Siku ya Kimataifa Kwa Wanafunzi

Siku ya Kimataifa Kwa Wanafunzi

Imetafsiriwa na/ Habiba Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Siku ya Kimataifa Kwa Wanafunzi huadhimishwa kila mwaka tarehe kumi na saba ya mwezi Novemba, ikiwa ni ishara ya kukataa vurugu, Ubeberu, Ubaguzi wa rangi, Ukandamizaji na Ukoloni, na ishara ya mapambano ya Ukombozi na Uhuru, na Ujenzi wa maadili ya amani, mshikamano na haki.

Tukio hili ni Ushahidi wa mapambano ya harakati za wanafunzi katika sehemu mbalimbali za dunia, na Umoja wa Kimataifa wa Wanafunzi ilianzishwa katika 1946, yenye makao yake Prague, na mnamo Novemba 17, baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Umoja wa Mataifa ulijitolea siku hiyo ili kwenda sambamba na kumbukumbu ya mauaji ya mwanafunzi "Jan Obla Til" huko Prague, mji mkuu wa zamani wa Czechoslovakia, na wanafunzi wengine wa 1200 walioondolewa baada ya kupinga na kukabiliana na vikosi vya Nazi vya Ujerumani mnamo 1939.

Siku ya Kimataifa kwa Wanafunzi pia huadhimishwa katika nchi nyingi za Kiarabu, hasa Sudan, Syria, Lebanon, Jordan na Misri, mnamo Februari 21 kila mwaka, kama sherehe hii inaanzia Misri kukumbuka mapambano ya wanafunzi dhidi ya Waingereza mnamo 1946.

Ni vyema kutajwa kuwa baadhi ya wanahistoria huandika historia ya harakati za wanafunzi nchini Misri hadi mwaka 1893, ambayo ni tarehe ya kuanzishwa kwa jarida la kwanza la shule kwa wanafunzi, kwa lengo la kueneza roho ya taifa kupitia fasihi na sanaa zake, na kisha Klabu ya Shule za Juu ilianzishwa mwaka 1906, ambayo ni hatua kubwa katika historia ya harakati za wanafunzi wa Misri, ambayo kwa mujibu wa mwanahistoria Walter Lacker kwamba hakucheza wanafunzi ulimwenguni kama jukumu lililochezwa na wanafunzi wa Misri katika harakati za kitaifa na mchango wao katika kutatua masuala ya nchi, ya kwanza iliyokuwa mafanikio ya Uhuru, na kusababisha Uwajibikaji na Ushiriki wa habari katika maisha ya kisiasa.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy