Saad Zaghloul
Ukuaji wake
Kiongozi wa Misri Saad Pasha Zaghloul amezaliwa mnamo Julai,1858 katika kijiji cha Abyaneh mkoani mwa Kafr Elsheikh ,alikuwa yatima kabla ya kufikia miaka mitano kutoka umri wake baadaya kifo cha baba yake ambye ni Mkuu wa kijiji ,kuhusu mama yake ni Bi.Mariam binti wa mzee Abdo Barkat ambye ni moja ya wamiliki wakubwa zaidi ,mjumbe wake aliyemtunza ni Abdall Barkat .
Ufupi kuhusu maisha yake ya kielimu
Saad Zaghloul alipata elimu yake katika Kuttab ,kisha alijiunga Alazhar mnamo 1873, na alikuwa mwanafunzi wa Bw.Gamal Eldin Elafghany ,na Mzee Mohamed Abdo ,na Saad alifanya kazi katika gazati la (Elwakaa Almasria ) ikiwa anakosoa hukumu za baraza zinazofuatwa , ametoa ufupisho wake na ametoa maoni yake , hadi alifanya kazi katika Sheria .
Alioa Safya Zaghloul mnamo 1895 aliyeitwa baadaye kama (Mama wa Wamisri ),ambye ni msichana wa Mustafa Fahmy Pasha ambye ni moja Waziri Wakuu wa zamani wa Misri.
Maisha yake ya kisiasa
Saad alifanya kazi katika gazati la (Elwakaa Almasria ) ikiwa anakosoa hukumu za baraza zinazofuatwa , ametoa ufupisho wake na ametoa maoni yake, hadi Wizara ya Elprody iliona dharura ya kumhamisha kwa kufanya kazi kama msaidizi kwa Wizara ya ndani kutoka hapa alipata nafasi ya kushughulikia ulinzi wa sheria na masomo ya sheria ,milango ya Utetezi wa kisiasa na vitu vya kisiasa ,kisha punde si punde alifanya kazi pale hadi alionesha Mafanikio yake kisha amehamishwa kwa kufanya kazi kama katibu katika Kurugenzi la Giza .
Saad Zaghloul alishirki katika mapinduzi ya Orabi na aliandika makala dhidi ya ukoloni wa kiingereza ,ambapo alihamasisha watu kwa mapinduzi ,na aliita kwa kusimamisha utawala wa Khedive Tawfik uliokuwa ukikuza Waingereza, basi amekosa kazi yake .
Zaghloul alianza kazi yake katika Uwanja wa kisiasa ,kwa kujiunga kwake kwa upanda wa kisiasa kwa Kundi la El Manar , lililokuwa kujumuisha Watu wa Al Azhar ,waandishi na wanasiasa ,alishiriki katika Harakati kuu kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha Misri na alikuwa moja ya wakuu wa kuweka msingi kwa kuanzisha kwake mnamo 1907 na manmo wakati huo, saad ametetea kwa kitabu cha Kasam Amen, kikiwa na inwani ya (Uhuru wa Wanawake ) na mnamo1906 ameteuliwa kama Mkuu wa Wizara ya Elimu ,kisha kufanya kazi kama Mkuu wa Wizara ya Haki mnamo 1910 .
Saad akawa Naibu wa Mahali pawili kutoka pa Kairo, akashinda Mwakilishi aliyechaguliwa kwa Jumuyia ,na baada ya vita vya kwanza vya Dunia aliongoza upinzani katika Jumuyia ya kisheria iliyoshikilia baadaye Nguzo ya Kundi la Al Wafd, imeita kwa Uhuru na kufutwa Ulinzi wa kiingereza .
Kuanzisha kwa Chama cha Al Wafd
Mnamo 1918, Saad Zaghloul aliwaza kuunda Al Wafd ya kimisri ; kutetea kesi ya kimisri dhidi ya Ukoloni wa kiingereza na ilijumuisha kia Saad Zaghloul ,Abd Elziz Fahmy ,Ali Sharwy ,na wengine ,pia wamekusanya kutia saini kutoka wahusika wengine, kwa lengo la kuhakikishia sifa zao za kuwakilisha .
Mnamo Machi 8,1919, Saad Zaghloul na wenzake wengine walifungwa na walifukzwa kwa kisiwa cha Malta katika Bahari ya kati ,hilo ndilo lililokasirisha wamisri na lilikuwa kama chanzo ya kwanza cha mapinduzi ya 1919, yaliyokuwa sababu kuu ya Uongozi wa Saad Zaghloul .
Baada ya kurudi kwake kutoka Uhamisho ,Saad Zaghloul ameanzisha Chama cha Al Wafd cha kimisri, kilichofanikiwa kikubwa katika uchaguzi wa kibunge wa 1923, akawa Waziri Mkuu katika mwaka huo huo ,na aliendelea hadi kufikia 1924 .
Mnamo Novemba 24,1924 , kujiuzulu kwa Saad Zaghloul kumekubaliwa,alikuwa na mgogoro Pamoja na mfalme Foaud ,na chama cha wachache kinachofuata mfalme kutetea Katiba ,na Mapambano ya Kiongozi wa Umma yamefanikiwa kwa ushindi wa chama cha Al Wafd kwa wengi wa Bunge mara ya pili mnamo 1927 na Saad alichaguliwa kama Mkuu wa Bunge hadi kifo chake mnamo 1927 .
Kutoka Kauli zake Maarufu Zaidi
Usemi maarfufu zaidi wa kiongozi wa kimisri Saad Zaghloul ni sentensi maarufu (Hakuna Faida ) ,na ilihusiana kwa wengi kwa sababu ya mtindo wa kikoloni naye kupitia mazungumzo yake baada ya mapinduzi ya 1919,miongoni mwa mahusiano na mjumbe wa kiingereza ,wakati ambapo alijua kuwa kujadili pamoja nao hakutakuwa na mapya,kama anazungumza na mwenyewe ,lakini hakika ya kihistoria haikuwa kama hivyo kamwe.
Asili ya sentensi maarufu ilirejea ambapo mke wa Saad Zaghloul,Bi.Safya Zaghloul alipokuja alimpa dawa kabla ya kifo chake ,alimwambia sentensi iliyotajwa, ambapo alikuwa anasikia kifo chake kilikarbia,akitaka kutochukua dawa zaidi kwa sababu haitaleta matokeo wazi tena ,licha ya hayo ila kauli hiyo ilibaki maarufu zaidi inayotumiwa na wamisri; wakieleza dhuluma ya kisiasa na kukubali ugumu wa kufanya marekebisho .
Kifo chake
Mnamo Agosti 23, 1927, Saad Zaghloul alikufa na amezikwa katika Kaburi lake linalojulikana kwa nyumba ya Umma iliyojengwa mnamo 1931.