Wanaume Karibu ya Rais Abdel Nasser (8)... Hussein Al-Shafei, Makamu wa Rais wa Jamhuri

Wanaume Karibu ya Rais Abdel Nasser (8)... Hussein Al-Shafei, Makamu wa Rais wa Jamhuri

Imetafasiriwa na/ Sara Saed
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Alizaliwa tarehe nane ya Februari 1918, kwenye mji wa Tanta huko Mkoa wa Gharbia, baba yake alikuwa mhandisi katika manispaa ya Tanta, kisha akahamia mji wa Mansoura, ambapo babu yake Hassan Al-Shafei, meya wa kijiji cha Kafr Taha Shubra, Kituo cha Quesna huko Menoufia, na babu yake wa mama Mustafa Al-Azizi, meya wa jiji la Tanta, alijiunga na Shule ya Kifaransa ya Saint Louis (Frere) kwa miaka mitatu, kisha akahamia Shule ya Msingi ya Al-Qased huko Tanta mnamo 1926, kisha Shule ya Sekondari ya Mansoura mnamo 1934.

Al-Shafei alijiunga na Chuo cha Kijeshi mwaka 1936, ambapo alifahamu Abdel Moneim Riad, Gamal Abdel Nasser, Zakaria Mohieddin, Anwar Sadat, na alisafiri kwenda Uingereza kwa miezi mitatu kabla ya kuhitimu mwaka 1938, alijiunga na jeshi na kubaki huko hadi mapinduzi ya Julai 1952.

Al-Shafei alishiriki kwenye vita vya Palestina mwaka 1948, na aliingizwa katika Utawala Mkuu wa Jeshi, wakati majeshi ya Misri yalipozingirwa huko Fallujah, na Uhusiano wa Al-Shafei na maafisa wengi ulipanuka kupitia Uwepo wake kwenye Idara ya Jeshi, kuwajibika kwa maafisa na harakati zao, na kufuatia matokeo ya vita, hisia ya kuchemka ilianza kutawala miongoni mwa maafisa wa jeshi.

Mnamo Septemba 1951, Abdel Nasser alikuwa akipita juu ya Usimamizi wa jeshi, na wanaume hao wawili walikutana kwenye ngazi ya nje, na hawakumfahamu Shafi'i, alijua kwamba Nasser akiwa mkuu wa Shirika la Maafisa Huru, na kuzungumza naye juu ya hali ya Misri, alichukua Abdel Nasser anasikia maneno ya Shafei bila maoni yoyote. Siku hiyo hiyo, al-Shafei aliwatembelea Tharwat Okasha na Othman Fawzi na kumjulisha juu ya jukumu lake la kuongoza jeshi siku ya mapinduzi na silaha zake na mizinga.

Alimaliza mamlaka ya Al-Shafei katika Usimamizi wa jeshi mnamo Oktoba 20, 1951, na kisha akarudi kwenye jeshi, na akaanza kuajiri wengi kwa manufaa ya mapinduzi, ambapo alichukua Uongozi wa kikosi cha kwanza cha magari ya kivita yaliyopindua Utawala wa kifalme Usiku na tarehe ishirini na tatu ya Julai 1952, na akawa mwanachama wa Baraza la Amri ya Mapinduzi, akiwa na Umri wa miaka 34.

Mnamo Oktoba 1952, Hussein alijiunga na Chuo cha Wafanyakazi na kupata shahada ya Uzamili kwenye sayansi ya kijeshi mnamo 1953. Mnamo tarehe Aprili 17,1954, Al-Shafei alihudumu kama Waziri wa Vita kwenye serikali ya kwanza ya Gamal Abdel Nasser, kisha akateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Jamii mwaka 1956, kuanzisha mfumo wa bima ya kijamii, misaada ya majira ya baridi, na treni ya huruma. Kisha akachukua nafasi ya Wizara ya Mipango.

Alishiriki katika mazungumzo ya Umoja kati ya Misri na Syria mnamo Februari 1958, kisha akateuliwa kuwa Waziri wa Awqaf na Masuala ya Al-Azhar na mjumbe wa Sekretarieti Kuu ya Umoja wa Kisoshalisti mwaka 1961, alisimamia Shirika la Ukaguzi wa Kati mwaka 1965, na akachukua Urais wa Mahakama ya Mapinduzi kwa maafisa wanaojiunga na Uasi ulioongozwa na Waziri wa Vita, Field Marshal Abdel Hakim Amer, baada ya kushindwa Juni 1967.

Abdel Nasser alimchagua kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri mwaka 1963, na akaendelea na wadhifa wake hadi Sadat alipoteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka 1969, kisha Sadat akamchagua kwa dhana yake ya Urais wa Jamhuri kama Makamu wake wa Rais mwaka 1970, na akaendelea kuwa madarakani hadi mwaka 1975, na kuacha wadhifa wake bila kufukuzwa au kujiuzulu, akatoweka katika maisha ya kisiasa, hadi alipofariki Ijumaa, Novemba 18, 2005, akiwa na Umri wa miaka 87, baada ya kuugua kwa miezi miwili.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy