"Wilaya...Uamuzi wa Kidemokrasia" ni Riwaya ya aina tofauti

Imetafsiriwa na: Omar Samir
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Mwandishi wetu kijana Ahmed Al-Juwaili, mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, anashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Kairo kwa kitabu, na riwaya yake ya pili, ambayo inaitwa: "Wilaya... Uamuzi wa Kidemokrasia" ni riwaya ya aina tofauti.... Ina upande wenye nguvu wa mashaka.
Licha ya ugeni wa jina, riwaya hiyo ni Riwaya halisi yenye msukumo wa kifalsafa, kwani inachangia kukuza ufahamu wa umma, na ilikuwa na itaendelea kuwa kujitolea kwa watu wetu, mashujaa wa vita vya akili, na inaonesha kile wanachoteseka ili kutumikia nchi.
Pia inafunua sura halisi ya ugaidi na makundi ya kigaidi, na inaelezea falsafa ya magaidi wanaopenya majimbo, kula njama dhidi yao na kwa nini wanataka kuchukua nafasi ya vyombo vya kitaifa! Hii ni riwaya yake ya pili, ya kwanza ilikuwa na kichwa "Al-Amir Sirr Dawla(Kiongozi ni Siri Ya Serikali)", iliyotolewa mnamo Januari 2017, na riwaya ya mwisho ya asili ya kimkakati "Matempla... Mapambano ya Wakati"
Ikumbukwe kuwa riwaya hiyo itachapishwa katika Ukumbi Na. 1, Banda C17, Dar Scheherazade kwa Uchapishaji na Usambazaji. Maonesho ya Kimataifa ya Kairo kwa kitabu 2021, ambayo yatafanyika katika Kituo cha Maonesho cha Misri kwa Kimataifa, katika Makazi ya Tano, ambayo itaanza mnamo Juni 30.