrika, na ubinadamu. Hivyo basi, ziara hii inathibitisha imani yetu kwa jukumu mnaloendelea kulitekeleza katika kufanikisha malengo ya harakati za mapambano ya Afrika, ambapo mji mkuu wenu, "Dar es Salaam," umechukua nafasi kama kituo muhimu cha harakati za ukombozi wa Afrika. Haya yote yatasaidia katika kutekeleza majukumu yenu kwa kujitolea.
Ucheleweshaji wa raia wenye ufahamu mkubwa wanajua kwa imani kwamba majukumu na kujitolea wanayobeba ndiyo njia pekee ya kufikia kesho wanayoitamani. Watu wa Afrika hawakuweza kuvumilia ucheleweshaji mrefu waliolazimishwa nao na utawala wa kikoloni na ukandamizaji bila kujua umuhimu wa majukumu na kuwa tayari kwa kujitolea. Hata hivyo, kuna sheria ambazo tunapaswa kuzizingatia katika suala la kupinga na kuondoa ukoloni:
Kwanza: Ukoloni hauendani na maadili yoyote ya kibinadamu, na hii ni tusi kwa dhamira zetu na uwepo wetu.
Pili: Ubaguzi wa rangi sio tu tusi kwa bara letu na ustaarabu wa binadamu katika karne ya 20, bali pia ni aina ya ukoloni, na unaonesha sura yake mbaya zaidi.
Tatu: Tamaa ya Umoja wa Afrika haiwezi kufikiwa katika hali halisi hadi ukombozi ukamilike.
Nne: Uwepo wa nguvu za kikoloni kwenye ardhi ya bara letu ni tusi kubwa na wazi kwa nchi zetu na ndoto zetu. Kwa hivyo, tunapounga mkono na kusaidia harakati za ukombozi nchini Msumbiji, Angola, na Rhodesia, na tunapopinga ubaguzi wa rangi, tunafanya hivyo kwa kuongozwa na maadili makubwa ambayo raia wetu wanayaamini, na wakati huohuo kwa ajili ya usalama na maisha yetu.
Raia huru hawasiti mbele ya njia ngumu na ndefu kwa sababu wanaamini kwamba njia hii inawaongoza kwenye maadili makubwa na matumaini yetu.
Njia ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni yenye changamoto, na inahitaji uwajibikaji na kujitolea pande zote mbili, lakini katikati yake kuna vikwazo. Tumekuwa tukichelewa sana kufaidika na hali hii, inatuhitaji rasilimali nyingi za kifedha, kibinadamu, na kiteknolojia, ambazo si rahisi kupatikana kwa wakati huu, hasa baada ya maendeleo yanayoambatana na hatari ya nyuklia. Hii inatishia kazi yetu ndani ya nchi kwa njia zinazowekwa chini ya shinikizo kubwa, ambalo linaweza kuwa la siri au la wazi, kama vile shinikizo za kisiasa, kiuchumi, kibinafsi, na kijeshi katika nyakati tofauti.
Kushiriki katika masuala ya dunia -ambayo ni haki na wajibu wetu- kunatuweka dhidi ya wale wanaopinga wito wa amani unaosimamia haki, hata wakati unatolewa kwa msimamo wa kutokupendelea upande wowote. Kwa dhati, tunajaribu kuepuka kulazimisha binadamu kukabiliana na uchaguzi mgumu, kama ilivyokuwa nchini Vietnam, ambapo sera za nguvu zilitumika bila kuzingatia matokeo yake. Hata hivyo, hali hiyo inaweza kutufundisha mengi na kuongeza uzoefu wetu katika kuelewa uhusiano wa karibu na wa asili kati ya mapambano ya uhuru wa kisiasa na kijamii ndani ya nchi yoyote na mapambano hayo hayo nje ya nchi.
Vita vya uhuru ni kimoja, na ushindi wa uhuru mahali popote ni kuimarisha uhuru kila mahali. Vilevile, kuondolewa kwa nira ya ukoloni kutoka kwa shingo ya taifa lolote ni pumzi mpya kwa kila taifa ambalo bado linapigania uhuru dhidi ya ukoloni huo. Adui tunayempinga anaelewa ukweli huu, na ndio maana kuna umoja kati ya nguvu za ukoloni wa zamani na mpya, kati ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na kati ya wote wanaochukia uhuru na umoja wa Afrika. Huu ndio umoja unaounganisha mabaki ya milki zilizoporomoka na njama za ukoloni mpya unaoendelea, utawala wa kibaguzi wa "Ian Smith", na udikteta usio na huruma wa Afrika Kusini pamoja na ukoloni mkali wa Ureno.
Umoja huu unagawanya majukumu kati ya washirika wake; wakati Uingereza inadanganya umma wa dunia na kumwezesha utawala wa "Ian Smith" kutangaza uhuru wa upande mmoja unaopingwa na wengi wa Waafrika nchini Rhodesia, ukoloni mpya unajaribu kuingia kwa siri kwa kutumia njama na ugaidi katika maeneo mapya. Kwa upande mwingine, serikali ya Afrika Kusini inajaribu kudumisha ukoloni wake nchini Afrika Kusini Magharibi, na Ureno inazidi kuwa katili dhidi ya vyama vya uhuru wa kitaifa katika makoloni yake. Zaidi ya hayo, kuna juhudi za kutilia shaka Shirika la Umoja wa Afrika kwa kila njia.
Tukabiliane na umoja huu na washirika wake. Funzo la mapambano linatufundisha kuunganisha nguvu zetu, kupigana kwa mkakati mpana, kuhimili changamoto, na kujaribu kuhamasisha nguvu zote zinazopenda uhuru na zinazoamini kuwa hakuna amani pale ambapo kuna ukoloni na unyonyaji. Afrika ni nguvu kubwa zaidi kuliko wanavyofikiria maadui wa uhuru wa Afrika na umoja wake. Ni nguvu kubwa zaidi kuliko wale waliotajwa na Rais Julius Nyerere katika hotuba yake jana, ambao walionyesha shauku ya tuhuma kwa ukaribu kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na kuogopa kwa sababu wanaona hili kama ushahidi wa nia ya kushirikiana, ambayo haijumuishi nchi hizi mbili tu, bali pia inahusisha nguvu kubwa za mapinduzi zilizokomaa barani, zikingoja na kujibu mashambulizi. Bila shaka, wanaamini kuwa wakati ujao ni wao, ni wa uhuru na umoja.
Ikiwa baadhi ya watu wanaona kuwa sauti zinazonyamazishwa au zile zinazojitokeza mara kwa mara ni ishara ya kushindwa kwa Afrika, basi watu hao wako kwenye makosa. Sauti kama hizo ni za kawaida katika hatua za mabadiliko makubwa katika maisha ya mataifa. Hata kama kuna maneno yanayosemwa kuhusu madhara yake, sauti hizi husaidia kufafanua masuala ya mapambano, kuongeza mvuto wake, na kutenganisha kati ya wale wanaoweza kufanya mapinduzi na kubeba mizigo yake na wale ambao hawawezi kufanya zaidi ya kutoa mazungumzo. Afrika haitaweza kufikia malengo na matumaini yake isipokuwa kwa kufanya kazi pamoja, kwa mapinduzi yanayosukuma masuala yake mbele, bila kuyumbisha au kuyazuia kutokana na majaribio ya kufikia makubaliano na kushikilia utaratibu wa zamani.
Hata hivyo, hali hii haipaswi kuathiri Shirika la Umoja wa Afrika, kwa sababu shirika hili ni matumaini makubwa ambayo Afrika imeweza kuyapata baada ya mateso na subira ya muda mrefu. Hatupaswi kulitarajia Shirika la Umoja wa Afrika lifanye zaidi ya uwezo wake katika hali na mazingira yake.
Shirika hili linaonyesha hali na mazingira ya kuendelea kwa mapambano, na huo ni ukweli ambao tunapaswa kuukubali na kuuthamini. Ikiwa tunadhani kwamba shirika hili linaonyesha ushindi wa mwisho wa Afrika, basi hatutendi tu ukatili kwa hali halisi ya Afrika bali pia tunadhulumu mapambano ya Afrika yenyewe. Hata hivyo, ni muhimu kwamba wale wanaoweza kuchukua hatua, wale wanaoweza kubeba jukumu la mapambano, waanze kuchukua hatua.
Msimamo wa Tanzania wa kuunga mkono harakati za ukombozi wa mataifa ya Afrika na kuifanya Dar es Salaam kuwa mji mkuu wa shughuli za ukombozi wa Afrika nzima, hata kabla ya kupewa jukumu hilo rasmi na Shirika la Umoja wa Afrika, ni mfano bora wa uwezo wa kuchukua hatua. Mfano huu, licha ya hatari zote zinazouzunguka, ni usemi wa kweli zaidi wa Afrika kuliko mazungumzo yote ya kidiplomasia yanayofanyika chini ya mwangaza wa propaganda au ndani ya vyumba vilivyofungwa.
Enyi Ndugu
Siamini kuwa nitakuwa nikisema jambo jipya mbele yenu nikieleza kwamba watu wa Misri wanakubaliana nanyi katika falsafa ya mapambano ya ujumla, yaani kuunganisha uhuru wa kisiasa na uhuru wa kijamii, na pia kuunganisha mapambano ya ndani ya mipaka ya taifa na yale yanayotokea nje ya mipaka hiyo. Lakini, nasema bila kujivuna kwamba mapambano ya watu wa Misri yamefanyika katika mazingira magumu na yenye hatari kubwa. Watu wetu ni sehemu ya taifa la Kiarabu linaloishi katika eneo lenye umuhimu mkubwa wa kimkakati na kiuchumi, kwani liko kwenye makutano ya njia za bahari na anga za dunia, na ardhi yake inashikilia utajiri mkubwa wa mafuta unaojulikana na kuthibitishwa.
Ukoloni umetumia mbinu mbalimbali kuweka na kuimarisha utawala wake. Uligawanya taifa la Kiarabu, ambalo limeishi kwa maelfu ya miaka katika ardhi moja, na historia moja, na ambalo linasema lugha moja. Hii ilisababisha umoja wa maslahi, umoja wa akili, na umoja wa dhamiri kuvurugwa. Ukoloni ulijichimbia mizizi katika ardhi hiyo kwa kutawala kwa nguvu za kijeshi moja kwa moja.
Kabla ya mapinduzi ya Misri, kwa mfano, kulikuwa na wanajeshi elfu nane wa Uingereza katika Kituo cha Suez pekee, waliolenga kuanzisha tabaka la ndani lililoshirikiana nao katika unyonyaji, na ambalo kwa upande wake lingeweza kuwalinda. Labda mnajua kwamba asilimia 50 ya kipato cha taifa cha Misri kilikuwa chini ya udhibiti wa asilimia nusu ya wakazi wa Misri, wengi wao wakiwa wageni. Baada ya hapo, ukoloni ulipanga njama dhidi ya watu wa Kiarabu huko Palestina, ambayo haikuwa tofauti sana na ile mnayoiona karibu nanyi huko Rhodesia, ambapo wachache wa nje wanachukua ardhi ya Palestina kwa misingi ya ubaguzi wa rangi na kwa msaada wa ukoloni. Wanawafukuza wakazi wa asili kutoka kwenye nyumba zao na kuanzisha utawala wa ugaidi ambao hauwezi kuishi katikati ya wingi wa Waarabu isipokuwa kwa msaada wa ukoloni na kutegemea kabisa ulinzi wake.
Watu wa Misri walianza kwa kupindua utawala wa tabaka linalonyonya, wakapiga mashambulizi dhidi ya majumba ya wakulima wakubwa na mitaji iliyooza, na kusukuma umiliki wa mali za taifa kuwa mikononi mwa nguvu za wafanyakazi na watu. Ardhi iligawanywa kwa wakulima, benki, biashara ya nje, na viwanda vikubwa vilitaifishwa. Wafanyakazi walishiriki katika usimamizi wa vitengo vya uzalishaji na kugawana faida, na ushirika wa uzalishaji na matumizi ulianzishwa na kupanuka. Wakati huo huo, elimu ilifanywa kuwa ya bure, na udhamini ulitolewa kwa raia wa Misri. Pia, ilianzishwa kikomo cha masaa ya kazi kuwa saa saba kwa siku, kuliwekwa mishahara ya chini kabisa, na kutekelezwa bima ya afya kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na matibabu, bima dhidi ya ulemavu, uzee, na ukosefu wa ajira. Uhuru wa kijamii uliandaa njia kwa ajili ya kujenga uhuru wa kisiasa juu ya misingi imara ya kidemokrasia.
Kwa hivyo, nguvu za wafanyakazi wa watu, zilizoungana katika umoja wa kijamaa, ziliudhihirisha udemokrasia wao haraka juu ya magofu ya udikteta wa tabaka linalonyonya, na mfumo wake wa kisiasa ambao ulibomoka mbele ya mapinduzi. Ili kuimarisha mafanikio haya, ilihitajika kukuza uwezo wa uzalishaji. Miradi ya kukuza kilimo na viwanda ilienda sambamba na upanuzi wa udhibiti wa watu juu ya vyombo vya uzalishaji, pamoja na upanuzi wa huduma za kijamii. Watu wa Misri hadi sasa wamewekeza zaidi ya pauni bilioni moja katika viwanda, na katika mpango mpya wameanza kuongeza bilioni nyingine 1.5, wakilenga hasa kujenga msingi wa viwanda vizito nchini Misri. Katika uwanja wa kukuza kilimo, rafiki yangu Rais Nyerere alizungumza kwa muda mrefu kuhusu mradi wa bwawa kuu siku ya kwanza alipowasili nchini mwenu.
Enyi Ndugu
Hakuna ushahidi mkubwa zaidi wa uhusiano kati ya uhuru wa kisiasa na uhuru wa kijamii, na kati ya mapambano ndani ya mipaka ya taifa na yale yanayotokea nje ya mipaka, kuliko hadithi ya ujenzi wa bwawa kuu. Nguvu za ukoloni zilikuwa zikijaribu kuzuia mipango yetu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ambapo mradi wa bwawa kuu ulikuwa sehemu muhimu. Wakati Mfereji wa Suez, ambao uliokuwa kituo cha kipekee cha Misri, ulileta mapato ya kila mwaka ya pauni milioni arobaini kwa kampuni ya ukiritimba ya kimataifa, nguvu za ukoloni zilituwekea vikwazo na kukataa kutukopesha fedha kwa masharti ambayo tungeweza kutumia kujenga bwawa kuu. Wakati watu wa Misri walipoanza kudai haki yao iliyoporwa kwa kuitaifisha Kampuni ya Kanal ya Suez na kutumia mapato yake kuwekeza katika mipango ya maendeleo, nguvu za ukoloni ziliwashambulia – katika siku kama hizi miaka kumi iliyopita – zikizindua vita dhidi yao kwa njia ya ardhini, baharini, na angani.
Watu wa Misri walisimama na kupigana, na mataifa ya bara la Afrika na Asia yaliwaunga mkono, hata yale ambayo bado yalikuwa chini ya ukoloni wazi. Vilevile, dhamiri ya ulimwengu iliamka, na nguvu kubwa zinazopenda amani ziliunga mkono. Matokeo yake ni kwamba uvamizi wa mataifa matatu – Uingereza, Ufaransa, na Israeli – ulishindwa vibaya, na watu wa Misri wakashinda. Ushindi huu haukuwa wa watu wa Misri pekee bali ulikuwa na athari kubwa, hasa katika bara hili kubwa.
Enyi Ndugu
Watu wenu wakubwa wamekusanya uzoefu wao katika kauli mbiu yenye msukumo ya mapinduzi yenu "Uhuru na Umoja." "Uhuru" ni neno linalomaanisha uhuru katika lugha ya Kiarabu, na "Umoja" ni neno linalomaanisha umoja. Hivyo, maneno haya mawili yana asili moja. Kauli mbiu za mapambano zinatunganisha kile kilichopo kati yetu na malengo ya mapambano.
Natoa shukrani kwako, Mheshimiwa Rais, na pia kwenu - ndugu zangu - wanachama wa taasisi ya kimataifa. Na Al-Salaam Alaikum na rehema zake.
Baada ya mchana, mazungumzo kati ya marais "Nyerere" na "Nasser" na wajumbe wao yaliendelea. Mazungumzo hayo yalithibitisha haki ya Palestina juu ya ardhi yake iliyochukuliwa kwa nguvu, umuhimu wa kudumisha amani nchini Vietnam, na kuunga mkono mataifa yanayopigania uhuru wao. Wajumbe wote wawili walilaani sera za ubaguzi wa rangi nchini Indonesia na Afrika Kusini, na wakasisitiza umuhimu wa kushikamana na mkataba wa Umoja wa Mataifa. Vile vile, pande zote mbili zilibadilishana zawadi za kumbukumbu.
Usiku, Rais "Jamal Abdel Nasser" aliandaa karamu ya chakula cha jioni kumheshimu Rais "Julius Nyerere" na mkewe kama ishara ya kumalizika kwa ziara yake rasmi nchini Tanzania. Walioalikwa kwenye hafla hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais, ujumbe uliomfuata, na wanachama wa jamii ya Kiarabu pamoja na watu mashuhuri.
Rais "Julius Nyerere" alimpeleka Rais "Jamal Abdel Nasser" uwanja wa ndege wa Dar-es-Salaam kumwaga naye machozi wakati wa safari yake kuelekea Kairo, baada ya kumaliza ziara yake rasmi nchini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ziara hiyo ilisisitiza uhusiano wa ushirikiano, mapambano ya pamoja, na msaada wa pande zote kati ya watu wa Afrika katika kujenga na kukabiliana na njama za ukoloni, na kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi wa Afrika na kurudisha mali zake kwa watu wake ili waweze kuchukua jukumu lao katika kujenga ustaarabu wa kibinadamu na kuimarisha misingi ya amani iliyojengwa kuhusu haki.