"Nishati nchini Misri" ndani ya shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Afrika

"Nishati nchini Misri" ndani ya shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Afrika

Dokta Gamal Al-Qalyubi, profesa wa Uhandisi wa Petroli, Nishati na Petroli katika Chuo Kikuu cha Marekani na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mafuta la Misri, alithibitisha kwamba Misri imepiga hatua za juu mnamo miaka iliyopita katika kupunguza uagizaji wa Rasiliamali za mafuta kutoka nje ya nchi hadi kuondokana na uagizaji wake kikamilifu ifikapo mwaka 2022 baada ya kutosheleza  gesi asilia, na akiashiria kuwa uongozi wa kisiasa wa nchi ulikuwa na nia ya kupunguza Muswada wa Sheria ya Uagizaji bidhaa kupitia hatua kadhaa ulizozichukua ili kufikia Maendeleo endelevu.

Hiyo ilikuja wakati wa kikao cha "Nishati nchini Misri" ndani ya shughuli za siku ya tatu ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika" uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika, Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia), Chini ya uangalifu wa Dokta Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, na kwa ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 8 hadi 22 Juni 2019 katika Kituo cha Elimu ya Uraia humo Al Gazira.

Pia, Al-Qalyubi amefafanua mipango na hatua ilizochukuliwa na Misri kufikia Maendeleo katika uwanja wa Nishati,  akisisitiza kuwa hatua hizo ziwe sawa na Mafuta, Gesi asilia au Umeme ni hatua kubwa ya kufanikisha kujitosheleza kwa Nishati nchini Misri ambayo huokoa mabilioni ya Dola, akibainisha kuwa Nishati ndiyo nguzo kuu ya kufikia Maendeleo endelevu.

Al-Qalyubi alisisitiza kuwa mkakati wa serikali katika sekta ya Nishati unatokana na mihimili mitatu mikuu, nayo ni: kurekebisha upya sekta ya Gesi asilia, kusaidia ufanisi wa Nishati, na kushinda Uhalisia wa ongezeko la joto Duniani kwa kupunguza mambo yanayotokea.

Al-Qalyubi aliashiria kuwa shamba la Sola katika eneo la Benban Barabarani mwa Aswan ni miongoni mwa mitambo mitatu mikubwa ya Nishati ya Jua katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, akielezea uzoefu wa Misri katika kutumia Nishati ya Jua na kuibadilisha iwe Umeme, akisisitiza kuwa Serikali ya Misri katika mpango wake inazingatia suala la kutofautisha vyanzo vya Nishati, ambapo inapotegemea uzalishaji wa Nishati ya Umeme kwa kutumia njia za kisasa za Teknolojia.

Wakati Al-Qalyoubi ameonesha mafanikio muhimu zaidi yaliyohakikishwa na Misri kupitia uanzishaji wa miradi kadhaa ya ujenzi wa miundombinu na kuanzisha mtandao wa Umeme wa ndani kutoka Aswan ili kuzunguka maeneo yote ya Jamhuri kwa nguvu ya Umeme, na kubainisha kuwa Misri ina vituo 68 na vituo vitatu vya Umeme kutoka vituo vikubwa 8 Duniani pamoja na minara ya Umeme na kuanzishwa kwa mtandao wa kitaifa wa usafirishaji unaozingatia voltage ya juu na kupanuka hadi kufikia mji mkuu mpya.

Na Al-Qalyubi aliwataka Vijana waafrika kukabiliana na matatizo ya nchi yao wenyewe, kwani wao ndio wenye dhamana ya kuongoza mambo ya nchi zao na mambo ya mabara yao, pamoja na kunufaika na uzoefu wa Misri na kuihamishia nchi za Bara la Afrika kwa Ushirikiano na juhudi za pamoja, kwani Misri ni sehemu ya Afrika, na akisisitiza haja ya kutafuta kutatua matatizo ya bara hilo na kupata uhuru na usalama kwa ajili ya kuingia katika Maendeleo katika uwanja wa Nishati na kisha kufikia Maendeleo endelevu.