Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Mwandishi wa Guatemala Miguel Ángel Asturias

Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Mwandishi wa Guatemala Miguel Ángel Asturias

Imetafsiriwa na/ Husna Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

"Kwa nini miti inapaswa kuwa na kiu wakati mvua inanyesha" (Miguel Asturias)

Miguel Ángel Asturias ni Mwandishi wa Guatemala, mshairi, mwanahabari na mwanadiplomasia aliyeshinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 1967 na Tuzo ya Lenin ya Amani ya Kimataifa kutoka Umoja wa Kisovyeti mwaka 1966. 

Mwandishi wa Riwaya "Asturias" alizaliwa Oktoba 19, 1899 huko Guatemala, alisafiri kwenda Ulaya kwa mara ya kwanza mnamo 1923 na kukaa huko kwa miaka kumi, aliyotumia huko Paris, ambapo alisoma sheria katika Chuo Kikuu cha Sorbonne kabla ya kuhamia kusoma anthropolojia, na karibu na hii alifaulu katika fasihi, na alikuwa mmoja wa waandishi wa kwanza wa riwaya katika Amerika ya Kusini walioshughulikia suala la Udhalimu katika maandishi yake, ikifuatiwa na waandishi wengi wa riwaya. Miongoni mwa maarufu zaidi ya hizi ni El señor presidente, Hombres de maíz na kazi zingine zimezokuwa na zinaendelea kuwa Urithi tajiri wa fasihi ya Amerika ya Kusini. 

Kazi za fasihi za Asturias zilijulikana na mtindo wa kisasa aliopitisha na kufaulu, ambao ulimfanya kuwa mwanzilishi muhimu wa fasihi ya Amerika ya Kusini katika miaka ya sitini ya karne iliyopita.

Mwandishi huyu mkubwa na mchezaji wa michezo alitumia siku zake za mwisho nchini Hispania hadi kifo chake mnamo 1974, akiacha Urithi tajiri wa mashairi, hadithi, riwaya ya kisiasa na mifano mingi ya kuandika kuhusu Watu wa Asili baadaye inayojulikana kama "literatura indigenista", sasa ya fasihi imeyochukua wanahistoria wengi na shule muhimu katika Amerika ya Kusini tangu mwisho wa karne ya kumi na tisa. 


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy