Hali za Misri Kabla ya Mapinduzi ya Julai 23

Imeandikwa na/ Hagar Mohammed
Mapinduzi ya Julai 23 yanachukuliwa kuwa ni mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mapinduzi hayo yalimaliza utawala wa kifalme na familia ya kifalme ya Mohamed Ali Pasha. Kwa kutafakari hali ya kisiasa nchini Misri katika miaka michache kabla ya mapinduzi, tunaona hasira kubwa dhidi ya mfalme na Uingereza, na hapa tutarudi nyuma ili kujua hatua zilizokuwa msingi wa mapinduzi haya.
Hali za Kisiasa
• Kulikuwa na kutoelewana kati ya mfalme na Chama cha Al-Wafd (chama kilichokuwa na ushawishi mkubwa). Mfalme alikinyima chama hicho haki ya kuunda serikali licha ya ushindi wake katika uchaguzi wa bunge. Hali hii iliendelea hadi kuzuka kwa Vita vya Pili vya Dunia.
• Uungaji mkono wa mfalme kwa serikali chache zisizokuwa maarufu na kuteua wanasiasa wasio na umaarufu kulichochea hasira kubwa kati ya Wamisri dhidi ya Uingereza. Hii ilimfanya balozi wa Uingereza kutumia vifaru kuizingira Ikulu ya Abdeen, kumlazimisha mfalme kukubali kuundwa kwa serikali ya Chama cha Al-Wafd. Hii inachukuliwa kama uingiliaji katika mambo ya ndani ya Misri.
• Baada ya vita vya 1945, Wamisri walikubali tena kudai kutoka kwa Uingereza kumaliza ukoloni nchini mwao. Maandamano yalipangwa katika miji mbalimbali ya Misri, lakini hayakuleta mabadiliko yoyote.
• Waziri Mkuu Mahmoud Fahmy alikusudia kuipeleka kesi ya Misri kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1947, lakini alikosa msaada mkubwa, na nchi tatu tu ndizo zilimunga mkono: Syria, Umoja wa Kisovyeti, na Poland.
• Baada ya kushindwa kwa Jeshi la Misri katika vita vya Palestina kutokana na silaha dhaifu, baadhi ya wanahabari walisema kuwa waziri wa ulinzi na mfalme walihusika, lakini baadaye ilithibitishwa kuwa madai hayo yalikuwa ya uongo.
• Baada ya ushindi wa Chama cha Al-Wafd katika uchaguzi wa bunge mnamo mwaka 1950, Mustafa Al-Nahhas alikua mkuu wa serikali ya Misri. Hali za kisiasa zilikuwa zimeathiriwa sana na kushindwa kwa Jeshi la Misri katika vita vya Palestina na uingiliaji wa Uingereza. Mustafa Al-Nahhas alitangaza kuvunja mkataba wa 1936 na Uingereza, ambao ulisema kuwa Uingereza ilikubali uhuru wa Misri huku ikiwa na majeshi yake karibu na Mfereji wa Suez.
Hali za Kiuchumi
• Ingawa Misri haikushiriki moja kwa moja katika Vita vya Pili vya Dunia, iliteseka kutokana na hali mbaya ya kiuchumi kutokana na mapigano yaliyotokea katika ardhi zake baada ya vikosi vya Kijerumani kupigana na waingereza katika jangwa la Magharibi.
• Mfereji wa Suez ulidhuriwa na mapigano yaliyoshuhudiwa kwenye Bahari ya Mediteranea. Serikali ilijaribu kuhakikisha udhibiti wa mazao yote, na hivyo kulazimisha wakulima kutofautisha mazao, siyo pamba pekee. Hii ilimnyima mkulima faida kubwa ya kuuza pamba na kusababisha mateso makubwa kutokana na mgawanyo mbaya wa mashamba.
• Viwanda vingi vilitegemea malighafi kutoka kilimo, lakini viwanda vilikuwa na mchango mdogo katika mapato ya taifa ambayo yalitegemea kilimo.
• Wageni, hasa Waingereza, walihodhi biashara ya nje. Wakati huo, biashara ya nje ilikuwa ni asilimia 50 ya mapato ya taifa.
Vyanzo
• Tovuti ya Daktari Ali Alsalmy
• Tovuti ya Al-Ahram Leo
• Tovuti ya Paza Sauti Yako
• Tovuti ya Kairo 24