Kiashirio cha Mwanzo wa Baba Waanzilishi wa Umoja wa Afrika, ni miongoni mwa shughuli za siku ya nane
Leo, Jumuiya ya kiafrika iliwakaribisha vijana wa Afrika wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika katika makao makuu yaa Jumuiya huko Kairo, wakati wa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa uongozi wa kiafrika uliotolewa kwa Wizara ya Vijana na Michezo ( Ofisi ya Vijana ya kiafrika, Idara Kuu ya Ubunge na Elimu ya kiraia) kwa Uangalifu wa Waziri Mkuu Dkt. " Mostafa Madbouly" mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 8 hadi 22 Juni, kwa kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Afrika.
Na katika Makao makuu ya Jumuiya,mkutano fulani ulifanywa kwa vijana wa Afrika ukiwa na kichwa cha " Misri..ni Nukta ya mwanzo ya Baba Waanzilishi wa Umoja wa Afrika" kwa mahudhurio ya Mkuu wa Jumuiya ya kiafrika, Balozi
" Mohamed Nasr El Din" na Mwanzilishi wa klabu ya wanawake wa Afrika Dkt. " Amna Fazaa" na hiyo ni miongoni mwa shughuli za siku ya saba za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika.
Na mnamo mkutano huo Balozi " Mohamed Nasr El_Din alieleza historia ya jengo la Jumuiya, ambapo lilianza shughuli zake mwishoni mwa 1956 mpaka sasa, akibainisha kuwa lilikuwa makazi ya Profesa wa chuo kikuu na Mwanadiplomasia "Mohamed Abdulaziz Ishaq ", aliyesafirishwa kwa Chuo Kikuu cha Khortoum huko Sudan, na alikuwa na upendo mkubwa sana kwa Afrika, kisha alizindua majadiliano ya kiutamaduni sasa katika makao makuu ya Jumuiya; kujadili maudhui inayohusu Afrika na raia wake na kuhamisha uzoefu wake mnamo safari yake huko Sudan.
Na Nasr El_ Din alisisitiza mchango wa Kiongozi Marehemu " Gamal Abd El Nasser" katika harakati za ukombozi wa Afrika kutoka ukoloni zilizotolewa kwa Jumuiya ya kiafrika wakati huo, akibainisha kuwa yeye alitoa msaada wote kisiasa, fedha au nafsi kwa wanafunzi ambao wakawa viongozi wa ukombozi katika nchi yao hadi nchi za kiafrika zilipokomboa mnamo kipindi cha miaka sitini, iliyowezesha Jumuiya ya kuhakikisha dhamira yake muhimu ya kwanza.
Na aliashiria shughuli za Jumuiya ya kiafrika ambazo zinapinga ubaguzi katika kusini mwa bara la Afrika pamoja na kuwatunza waafrika nchini Misri na kuwapa msaada kamili, Udhamini na Kozi za mafunzo kwa raia wa nchi za kiafrika.
Kwa upande wake Dkt. "Amna Fazaa" alisifu nafasi ya Wizara ya Vijana na Michezo katika kujumuisha Vijana Waafrika na kuwaunga mkono kupitia kutekeleza Udhamini kama huo; ili kubadilishana Utamaduni na Uzoefu na kuhakikisha ukaribu kati ya raia wa bara la Afrika.
Na pia alisisitiza kuwa Jumuiya ya kiafrika ni moja ya juhudi za Rais Marehemu " Gamal Abd El Nasser" kwa lengo la kuunganisha bara la Afrika, ambapo ilizindua harakati za ukombozi na kubeba silaha pamoja na ilikuwa Mahali pa Majadiliano ya kiutamaduni inayowaunganisha raia wa nchi za kiafrika, akiashiria jukumu lake katika kukomboa bara la Afrika kutoka Ukoloni.
Na Fazaa alielezea kazi na sekta za Jumuiya ambazo katika sekta ya Diplomasia inayohudumia watu wa Jumuia na Masuala ya wanafunzi waafrika na sekta ya kiutamaduni inayotegemea mawasiliano na majadiliano kati ya nchi za kiafrika katika nyanja za Fasihi, Utamaduni, Sanaa, Senima, Michezo ya kuigiza, pia sekta ya Teknolojia ya habari inayoandaa kozi na kazi ya kuwafundisha waafrika mifumo ya kompyuta na kutoa vyeti vinavyoruhusiwa kutoka "Smart Village" pamoja na sekta ya mafunzo, maendeleo ya binadamu inayotoa kozi na kazi bure kwa waafrika katika nyanja za kuwaandaa viongozi, Redio, Vyombo vya Habari, Uandishi wa Habari, Afya ya Saikolojia na sekta ya mazingira inayolenga kutambulisha mazingira ya kiafrika na sekta ya klabu ya mwanamke Mwafrika inayopinga changamoto na matatizo
yanayokabiliwa na Mwanamke Mwafrika.
Makamu wa Rais wa Umoja wa wanafunzi wa Afrika "Abdullah Al_Bashir " alielezea kuwa Umoja huo ni moja ya misingi ya Jumuiya ya kiafrika ukihusiana na Umoja wa Afrika na unategemea misingi ya Umoja, Ndugu, na Mshikamano, akiashiria kuwa anatoa misaada ya kisayansi, kifedha, na nafsi kwa wanafunzi wote wa nchi za kiafrika katika Jamhuri ya kiarabu ya Misri, vilevile kuhifadhi Utambulisho wa kiafrika.