Siku ya Wajumbe wa Kimataifa

Siku ya Wajumbe wa Kimataifa

Imefasiriwa na/ Malak Hazem
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Siku ya Wajumbe wa Kimataifa inaambatana na siku ya kwanza ya Mkutano wa San Francisco, unaojulikana pia kama Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Shirika la Kimataifa. Mnamo tarehe 25 Aprili 1945, wawakilishi wa mataifa 50 walikutana kwa mara ya kwanza huko San Francisco kwa lengo la kuanzisha shirika ambalo litarejesha amani ya ulimwengu na kuweka misingi ya utaratibu wa ulimwengu baada ya uharibifu wa Vita vya Pili vya Dunia.

Wajumbe 850 walishiriki katika mkutano huo wa miezi miwili, unaowakilisha asilimia 80 ya idadi ya watu duniani, wa kila rangi, dini na bara, ambao wamejitolea kikamilifu kuunda Shirika linalolinda amani na kusaidia kujenga ulimwengu bora.

Mnamo Tarehe Juni 26, 1945, Mkataba wa Umoja wa Mataifa ulisainiwa na wawakilishi wa nchi hamsini waliohudhuria mkutano huo. Mkataba huo ulisababisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, shirika ambalo sasa linajumuisha nchi wanachama wa 193 na hutumika kama eneo kuu la kimataifa la mazungumzo ya pamoja kati ya wajumbe wa nchi wanachama. Wakati wa mkutano huo hakukuwa na serikali ya Kipolishi inayotambuliwa rasmi, lakini mnamo tarehe Juni 28 serikali ilitangaza Poland ilisaini Mkataba - na hivyo kuwa moja ya nchi za wanachama wa awali, na hivyo kuongeza idadi ya nchi wanachama waanzilishi hadi 51.

Azimio la Mkutano Mkuu 73/286 la Aprili 2, 2019 lilisisitiza umuhimu wa mafanikio ya Mkutano wa San Francisco na kuamua kuteua 25 Aprili kama Siku ya Wajumbe wa Kimataifa.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy