Kusherehekea Maadhimisho ya Mapinduzi ya Julai 23, 1952

Kusherehekea Maadhimisho ya Mapinduzi ya Julai 23, 1952

Imefasiriwa na / Ali Mahmoud

Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Julai 23 huadhimishwa kwa siku hiyo hiyo kila mwaka, ambapo mapinduzi hayo ni alama muhimu kabisa katika historia ya kisasa ya Misri, mapinduzi hayo ambayo malengo yake ikiwa ni pamoja na: kuondolewa kwa ukoloni wa kiingereza, ukabaila na kuanzishwa kwa maisha ya kidemokrasia.

Hayo Mapinduzi yalifanywa na Maafisa Huru katika Jeshi la Misri, tena Maafisa hao walifanikiwa kudhibiti mambo, na mapinduzi hayo yalipata uungaji mkono mkubwa wa watu, Mapinduzi ya Julai 23, 1952  yalileta mabadiliko nchini Misri katika ngazi zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii, hivyo Mapinduzi hayo yaliwapa  wengi wa Misri haki zao haswa tabaka hilo lililoteseka kwa dhuluma na kunyimwa haki.

Miongoni mwa matokeo ya mapinduzi hayo kwamba: utawala wa kifalme ulikomeshwa na Jamhuri ilitangazwa, Meja Jenerali Muhammad Naguib aliteuliwa kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mnamo Juni 18, 1953, katiba ya 1923 ilifutwa, makubaliano ya Kuenda Kabisa kutoka Misri yalitiwa saini mnamo  Oktoba 19, 1954 na Mwanajeshi wa mwisho wa Uingereza aliondoka Misri mnamo Juni 18, 1956 tena Kampuni ya Mfereji wa Suez ilitaifishwa mnamo Julai 26,1956.

Baada ya mafanikio ya mapinduzi, miradi mingi mikubwa ya kitaifa ilitekelezwa, ikiwa ni pamoja na: Mradi wa Kurejesha Kilimo, pamoja na Mradi wa Bwawa la Juu, ambalo huchukuliwa moja ya miradi muhimu zaidi ya kitaifa katika historia ya kisasa ya Misri.

Na kwa upande wa Elimu, Mapinduzi ya Julai 23 yalichangia kufanya Elimu iwe  bure, na Wizara ya Elimu ya Juu ilianzishwa mnamo 1961, na utamaduni nchini Misri ukawa na nafasi kubwa ya michango hiyo, ambapo Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kitaifa ilianzishwa mnamo 1958, Televisheni ya Misri ilifunguliwa mnamo 1960, na Shirika la Habari la Mashariki ya Kati lilianzishwa kuanza kazi yake ya habari kwa Februari 28, 1958; liwe shirika la kwanza katika Mashariki ya Kati.