Nafasi ya Lugha na Ajenda ya Afrika 2063

Imeandikwa na/ Rwan Abd El-Naby
Kupitia maadhimisho ya miaka 50 ya kuundwa Umoja wa Afrika ulizindua maoni mapya kwa bara la Afrika chini ya anwani ya “Ajenda ya 2063” na lengo lake ni “Afrika tunayotakia”, na wanachama 54 wa Umoja wa Afrika walionesha mpango huo kama wito wa kuchukua hatua katika jamii zote za kiafrika, ili kujenga Bara lenye mafanikio na umoja, misingi yake ni maadili na mustakabali wa pamoja.
Ajenda ya Afrika 2063 ni mfumo wa kimkakati wa kugeukia upande wa kiuchumi na wa kijamii kwa bara katika miaka ya 50 ijayo, na Ajenda hiyo inategemea kuharakisha utekelezaji wa mipango ya awali na hali maalumu ya ukuaji na maendeleo endelevu kama: Mpango wa Utekelezaji wa Lagos, Mkataba ya Abuja, Mpango wa Kiwango cha chini cha Ushirikiano, Mpango wa Maendeleo ya Miundombinu barani Afrika (PDIA), Mpango wa Maendeleo ya kilimo ya jumla (CADDP), Ushirikiano mpya wa Maendeleo Afrika (NEPAD), na pia yategemea sera za kitaifa, kikanda, na bara ambazo ni bora zaidi ili kuhakikisha maendeleo.
Mojawapo ya sababu za kuunda Ajenda ya Afrika katika wakati huo; ni mabadiliko ya muktadha wa kimataifa kwa kuwa inaweza kuyapitia kwenda mbele na kuokoa makundi mengi ya watu kutoka umaskini, kuboresha kwa kipato, kuchochea mabadiliko ya kiuchumi na ya kijamii, na vilevile mojawapo ya sababu zake kuwa Afrika imara na yenye umoja kwa kuwa Afrika inaunganishwa zaidi na kuwa nguvu inayoathiri; na maoni ya ajenda ni “Bara la Afrika lenye ushirikiano na mafanikio na bara bora na inayoendeshwa na umma wake na kuwa na nguvu inayoathiri”, na kauli yake ni “Umoja, ustawi wa pamoja na amani”.
Matamanio na Malengo ya Ajenda ya Afrika 2063
- Malengo 18 yanatokana na matamanio 7 ya kiafrika, na matamanio haya ni:
- Tumaini la kwanza: Afrika yenye mafanikio kupitia ukuaji jumuishi, maendeleo endelevu, kuondoa umaskini na kufikia ustawi katika mchakato ya mabadiliko ya kijamii na ya kiuchumi ya bara.
- Tamaini la pili: Afrika inaunganisha kwa kisiasa, na inategemea maadili ya juu kwa Afrika kwa ujumla na maoni ya kuendeleza Afrika tangu mwaka 1963, pamoja na kuzingatia uhuru wa kisiasa na wa kijamii, kwa lengo la maendeleo yanayotegemea nafsi na utawala wa kidemokrasia.
- Tumaini la tatu: Afrika ina utamaduni wa kimataifa kwa utawala bora, uadilifu, maadili ya kidemokrasia, utawala wa sheria na usawa wa kijinsia na heshimu haki za binadamu.
- Tumaini la nne: Afrika yenye usalama kupitia kutumia njia za kufikia amani, kutatua migogoro kwa njia zote na kutia utamaduni wa amani ndani ya watoto na vijana wa Afrika kupitia elimu.
- Tuamini la tano: Bara la Afrika lenye utambulisho wa kitamaduni, urithi na maadili ya pamoja kupitia kuimarisha historia ya pamoja kwa Afrika na pia kimarisha maadili ya utu na utambulisho na heshima tofauti ya kisini ya umma wa Afrika.
- Tumaini la sita: kushirikisha watu waafrika wote katika mchakato wa maamuzi kwenye nyanja zote, ili hamtupiwi mbali mtoto au mwanamke au mwanamume kwa sababu ya jinsia au mwelekeo wa kisiasa, au kidini au kikabila, au umri, au kwa sababu yoyote nyingine.
- Tamaini la saba: Afrika yenye nguvu na umoja na kuwa na jukumu muhimu linalotoa athiri nzuri katika masuala ya kimataifa, na hiyo kwa sababu ya umuhimu wa Umoja wa Afrika kukabiliana na uingiliaji wa nje unaoendelea na unaojaribu kugawanya bara la Afrika na kuweka vikwazo mbele ya baadhi ya nchi.
Lakini kwa ajili ya kufikia matamanio na malengo ya Ajenda ya Afrika 2063, lugha lazima iwe nafasi ya msingi, na hiyo inarejea kwa sababu mbalimbali kama:
- Mawasiliano:
Lugha ni chombo muhimu cha kuwasiliana baina ya sehemu za jamii zote za kiafrika.
Kutafsiri Ajenda ya Afrika 2063 kwa lugha kuu zote za Afrika, kuhakikisha kufahamiwa na umma wote waafrika.
Kutumia njia mbalimbali za kuwasiliana na ikiwa ni pamoja na Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii, ili kueneza maelezo kuhusu Ajenda ya 2063 na lugha mbalimbali.
- Kukusanya na Kushiriki:
Kutumia lugha ili kuvuta kuunga mkono kwa Ajenda na kuwahimiza watu kwa kushiriki utekelezaji wake.
Kutumia lugha wazi katika kuwasiliana na hadhira, kuhakikisha kufahamu kwao kwa malengo ya Ajenda na faida zake.
Kushirikisha vijana katika mchakato wa kuwasiliana kwa umakini, kiasi kwamba vijana ni wasukumu wakuu wa mabadiliko barani Afrika.
- Kujenga Utambulisho:
Lugha ni kipengele kikuu cha kuimarisha hisia ya utambulisho wa Afrika wa pamoja, na ni jambo muhimu ili kufikia umoja na mshikamano baina ya nchi za Afrika.
Kuhimiza kwa kutumia lugha za Afrika kwenye maisha ya umma, kama vile sanaa, muziki, na fasihi.
- Elimu na Utafiti wa Kisayansi:
Kuhimiza kwa kufanya utafiti wa kisayansi katika uwanja wa lugha za kiafrika, ili kuendelea njia mpya kwa kuzifundisha na kuzitumia.
Lugha ni kipengele muhimu ili kufundisha vizazi vijavyo kuhusu Ajenda 2063 na kuwahimiza kushiriki utekelezaji wa malengo yake.
- Mabadiliko ya Kitamaduni:
Lugha inasaidia kubadilishana maarifa na ujuzi baina ya nchi za kiafrika, na hiyo inachangia kuimarisha ushirikiano na mshikamano kwenye nyanja zote.
Kuunga mkono mpango wa kubadilishana wanafunzi baina ya nchi za kiafrika, ili kuwahimiza wanafunzi kujifunza lugha za Afrika.
Kuhimiza mipango ya kitamaduni inayoimarisha matumizi ya lugha za kiafrika kama tamasha za fasihi na muziki.
Ingawa umuhimu wa lugha, lakini kuna changamoto nyingi za lugha zinazokabiliana na Ajenda 2063, zikiwemo:
- Tofauti za Lugha:
Bara la Afrika ni bara lenye lugha nyingi zaidi duniani, likiwa na lugha zaidi ya 2000 huongewa naye, na tofauti hiyo ni changamoto kubwa ya kuwasiliana na kushirikiana kati nchi za Afrika.
-
Uenezi wa Lugha za Kigeni:
Lugha za kigeni zinaenea katika nyanja nyingi za kiafrika hasa Kiingreza na Kifaransa, na hiyo inapunguza kutumia lugha za kiafrika katika nyanja kama elimu, utafiti wa kisayansi na maisha ya umma.
- Ukosefu wa Nyenzo za Lugha:
Lugha nyingi za kiafrika zenye ukosefu wa nyenzo za lugha kama vile kamusi, vilivyotafsiriwa, na vifaa vya kufundishia, na hiyo inazuia kutumia kwake kwenye nyanja mbalimbali.
Lakini kuna hatua nyingi zinazoweza kuzichukuliwa ili zishinde changamoto za lugha zinazokabili Ajenda 2063, zikiwemo:
- Kuimarisha Lugha za Afrika:Kuimarisha lugha za kiafrika ni lazima katika nyanja zote, kwa njia ya kusaidia elimu na utafiti wa kisayansi na kuchapisha na lugha za kiafrika.
- Kujenga Uwezo wa Lugha: Inapaswa kujenga uwezo wa watafsiri na wataalamu wa lugha kwenye nchi za kiafrika, ili kutoa huduma za ufasiri na uarabishaji kwa madhubuti.
- Kuimarisha ushirikiano wa Lugha: Ni lazima kuimarisha ushirikiano wa lugha kati ya nchi za kiafrika katika uwanja wa lugha na kubadilishana ujuzi.
Mwishoni, waandaaji wa ajenda hii wanaona tofauti na mipango ya awali, kwani inakaribia zaidi na wananchi waafrika, inasukumwa na sauti za watu waafrika na wanachotaka, lakini ili kufikia malengo juu ya kiwango cha kitaifa, kikanda na bara, inapaswa kuna lugha, kwani lugha ni chombo kikuu kwa hiyo, na inaweza kugeuza lugha kwa kipengele cha kufikia maendeleo endelevu na umoja na mshikamano barani Afrika.