Siku ya Kimataifa ya Uongozo wa Kitalii

Siku ya Kimataifa ya Uongozo wa Kitalii

Imetafsiriwa na/ kamal Elshawadfy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Imeandikwa na/ Saeed Al-Batouti

Siku ya Kimataifa ya Uongozo wa Kitalii, au Siku ya Uongozo wa Kitalii Duniani, husherehekewa tarehe 21 Februari kila mwaka, ambapo Shirikisho la Kimataifa la Waongozo wa Kitalii (WFTGA - shirikisho la dunia la vyama vya waongoza watalii) lilianzishwa mwezi Februari mwaka 1985 katika Mkutano wa Kimataifa wa Kwanza wa Waongozo wa Kitalii.

Maadhimisho ya siku hiyo yanakusudia kuongeza uelewano ulimwenguni kote kuhusu ukweli muhimu, ambao ni kwamba Waongozo wa Kitalii wanawakilisha mabalozi wa utamaduni kwa nchi na vivutio vya utalii wanavyoviwakilisha.

Kwa maoni yangu, na uhalisi pia, ninaamini kuwa uongozi wa kitalii ni mojawapo ya kazi hatari zaidi katika sekta ya utalii kwa ujumla. Mwongozo wa Kitalii ni kiungo kati ya bidhaa ya kitalii katika eneo la kitalii na watalii, pia ni chanzo cha habari kuhusu kila jambo dogo na kubwa kwa mtalii, ambazo zinaweza kutoa taswira nzuri au mbaya ya eneo la kitalii.

Kazi ya Mwongozo wa kitalii ni kazi ngumu sana, ambapo ana jukumu la mafanikio ya safari ya kitalii, bali singetia chumvi nikisema kwamba ana jukumu kubwa katika mafanikio ya juhudi za kimasoko zinazofanywa na vyombo husika kwa masoko; kwa ajili ya eneo la kitalii. Yeye ndiye chanzo kikuu cha habari kwa wageni, na huwapa habari za aina mbalimbali kuhusu nchi, historia yake, urithi wake wa kitamaduni, desturi na mila, na asili ya maisha ya kijamii ambayo wenyeji wake wanaishi, na mambo mengine mengi. Aidha, anakabiliana na maswali na shaka zao, ambazo mara nyingi zinahusisha masuala mbalimbali yanayohusiana na nchi na kila kitu ndani yake. Majibu hayo na jinsi yanavyotolewa yanachangia sana katika picha ya kiakili kuhusu nchi na eneo la kitalii, ambayo inabaki akilini mwa mtalii na kuhamishiwa au kusambazwa naye wakati anaporudi kwenye jamii anayofanyia kazi na kuishi, kama ilivyothibitishwa katika akili yake.

Kama nilivyotaja hapo awali, tumegundua mabadiliko mengi yaliyotokea katika mwelekeo, tamaa, na mienendo ya makundi mbalimbali ya watu katika jamii nyingi wakati huu, na mwelekeo wa uokoaji wa mtindo wa utalii umeanza kuongezeka tena kwa nguvu baada ya kupungua kwa kiasi kikubwa katika miaka iliyopita.

Utalii wa kitamaduni ni mfano mkuu wa utalii endelevu, ambapo utalii endelevu ni utalii unaozingatia kabisa athari za kiuchumi, kijamii, na kimazingira za kisasa na za baadaye, na kujibu mahitaji ya wageni, viwanda, mazingira, na jamii zinazowapokea. Utalii wa kitamaduni unafanikisha hilo kutokana na athari zake moja kwa moja kwa uchumi wa nchi na jamii za ndani.

Tunawaombeni wadau wa vivutio vya utalii kuchukua hatua muhimu kuhusu kazi ya uongozo wa kitalii, na kuzingatia umuhimu wao, pamoja na kusaidia na kusimamia vyama vyao vya kitaaluma, na kuweka kanuni bora za uteuzi na utoaji leseni, badala ya kutoa leseni kiotomatiki kwa kila mhitimu wa fani ya mwongozo wa utalii kutoka vyuo au taasisi za utalii, ambao wengi wao hawajui lugha vizuri na hawana taarifa za kutosha, na labda hawana taarifa kabisa, kama inavyofanyika katika baadhi ya nchi.

Tunasisitiza pia umuhimu wa kuzingatia programu kali za maandalizi na mafunzo yanayohusiana na kazi hiyo hatari na muhimu.

Wakati huo huo, tunawaomba waongoza wa kitalii kuunga mkono wale wanaosimamia kazi za utalii na mamlaka za ndani katika vivutio vya utalii na kushirikiana nao kwa ajili ya kuhifadhi kipato na riziki za watu katika jamii za wenyeji ambazo watalii wanatembelea, na kufanya kila juhudi ili kuwafaidi na kuwasaidia kifedha na kiroho.

Ni lazima tumepeleke mashada ya maua, upendo, na shukrani kwa waongozo wa kitalii ulimwenguni kote - nguvu na hamasa halisi ya kuelewa na kufahamu kuhusu bidhaa za kitalii na vivutio vya utalii.

Asante kwa mchango wenu katika kuunganisha tamaduni na watu na kueneza thamani za upendo, uvumilivu, na amani!

Heri ya Mwaka Mpya kwa ndugu waongozo wa kitalii duniani..


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy