Omar al-Mukhtar...Simba wa Jangwa na Sheikh mkuu wa Wapambanaji

Omar al-Mukhtar...Simba wa Jangwa na Sheikh mkuu wa Wapambanaji
Omar al-Mukhtar...Simba wa Jangwa na Sheikh mkuu wa Wapambanaji

Katika historia ya kila taifa kuna wanaume wakubwa wameongoza mapambano kwa ajili ya kukomboa nchi zao na kuzifikisha Usalama kulingana na uwezo wao wa pekee na vipaji vya uongozi na ujasiri, waliweza kufikia malengo na matarajio ya watu wao, kwa hiyo walipata heshima na heshima na historia iliwahifadhi katika kumbukumbu yake.

Omar bin al-Mukhtar alizaliwa mnamo 1862, kijijini mwa Zawiyat Janzur katika Cyrenaica Mashariki mwa Libya, kwenye mibaka ya Misri, baba yake alifariki Dunia akiwa mdogo, ambapo alifariki alipokuwa akielekea Makkah Al-Mukarramah ili kuafanya ibada ya hijja pamoja na mkewe Aisha bint Moharib, na Al-Sheikh Al-Mujahid anahusisha kabila la "Al-Manfah" , ni moja ya makabila makubwa Al-Moravids katika Cyrenaica, Shekhe wa Zawiyat Janzur Al-Senusiyya, Hussein El-Gariani alimtunza kwa amri ya babake, alimwingiza katika shule ya Qurani Tukufu huko Zawiyat, akiwa na miaka tisa katika kona ya kijiji, kisha Omar akaelekea Jaghbub Oasis, ngome ya wito wa Senussi, ili kusoma elimu ya sheria, hadithi, tafsiri na lugha ya Kiarabu mikononi mwa mashekhe makubwa wa wito, wakiongozwa na Al-Mahdi as-Senussi.

Al-Mahdi as-Senussi alimkabidhi Ushekhe wa mji wa Zawiyat Al-Qusour, katika eneo la Al-Jabal Al-Akhdar mwaka wa 1897, wakati wa kipindi hicho alipata  jina la 'Bwana', ambalo hakuna mtu alilipata isipokuwa Mashekhe makubwa wa Senusiyya.

Omar al-Mukhtar alihamia Chad mwaka wa 1900, ili kueneza mafundisho ya dini ya kiislamu na kupinga wakoloni wa kifaransa katika nchi hiyo. Al-Mukhtar aliishi pia kwa miaka mingi katika Sudan, ambamo kulikuwa na uwepo mkubwa wa vuguvugu la Senusiyya, kama mwakilishi wa Al-Mahdi as-Senussi ambapo alisema kwa shangaa : " Kama tungekuwa na wanaume kumi kama Omar al-Mukhtar tungewatosha". 
Al-Mukhtar alikaa Qaru Magharibi mwa Sudan, kisha Al-Mahdi akamteua kuwa Sheikhe wa Zawiyat Ain Kalak. Pia alishiriki katika mapambano yaliyozuka kati ya Senusiyya na Wafaransa katika maeneo ya Kusini nchini Sudan, inaelezwa kuwa tangu safari yake kwa Sudan alipata jina la " Simba wa Jangwa".
Na riwaya inasema kuwa Omar Al-Mukhtar aliposafiri pamoja akiwa kiongozi wa ujumbe wakielekea Sudan, ulijumuisha: Bwana Khaled bin Mousa, Bwana Mohammed Al-Masalusi, Qarjila Al-Majbari na Khalifa ad-Dabbar Al-Zuway mmoja wa wajumbe wa Zawiyat Waw Fezzan. Na katika Kufra ujumbe ulipata msafara wa wafanyabiashara kutoka makabila ya Zuwayya na Al-Majabra, na wafanyabiashara wengine kutoka Tripoli na Benghazi wakijaandaa ili kusafiri Sudan, ujumbe ulijiunga na wafanyabiashara hao ambao wamezoea kutembea katika barabara za jangwa na wana uzoefu mzuri na njia zake.
Na wasafiri walipofikia katikati mwa jangwa karibu na Sudan, baadhi ya wafanyabiashara waliozoea kupita katika nje hii walisema kwamba : " Baada ya muda mfupi tutapita katika barabara mbaya ambayo hatuna nyingine, na kwa kawaida -isipokuwa kwa uchache tu- kuna ndani yake Simba anayeongoja mawindo yake kutoka misafara iliyopata barabara hii, na misafara ilizoea kuacha kwa simba ngamia kama mwanadamu huacha nyama kwa mbwa au baka, na misafara hupita kwa amani, na mzungumzaji alipendeza kwamba wote walishiriki katika bei ya ngamia mdoga na kumwachia simba alipotokea, lakini Omar Al-Mukhtar alikataa sana akisema: " Mrahaba uliowekwa wenye nguvu miongoni mwetu kwa wanyonge bila ya haki umebatilika, vipi ni Sawa kwetu kuwarudisha kwa mnyama? Ni dalili ya unyonge. Tutapambana na simba kwa silaha zetu akiingia katika njia yetu".
Na baadhi ya wasafiri walijaribu kumzuwia na nia yake, akawajibu kwa kusema :" Nina aibu ninaporudi na kusema: Nilimwacha ngamia kwa mnyama aliyepita njia yangu, na nipo tayari kulinda ninacho pamoja nami. Na nyinyi wote ni wachungaji na wote mnawajibika kwa kundi lake, ni tabia mbaya tunapaswa iondoe. Msafara ulikaribu korido nyembamba, simba akatoka katika mahali yake aliyoichukua kwenye moja ya balcony ya korido. Mmoja ya wafanyabiashara alisema -alikuwa na hofu na mandhari- :" nipo tayari kuacha mmoja ya ngamia wangu, wala msijaribu kucheza na simba". Omar Al-Mukhtar akakimbia na bunduki yake - ilikuwa na aina ya Kigiriki- na akampiga simba kwa risasi ya kwanza, ilimpiga lakini bila kumuua na simba akaelekea kwa nguvu kwa msafara, Omar akampiga kwa risasi nyingine na ilimwangusha, Omar Al-Mukhtar akasisitiza kuchuna ngozi yake ili wenye misafara wamuone, na walifanya hivyo.
Katika taarifa nyingine alipata jina hilo kulingana na ushujaa na ujasiri wake katika kuwapinga wakoloni wa Italia katika vita vikali vilivyojiri katika maeneo mbalimbali ya jangwa ya Libya ambavyo vilitumia vifaru katika jangwa kwa mara ya kwanza. Al-Mukhtar alizunguka Afrika Mashariki na Jangwa kubwa, ambapo alijenga misikiti na kona ili kuwafundisha watu dini Yao na kueneza Islam baina yao.
Na baada ya kifo cha Mohammed Al-Mahdi as-Senussi, mwaka wa 1902, Omar Al-Mukhtar alirudi Cyrenaica kwa ombi la uongozi wa Senusiyya, ili kuwa Sheikhe wa mji wa Zawiyat Al-Qusour mara tena katika mwaka wa 1906. Al-Mukhtar alibaki katika ngazi hii kwa miaka 8 hadi mwaka wa 1911, na aliosimamia vyema kiasi kwamba Usultani wa Ottoman katika wakati huo, ulikaribusha uongozi wake wa eneo hilo, ambalo alilileta utulivu.

Omar al-Mukhtar hakuwa shujaa alipokuwa Sheikh mkubwa kama wengi wanavyoamini, lakini alikuwa shujaa katika maisha yake yote. Katika mwaka wa 1908, alishiriki katika vita baina ya wenye Senusiyya na vikosi vya Uingereza katika mibaka ya Libya-Misri.

Mnamo Septemba, mwaka wa 1911, Italia ilituma onyo kwa serikali ya Ottoman ambalo lina tishio la kukalia Tripoli na Benghazi, jambo ambalo serikali ya Ottoman ililikutana kwa aina ya udhaifu na kuridhika ikiomba kukaa kwa ajili ya kufanya mazungumzo, lililotoa Italia nia ya kutangaza kwamba Libya ni koloni la Italia na ilituma meli zake za kivita ili kukaa katika mji wa pwani ya Libya. Na mnamo Septemba 29, mwaka wa 1911, meli za kivita zilianza kushambulia pwani ya Libya, Omar Al-Mukhtar aliharakisha kurudi kwenye Zawiyat Al-Qusour ili kuandaa harakati ya jihadi dhidi ya wavamizi wa Italia. Alishiriki katika vita vya Al-Salawi mwishoni mwa mwaka wa 1911.

Al-Mukhtar, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 53, alichukua uongozi wa "Baraza Kuu" la operesheni za jihadi, ambalo lilisimamia vita kubwa zaidi katika historia ya Libya na wavamizi wa Italia, hadi Mujahidina kwa uongozi wake wakawashinda vikali, wavamizi wa Italia,waliua mamia ya maafisa na askari, wakati huo serikali ya Italia ilianza kutambua utu wa Omar al-Mukhtar, kama jina lake lilianza kuenea kati ya uongozi wa Italia kama kamanda wa kijeshi wa Kiislamu aliyesababisha hasara nyingi kwa wakoloni ,vishawishi vyote vilivyowasilishwa kwake na serikali ya Italia havikufaulu kukatisha tamaa yake katika jihadi.

Kwa kuzingatia kukosa uwezo kwa serikali ya Italia kumpinga kiongozi huyo mkuu, ilikimbilia Astana kuhitimisha mkataba wa Amani na serikali ya Ottoman, ambapo Mkataba wa Lausanne ulitiwa saini kati ya nchi hizo mbili mnamo Oktoba 21, 1912,kutokana na hali hiyo, serikali ya Ottoman iliondoa majeshi yake kwa kuamini kwamba makubaliano haya yalimaliza vita, na licha ya kwamba majeshi ya Italia yaliondoa majeshi yao katika miji ya Libya, walifanya operesheni nyingi za kichochezi, kwani walitumbukiza wengi.

 Mujahidina kuingia magerezani na kushambulia mali zao mbalimbali, Jambo ambalo lilifananishwa na Mujahidina wa Libya kwa kuwateka nyara na kuwaua wanajeshi wa Italia na kujaribu kuwatia hasara nyingi iwezekanavyo, ikiwa ni pamoja na Vita vya Derna mnamo Mei 1913, ambayo ilidumu kwa siku mbili, na kumalizika kwa kifo cha askari 70 wa Italia na kujeruhiwa kwa wengine 400, na Vita vya Bushmal huko Ain Marah mnamo Oktoba 1913, na vile vile vita vya Umm Shakhanb, Shalima, na Zueitina mnamo Februari 1914, ambapo Al-Mukhtar alihamia kati ya safu za vita.

Baada ya mapinduzi ya kifashisti nchini Italia mwezi Oktoba mwaka wa 1922, hali ndani ya Libya ilibadilika, na shinikizo likaongezeka kwa Mfalme wa Libya wakati huo, Muhammad Idris al-Senussi, kukabidhi Libya kwa mkoloni wa Italia, hivyo yeye alilazimishwa kuondoka nchini na kwenda kuishi Misri, na akakabidhi masuala ya kijeshi na kisiasa kwa Omar al-Mukhtar.

Na baada ya kuthibitishwa kwa Mukhtar makusudio ya Waitalia katika uchokozi huo, alikwenda Misri mwaka 1923, ili kushauriana na Mfalme Idris kuhusiana na suala la nchi, na baada ya kurejea alipanga safu za Mujahidina na kushika uongozi wao , na baada ya uvamizi wa Italia katika mji wa Ajdabiya, makao makuu ya uongozi wa Libya, maagano na mikataba yote ilibatilika,mujahidina wakaondoka katika mji huo, na Italia ikaanza kusonga mbele na majeshi yake kutoka maeneo kadhaa kuelekea Mlima wa Kijani, na wakati huo huo umati wa Mujahidina wakakimbia kuunda majukumu na kuungana chini ya uongozi wa Omar Al-Mukhtar, watu pia walichukua hatua ya kuwapa Mujahidina vifaa, vifaa na silaha, na Waitaliano walipochoshwa na kushindwa na Mujahidina, walitaka kuwazuia wasiwape, hivyo wakatafuta kukalia” Al- Jaghbub",kampeni kubwa ilielekezwa kwake mnamo Februari 1926, kwani kuanguka kwake kulifanya mizigo na shida mpya kwa Mujahidina, wakiongozwa na Omar Al-Mukhtar, lakini mtu huyo alibeba mzigo huo kikamilifu kwa azimio la wakuu na dhamira ya mashujaa. .

 Licha ya mujahidina kuzingirwa na kukatwa kutoka kwenye vituo vyao vya ugavi, matukio hayo hayakuwaathiri wao na azma yao, na ushindi uliendelea, jambo ambalo liliifanya Italia kufikiria upya mipango yake na kufanya mabadiliko makubwa,Mussolini aliamuru mabadiliko katika uongozi wa kijeshi, kwani alimteua Badoglio kama mtawala wa kijeshi wa Libya mnamo Januari 1929, na mabadiliko haya ni mwanzo wa awamu ya maamuzi kati ya Waitaliano na Mujahidina.

 Mtawala mpya wa Libya alionesha nia yake ya kutaka amani kupata muda unaohitajika wa kutekeleza mipango yake na kubadili mtindo wa mapigano wa askari wake, na akaomba kufanya mazungumzo na Omar Al-Mukhtar, na sheikh akaitikia wito wa amani,na pale Al-Mukhtar alipoona kwamba mazungumzo hayo yalimpa chaguo baina ya kuondoka nchini kwenda Hijaz au Misri, au kukaa Cyrenaica, kuhitimisha jihadi na kujisalimisha kwa malipo ya pesa na vishawishi, na kama ilivyo desturi ya mashujaa na mujahidina. Sheikh alikataa isipokuwa kuendeleza jihadi mpaka ushindi au kifo cha kishahidi.

 Na katika mkutano wa "Sidi Rahouma" uliohudhuriwa na Omar Al-Mukhtar, Pietro Badoglio, Gavana wa Tripolitania Magharibi na Cyrenaica, na Naibu Gavana wa Cyrenaica Sechliani,Mukhtar aliwasilisha masharti ya kusitisha mapigano, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa tena kwa shule za Waarabu, kuachiliwa kwa wafungwa, na kukomesha uvamizi wa vijiji na vitongoji.

 Wakati Waitaliano walitoa ofa, iliyokuwa sawa na rushwa, ikiwa ni pamoja na pensheni ya kuvutia kwa mukhtar, wakati watu wake wengine walijisalimisha wenyewe na silaha zao kwa afisa wa Kiitaliano aliyeitwa na Roma.

Ofa hiyo ilitolewa kupitia upatanishi wa Al-Hassan bin Al-Ridha Al-Senussi, ambao ulikataliwa na Al-Mukhtar na Al-Hassan alimkemea Al-Ridha, akisema, “Wamekuhadaa, mwanangu, kwa vitu vinavyoharibika vya Dunia. 
Mazungumzo magumu yaliendelea zaidi ya mara moja, na yakaisha yalipoanza
Hata hivyo, Badoglio, katika mkutano na waandishi wa habari, alizindua uvumi kwamba "Omar al-Mukhtar na watu wake walijisalimisha," ambayo baadaye ilikanushwa na ukweli.

 Wakati Graziani aliposhindwa kuwashinda Mukhtar kwa njia ya mazungumzo, alikimbilia kwenye kambi za mateso za watu wengi jangwani, akazingira kwa waya wenye miiba, na akaingiza makabila mengi ya Libya huko Cyrenaica, katika jaribio la kumshinikiza Mukhtar kujisalimisha.

Hata hivyo, Mukhtar hakukubali shinikizo, kwa kuzingatia kwamba kuacha upinzani na kusalimu amri ilikuwa "usaliti dhidi ya Walibya."

 Mwandishi wa habari wa Italia Cannivar alielezea kuwasili kwa Omar al-Mukhtar kwenye mazungumzo, "akiwa amezungukwa na mashujaa wake, wakati mshindi anafika ambaye alikuja kuamuru masharti yake kwa walioshindwa."

Misimamo thabiti ya Mukhtar iliifanya Italia kubadili mbinu zake kwa kumteua Graziani, ambaye alikuwa na tabia ya kikatili na ya umwagaji damu, kutekeleza mpango usio na kifani wa maangamizi na maangamizi katika historia,Ambapo aliamuru kuwekwa kwa waya wa miba kwenye mpaka wa Libya na Misri ili kuzuia kuwasili kwa vifaa na risasi, kuanzishwa kwa mahakama ya dharura, kufunguliwa kwa milango ya magereza katika kila mji na kijiji, kusimamishwa kwa mti kila upande, kuzingirwa kwa mujahidina katika Mlima wa Kijani na kukaliwa na Kufra.

Katika kitabu chake "Omar Al-Mukhtar, Shahidi wa Uislamu na Simba wa Jangwani," Muhammad Mahmoud Ismail anasema kwamba Al-Mukhtar alichapisha ujumbe kwa Walibya wakati huo ambapo alisema kwamba alikubali uasi huo kwa kubadilishana, kwa kurudi kwa Mwanamfalme Muhammad Idris Al-Senussi, kuondolewa kwa Waitaliano kutoka Jaghbub, na msamaha wa jumla kwa wafungwa wote wa kisiasa.

Waitaliano hawakutekeleza masharti ya kusitisha mapigano, na kabla ya mwisho wake walidai kuongezwa kwake kwa kisingizio cha safari ya Badoglio kwenda Roma, kwa hivyo iliongezwa kwa siku kumi tena siku ishirini. 
Hivyo, Omar Al-Mukhtar alipogundua kwamba Waitaliano wanataka kununua muda, alizidisha operesheni za upinzani, hivyo Mussolini akamteua Jenerali Graziani kuchukua nafasi ya Badoglio, Waitaliano walizidisha shinikizo lao kwa Al-Mukhtar, na eneo la Kufra likaangukia mikononi mwao.

Mnamo Septemba 11, 1931, wakati Sheikh Omar Al-Mukhtar anafanya kazi za upelelezi katika eneo la Sultana na masahaba zake, majeshi ya Italia yalifika eneo lake na kutuma vikosi kumzingira,Walipata kujua utu wake, na mara moja akahamishiwa Marsa Sousse, na kisha Benghazi, ambako aliwekwa katika gereza kubwa katika eneo la Sidi Akher Yabish.

Siku tatu baadaye, mnamo Septemba 14, mwaka huo huo, kiongozi wa kiitalia "Graziani" alifikia Benghazi, na akaharakisha kuandaa "mahakama maalum" yenye upuzi ya shahidi Sheikh, ilimaliza kwa kutolewa kwa hukumu ya kifo kwa kunyongwa, mnamo tarehe 15  ya mwezi huo huo, na asubuhi iliyofuata kesi hiyo, yaani, mnamo Septemba 16, 1931, Sheikh mkuu aliletwa akiwa amefungwa minyororo, na kichwa chake kikiwa juu, na kwa tabasamu ya kuridhika na hukumu na hatima , na wakati hukumu hiyo ilipotafsiriwa kwake, Sheikh alisema, "Hukumu ni kwa Mungu tu ... Hapana kwa hukumu yako bandia... Sisi ni wa Mungu, na kwake Yeye tutarejea." Roho yake safi ilipaa kwa Mungu wake , ikimlalamikia kuhusu wadhalimu na ukandamizaji wa wakoloni.

Mbele ya Zaidi ya watu  20,000, kutoka wana wa Barqa, ambao walimuaga  kwa vigelegele na idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa walipelekwa nje kutazama mauaji hayo. Omar Al-Mukhtar aliletwa kwenye jukwaa la mauaji wakati akisoma maneno ya Mwenyezi: (Ewe nafsi iliyotua, rejea kwa Mola wako Mlezi, umeridhika na umemridhisha), na hukumu hiyo ilitekelezwa.

Jenerali Rodolfo Graziani aliandika kuhusu hilo katika kitabu chake "Barqa yenye utulivu"  Cirenaica pacificata: Inaonekana kwangu kwamba mtu aliyesimama mbele yangu ni mtu ambaye si kama wanaume wengine; ana uwepo na heshima licha ya kuhisi uchungu wa kifungo. Hapa anasimama mbele ya ofisi yangu, tukimuuliza, na anajibu kwa sauti tulivu na wazi.

Graziani: Kwa nini ulipambana sana  serikali kuu?

Al-Mukhtar: Kwa ajili ya Dini na Nchi yangu.

Graziani : Na utafikia wapi kwa dhana yako hii ?

Al-Mukhtar: Hakuna chochote isipokuwa kufukuzwa kwenu. Kwa sababu ninyi ni wabakaji, vita ni wajibu wetu na ushindi ni kutoka kwa Mungu tu." 

Graziani alisema  mwisho wa mkutano na Omar Al-Mukhtar kwamba "aliposimama kujiandaa kuondoka, paji lake la uso lilikuwa angavu kama kwamba halo ya mwanga inamzunguka, na moyo wangu ulitetemeka kutoka kwa ukuu wa hali hiyo, mimi ambaye nilipigana vita na vita vya ulimwengu, na jangwa, na licha ya hili, midomo yangu ilikuwa ikitetemeka, na sikuweza kusema herufi hata moja." Katika kitabu hicho, alitaja pia kwamba "kosa lake pekee lilikuwa kwamba alituchukia sana."

Jenerali Graziani hapo awali, alitangaza zawadi ya Franc 200,000 kwa yoyote  atakayemleta Al-Mukhtar hai ama maiti.

Al-Mukhtar alikuwa na akili timamu, na alijulikana kwa umakini, uthabiti, uadilifu, na uvumilivu. alikuwa na ufahamu mpana wa mambo ya mazingira yaliyomzunguka, na alikuwa na ufahamu wa hali ya mazingira ambayo aliishi, na ujuzi mpana wa matukio ya kikabila na historia ya matukio yake, na ujuzi wa nasaba na viungo vinavyounganisha makabila haya na kila mmoja, na mila na desturi zake, na maeneo yake, kwa hivyo alielewa njia za kutatua ushindani wa Bedouin. 

Alikuwa mtaalam katika njia za jangwa na kwenye njia kutoka Barqa hadi Misri na Sudan nje ya nchi na Jaghbub na Kufra ndani . Pia alikuwa na ujuzi wa aina ya mimea ya Barqa na sifa  zake za kitiba . Pia alikuwa na ufahamu wa magonjwa yanayoathiri ng'ombe na mbinu za matibabu yake.

Katikati ya jihadi, angeifunga Qur'an mara moja kwa wiki, kuifundisha kwa wavulana, kukaa usiku, kufunga siku mbili kwa wiki, na kulala masaa machache tu, mengi ya chakula chake ni  maziwa ya mbuzi, tende na mkate. Yote anayomiliki katika ulimwengu huu ni Qur'an ndogo ambayo alirithi kutoka kwa baba yake, Miwani aliyoichukua kutoka kwa jenerali wa kiitalia, farasi aliyopewa na rafiki yake Youssef Bourahil, na nguo mbili zinazoosha moja na kuvaa nyingine.

Alikuwa mfano wa ukombozi wa roho na damu, Al-Mukhtar akawa mmoja wa wajihadi  ambao hawajasahaulika katika kumbukumbu ya historia, mpinzani mkali na shujaa anatetea sana nchi yake, inatosha yeye kujivuna kwamba msemo wake (hatutajisalimu ama,  kushinda au kufa) ulikuwa ni jina la maisha yake akikataa kusalimu,na kukaribisha kifo na ushuhuda", na inatosha alijivunia kwamba maneno yake, "Vizazi vitanifuata kupigana nanyi, lakini maisha yangu yatakuwa marefu kuliko maisha ya uliyemuua " yamethibitishwa kuwa ya kweli. Miaka michache baada ya kifo chake, mnamo 1943, Libya ilipata uhuru kutoka kwa urithi wa ukoloni na Al- Mukhtar akawa katika kumbukumbu na historia.

Vyanzo

Tovuti ya BBC.

Tovuti ya Mayadeen.

Tovuti ya Misri na Afrika.