Tamasha la Mavuno la Kwanza "Umuganura" Nchini Rwanda 2023

Tamasha la Mavuno la Kwanza "Umuganura" Nchini Rwanda 2023

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky

Umuganura ni neno la Kinyarwanda lenye maana ya sikukuu ya kwanza ya mavuno au tamasha la kwanza la matunda, ni tamasha la kiutamaduni ambalo huadhimishwa nchini Rwanda kila mwaka wakati wa mwanzo wa msimu wa mavuno, Siku hiyo huwekwa na serikali ya Rwanda mwanzo wa Agosti, haswa Ijumaa ya kwanza katika mwezi tena ni likizo rasmi ya umma.

Umuganura asili yake ni enzi za kabla ya ukoloni, wakati Wanyarwanda walitegemea sana kilimo ili kujipatia riziki, Sherehe hiyo inaadhimisha mwisho wa msimu wa mvua na mwanzo wa msimu wa mavuno, wakati muhimu katika kalenda ya kilimo. Umuganura ni sherehe muhimu katika utamaduni wa Rwanda kwa sababu; Inaashiria umuhimu wa kilimo wakati wa msimu wa mavuno, pia ni fursa nzuri kwa Wanyarwanda kukutana, kuonesha utamaduni wao, na kusherehekea mafanikio yao. Aidha, inakuza umoja, ujasiriamali, na huduma kwa jamii.

Awali Umuganura ilikuwa ya kifalme iliyosimamiwa na mfalme ambaye hubariki mavuno na kuomba maombi ya shukrani, lakini baada ya muda ilipitia mabadiliko na maendeleo mbalimbali na kuwa tukio ambalo tunaona leo kuwa tukio la kitaifa ambalo Wanyarwanda kutoka pande zote za nchi wako katika mavazi yao ya kiutamaduni na kucheza ngoma na nyimbo zinazoonesha urithi wao wa Kiutamaduni kama hivyo:

Maonesho ya kilimo na mavuno: Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Rwanda, na maadhimisho ya Umuganura yanatoa fursa kwa wakulima na wataalamu wa kilimo kuonesha bidhaa na ubunifu wao, kwani hafla hiyo inajumuisha maonyesho na  mengi yanayoonyesha utofauti wa mazao ya kilimo yanayolimwa nchini Rwanda.

Maonesho ya Sanaa na Ufundi: Maadhimisho ya Umuganura yanazingatiwa sana na ni sehemu muhimu ya turathi za kitamaduni nchini, huangazia maonyesho ya sanaa na ufundi, yakiwapa mafundi na wasanii wa ndani jukwaa la kuonesha kazi zao.

Maonesho na Hotuba: Tamasha la Umuganura linatoa fursa kwa viongozi wa serikali, wataalamu wa kitamaduni, na viongozi wa jamii kutoa hotuba na mawasilisho kuhusu mada mbalimbali kuanzia kilimo hadi utamaduni, kutoa mwanga kuhusu siku za nyuma, sasa, na mtazamo wa mustakabali wa nchi.

 Vyakula na vinywaji vya kiasili: Vyakula vya Rwanda ni mchanganyiko wa ladha na viambato vilivyochochewa na nchi jirani kama vile Uganda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Vyakula vya Rwanda pia vyenye  aina mbalimbali za nyama ikiwa ni pamoja na mbuzi, nyama ya ng'ombe na kuku, kama vile mboga mboga kama vile viazi vitamu na ndizi.

Maandalizi ya Tamasha la Umuganura 2023 tayari yanaendelea huku kamati ya maandalizi yenye jukumu la kusimamia upangaji na utekelezaji wa hafla hiyo Kamati inayojumuisha viongozi wa serikali, wataalam wa kiutamaduni na wawakilishi wa jumuiya mbalimbali kutoka kote nchini ndiyo inayohusika na maandalizi hayo sherehe. Ikumbukwe kuwa kundi la "Anganzo Ngari" moja ya vikundi maarufu vya ngoma za asili nchini Rwanda, litaandaa sherehe ya muziki  katika tamasha hilo kwa mwaka huu wa 2023, na litajaa ngoma na nyimbo halisi za Wanyarwanda zinazoelezea utamaduni wa Rwanda , na urithi

 Ni jambo la kushangaza katika habari hiyo ni sherehe hiyo imepangwa kuwa tafrija kubwa ambayo haijawahi kutokea hapo awali, kwani itarejea mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Covid-19, kwani ni fursa nzuri kwa wale waliokosa tafrija hiyo mnamo  miaka iliyopita ili kufurahia uzoefu wa kusisimua na usiosahaulika.

Hadi sasa eneo na tarehe kamili ya tamasha hilo haijathibitishwa mwaka huu, lakini serikali inatarajiwa kutangaza tarehe na eneo haraka iwezekanavyo.Hata hivyo, ni wakati wa kusherehekea tamasha la Umuganura.

 

Vyanzo

https://es.unesco.org/creativity/policy-monitoring-platform/art-culture-festivals-umuganura /     

https://nationaltoday.com/umuganura-day/

https://www.officeholidays.com/holidays/rwanda/umuganura-day ,