Kikao cha kazi cha kujua kuhusu Tamaduni na uzoefu wa nchi za Kiafrika ndani ya matukio ya siku ya kwanza ya Udhamini wa Nasser 

Kikao cha kazi cha kujua kuhusu Tamaduni na uzoefu wa nchi za Kiafrika ndani ya matukio ya siku ya kwanza ya Udhamini wa Nasser 

Dokta Nizar Samy, Mshauri wa Uvumbuzi na Ujasiriamali alionesha programu ya Udhamini pia aliwagawanya vijana katika vikundi vya kazi kwa lengo la kuvunja vikwazo na kuingiliana kati ya tamaduni tofauti za nchi zinazoshiriki kupitia shughuli kadhaa.

Hiyo ilifanyika ndani ya matukio ya siku ya kwanza ya Udhamini wa Nasser unaotolewa kwa Wizara (Ofisi ya vijana waafrika na idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuli "Waziri Mkuu", mnamo kipindi cha tarehe ya 8 hadi 22 Juni, 2019,kwa ushirikiano wa Shirikisho la vijana waafrika.

Wakati vijana waafrika walitayarisha onyesho la kila nchi ili kutambulisha tamaduni tofauti na kubadilishana uzoefu, pamoja na kuwaunganisha vijana waafrika, kufaidika na uwezo na mawazo yao, kukuza maadili ya Kiafrika kati yao, kujenga daraja la mawasiliano kati ya watu wa bara la Afrika na kuimarisha mahusiano kati ya ndugu wa Afrika.

Matukio ya leo yamejumuisha ziara ya makumbusho ya Kiongozi "Gamal Abd El Nasser pia kufanyika mkutano na Mkurugenzi wa zamani wa Chuo cha Tafiti na Masomo ya kiafrika, Profesa. El-Sayed Fleifel, kuhusu Gamal Abd El Nasser na Afrika.

Ikumbukwe kwamba Udhamini unazingatiwa moja ya njia za utendaji wa mpango wa (Million by 2021) ili kuwawezesha vijana waafrika milioni moja, uliotolewa kwa Kameshina ya Sayansi, Teknolojia, na Rasilimali za binadamu katika Umoja wa Afrika, na unalenga kuhamisha jaribio kale la kimisri la kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha makada vijana waafrika wa kimageuzi wenye mitazamo inayosawazisha na mielekeo ya Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika.