Hatua ya Mwanzo ya Baba Waanzilishi wa Umoja wa Afrika ndani ya shughuli za siku ya nane ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Imetafsiriwa na: Youssef Ibrahim
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Leo, Jumuiya ya Afrika ilipokea vijana wa Kiafrika wanaoshiriki katika "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika", katika makao makuu ya Chama huko Kairo, wakati wa shughuli za "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika" iliyozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana wa Afrika na Utawala wa Kati wa Bunge na Elimu ya Kiraia) chini ya ufadhili wa Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, wakati wa kipindi cha 8 hadi 22 Juni 2019, kwa kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Afrika.
Mkutano ulifanyika katika makao makuu ya Chama cha Vijana wa Afrika kilichoitwa "Misri... Mwanzo wa waasisi wa Umoja wa Afrika",kwa kuhudhuria ya Balozi Mohamed Nasreddine, Rais wa Bunge la Afrika na Dkt. Amna Fazza, mwanzilishi wa Klabu ya Wanawake ya Afrika, ikiwa ni sehemu ya shughuli za siku ya saba ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa".
Wakati wa mkutano huo, Balozi Mohamed Nasr El-Din alielezea historia ya jengo la chama hicho, ambapo lilianza shughuli zake mwishoni mwa mwaka 1956 hadi sasa, akionesha kuwa ni makazi ya profesa wa chuo kikuu na mwanadiplomasia Muhammad Abdul Aziz Ishaq, ambaye alikuwa wa pili katika Chuo Kikuu cha Khartoum nchini Sudan na alikuwa na shauku ya kupenda Afrika, kisha akazindua saluni ya kitamaduni katika makao makuu ya chama hicho kwa sasa kushughulikia mada zinazohusiana na Afrika na watu wake na kufikisha uzoefu wake wakati wa ziara yake nchini Sudan.
Nasreddin alisisitiza jukumu la kiongozi Gamal Abdel Nasser katika harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa ukoloni, ambao ulianza kutoka kwa Bunge la Afrika wakati huo, akionesha kwamba alitoa msaada wote muhimu, iwe kisiasa, nyenzo au maadili, kwa wanafunzi ambao walikuwa viongozi wa ukombozi katika nchi zao hadi uhuru wa nchi za Afrika katika miaka ya sitini, ambayo ilifanya Baraza kufikia dhamira yake ya kwanza, iliyoanzishwa.
Nasreddin alitaja majukumu ya Jumuiya ya Afrika, ambayo ni kupambana na ubaguzi wa rangi kusini mwa Afrika, pamoja na kuwajali Waafrika nchini Misri na kuwapa msaada kamili, misaada na mafunzo kwa watu wa nchi za Afrika.
Kwa upande wake, Dkt. Amna Fazza alipongeza jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo katika kuwakutanisha vijana wa Afrika pamoja na kuwasaidia kupitia utekelezaji wa Udhamini huo ya kubadilishana tamaduni na uzoefu na kufikia ushirikiano miongoni mwa vijana wa bara la Afrika.
Aidha amesisitiza kuwa Bunge la Afrika ni mojawapo ya jitihada za Hayati Rais Gamal Abdel Nasser kwa lengo la kuliunganisha bara la Afrika ambapo harakati za ukombozi zilizinduliwa na kubeba vifaa na silaha, pamoja na kwamba ni saluni ya kitamaduni inayowakutanisha watu wa nchi za Afrika, akieleza jukumu lake katika ukombozi wa Afrika kutoka kwa ukoloni.
Fazza alielezea kazi na sekta za chama, ambazo zinawakilishwa katika sekta ya kidiplomasia, ambayo hutumikia watoto wa jamii na masuala ya wanafunzi wa Kiafrika, na sekta ya utamaduni, ambayo inategemea mawasiliano na mazungumzo kati ya nchi za bara la Afrika katika nyanja za fasihi, utamaduni, sanaa, sinema na ukumbi wa michezo, na sekta ya teknolojia ya habari, ambayo huandaa kozi na warsha za kufundisha mifumo ya kompyuta ya Waafrika na hutoa vyeti vilivyoidhinishwa na Kijiji cha Smart, Mbali na mafunzo hayo, maendeleo ya binadamu na sekta ya kujiendeleza ambayo hutoa kozi na warsha za bure kwa Waafrika katika nyanja ya maandalizi ya uongozi, redio, vyombo vya habari, uandishi wa habari na afya ya akili, sekta ya mazingira, ambayo inalenga kuongeza uelewa wa mazingira ya Afrika, na sekta ya Klabu ya Wanawake wa Afrika, ambayo inapinga changamoto na matatizo yanayowakabili wanawake wa Afrika.
Abdullah Bashir, Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika, alieleza kuwa Umoja huo ni mojawapo ya taasisi za Jumuiya ya Afrika chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika, na umejikita katika misingi ya umoja, udugu na mshikamano, akibainisha kuwa hutoa msaada wa kisayansi, nyenzo na maadili kwa wanafunzi wote wa nchi za Afrika katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, pamoja na kuhifadhi utambulisho wa Kiafrika.