Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria

Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria

Imefasiriwa na/ Kamal Elshwadfy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Kila mwaka tarehe 25 Aprili, Nchi za Dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana Malaria, ikiangazia juhudi za kimataifa za kupambana na janga hilo.

Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2008 Barani Afrika, tukio lililoadhimishwa na serikali za Afrika tangu mwaka 2001, kama wakati wa kutathmini maendeleo kuelekea malengo yanayolenga kudhibiti malaria na kupunguza vifo katika nchi za Afrika. Mnamo mwaka 2007, katika kikao cha 60 cha Baraza la Afya Duniani, mkutano uliodhaminiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ulipendekeza kubadilisha Siku ya Malaria barani Afrika kuwa Siku ya Malaria Duniani, kutambua uwepo wa malaria katika nchi mbalimbali duniani, na kuongeza uelewa wa mapambano ya kimataifa dhidi ya ugonjwa huo. Kila mwaka, Aprili 25 imekuwa siku ya malaria inayotambuliwa kimataifa, ikiangazia juhudi za kimataifa za kupambana na malaria na kusherehekea mafanikio yaliyopatikana. Tangu mwaka 2000, dunia imepiga hatua ya kihistoria katika mapambano dhidi ya malaria, na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy