Luteni Jenerali Aziz Al-Masry

Imetafsiriwa na/ Alaa Zaki
Imeharirwa na/ Mervat Sakr
Abd El-Aziz Zakaria Ali alizaliwa mwaka wa 1880, ana asili ya Circassian kutoka familia ambayo asili yake ni Caucasus na inajulikana kama familia ya Shahalba, aliishi Iraq kwa muda kisha akahamia Misri. alikuwa na umri wa miaka kumi ambapo baba wake alifariki dunia, na mama yake alimtunza sana, lakini alifariki dunia miaka mitano baada ya kifo cha baba yake. Alifadhiliwa na dada yake mke wa Ali Pasha Zulfiqar, Mkoa wa Kairo.
Aziz alimaliza masomo yake ya msingi kwenye shule ya Al-Tawfiqiyah na alipata shahada ya pili mwaka wa 1898, na jina lake hapo ni Abd El-Aziz Zaki. Alipokuwa Istanbul alijitwalia jina la Abd El-Aziz Ali, na Waturuki walikuwa wakiliita. "Kairo - Li - Aziz - Ali", maana yake "Aziz Ali Al-Masry", ni jina ambalo anajulikana.
Aziz alitaka kujiunga na Chuo cha Kijeshi na akaingia Mhandisi Khana wa Misri ili kusoma hisabati, trigonometry, sayansi ya kisasa, na alijifunza Kituruki ili kuandaliza kujiunga na Chuo cha Kijeshi huko Istanbul. Al-Masry alifaulu katika masomo na alikuwa mmoja wa wanafunzi wa kwanza katika chuo, kilichomsaidia kujiunga na Chuo cha Wafanyakazi wa Vita, ambako alihitimu mwaka wa 1905.
Mnamo wa miaka yake ya masomo, alipendezwa na maofisa wa Ujerumani waliokuwa wakifundisha, na aliheshimu ndani yao mawazo mazito, kufikiri vizuri, heshima kwa wanadamu, na staha ya kazi. Mnamo wa kuwepo wake kwenye Chuo cha Kijeshi, alikutana na vijana kadhaa wa Kiarabu na Waturuki ambao hawakuridhika na Utawala wa Ottoman, wakiwemo Nuri Al-Saeed, Jaafar Al-Askari, na Mustafa Kemal Ataturk. Ataturk alikuwa ameunda (Jumuiya ya Nchi) mwaka wa 1906, na kisha chama hiki kilijiunga na Jumuiya ya (Muungano na Maendeleo) iliyolenga kumuondoa madarakani Sultani Abd El-Hamid na kuanzisha nchi ya kidemokrasia ya Uturuki, ni chama ambacho Aziz Al-Masry alikuwa mwanachama, na juhudi za jumuiya hiyo ziliishia mapinduzi ya kina mwaka wa 1909, yaliyosababisha kutengwa na uhamisho wa Sultani Abd El-Hamid na kuteuliwa kwa Sultani Muhammad wa tano badala yake.
Baada ya Wanajeshi wa Uturuki walichukua Udhibiti wa mambo ya nchi, mzozo ulizuka kati yao na maafisa wa Kiarabu waliokuwa na matumaini ya kupata aina ya Utawala huru wa nchi zao, na wakati jambo hilo halikuhakikisha, wito wa Uarabu ulianza kushika kasi, na Aziz Al-Masry alichukua jukumu kubwa katika wito huu, kwa hivyo maafisa wa Kiarabu walimchagua ili kuwaongoza. Vyama vya Waarabu vilivyojitenga na Jumuiya ya (Muungano na Maendeleo) na Aziz Al-Masry akaunda Jumuiya ya (Al-Kahtaniyah). Hata hivyo, mapinduzi ya Yemen dhidi ya Utawala wa Ottoman yalifanyika mwaka wa 1911, na Aziz Al-Masry alikwenda kichwa wa jeshi la Uturuki ili kukandamiza mapinduzi na kuweza kusimamisha damu ya pande zote mbili kwa kufanya mapatano ya amani na Yahya Hamid Al-Din, Imamu wa Yemen. Kisha, Aziz Al-Masry akasafiri hadi Libya ili kupigana na Waitalia.
Al-Masry alirejea Istanbul mwaka wa 1913, wakati ambapo uadui na mateso ya Uturuki dhidi ya Waarabu yalikuwa yamefikia kilele chake. Alijiuzulu kutoka jeshi na kujishughulisha kufanya kazi ndani ya safu ya Harakati ya Waarabu, na alianzisha mwaka huo huo, kwa Ushirikiano na kundi la maofisa wa Kiarabu, (Jumuiya ya Maagano), ambayo Uanachama wake ulijumuisha maafisa 315 wa Kiarabu. Mpango wa (Jumuiya ya Maagano) ulijikita katika kuanzisha muungano wa shirikisho uliojumuisha watu wote walio chini ya Milki ya Ottoman, ikiwa ni pamoja na Misri, Sudani, Tripoli, Morocco, na Tunisia, huku kila taifa likianzisha chombo huru cha Utawala na Sultani wa Ottoman akiwa rais wa mfano, si halisi wa muungano.
Shughuli ya utaifa ya Aziz Al-Masry iliongezeka, jambo lililofanya mamlaka ya Uturuki ili kumkamata Februari, mwaka wa 1914 na kumweka mahakamani, wakimtuhumu kwa mashtaka kadhaa ya Uwongo. Mahakama ya Kijeshi ya Uturuki ilimhukumu kifo, jambo lililozua harakati ya Upinzani ya kitaifa katika maeneo yote ya Waarabu. Telegramu na barua zilifika kutoka sehemu zote za ulimwengu wa Kiarabu, zikiomba kutoka Sultani Muhammad Rashad alimjaribia Anwar Pasha, aliyekuwa nyuma ya kesi hiyo, na kumwachilia shujaa (Aziz Al-Masry). Mkuu wa washairi, Ahmed Shawki, alimwandikia Sultani shairi ambamo alimsifu Aziz Al-Masry, shujaa wa Yemen na Libya, na miongoni mwao ni kauli yake: (Wallahi kwa Uislamu, kwa jeraha linaloendelea kutiririka Upande wa mwezi mpevu mpaka mfungwa afunguliwe - dhamana juu ya simba ni nzito) na Sultani Muhammad Rashad alilazimika kumwachilia huru (Aziz Al-Masry) aliyerudi Misri, lakini mwanamapinduzi hatulii, ambapo Al-Masry haina wasiwasi wala fikra isipokuwa kwa Umoja na Uhuru wa Waarabu.
Al-Masry alisafiri hadi Hijaz ili kuchangia kuandaa jeshi la Waarabu, baada ya wakuu wawili (Ali na Faisal), wana wa Sharif Hussein, walitangaza, mnamo wa tarehe 5, mwezi wa Juni, mwaka wa 1916, Uhuru wa Waarabu kutoka kwa Utawala wa Uturuki, na mapinduzi ya Waarabu yalichochewa huko Hijaz, na hapo Sharif Hussein alimteua kuwa katibu mdogo wa Wizara ya Vita na kamanda wa jeshi la Waarabu, ambapo alipata mafanikio makubwa katika kujenga jeshi na kuliongoza kwa ushindi.
Aziz Al-Masry aliteseka kutokana na kashfa, zilizokuwa rahisi kwao kutumia asili na sifa za utu wake wenye nguvu katika kumsawiri kwa njia iliyotaka uasi, kwa sababu Uwezo wa Aziz Al-Masry ulimstahilisha kuwa mwanasiasa wa kwanza wa nchi sio tu waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi. Kashfa hizi zilizusha mzozo kati ya (Aziz Al-Masry) na Sharif Hussein, kwa sababu Al-Masry alikataa mara kwa mara ofa za Waingereza za kushirikiana nao, kwa sababu alijua ukweli juu ya matamanio yao katika nchi za Kiarabu. Hivyo, Aziz Al-Masry alikuta kuwa afadhali arudi katika mji aliozaliwa (Kairo) mnamo wa Machi, mwaka wa 1917, ambapo kwa miaka 20, alikaa mbali na kazi ya moja kwa moja ya kijeshi na kisiasa, ingawa hakujiepusha na kile ambacho ni muhimu zaidi kuliko hii, inayokuza vizazi vikubwa ambavyo kutoka kwao alichukua Uzalendo, mapinduzi, na kazi ya Umma. Kwa hiyo, mara tu alipofika Kairo, Unyanyasaji wao dhidi yake ulianza, hasa baada ya kukataa kushirikiana nao huko Iraq na Yemen, wakamtolea kuwa mfalme, akawajibu kwa kusema: "Vipi nitakaa kwenye kiti cha enzi cha Yemen na hali ni cha watu wake na si nyinyi?". Alisafiri hadi Hispania uhamishoni, na hatua hii ilitarajiwa baada ya majaribio yao ya kumshawishi ajiunge nao kushindwa.
Aziz Al-Masry alisafiri kutoka Hispania hadi Ujerumani baada ya kumalizika kwa Vita vya Kwanza vya Dunia. Katika Ujerumani, Aziz Al-Masry alifanya kazi kama mwalimu kwenye Chuo cha Wafanyakazi wa Vita, ambako alisoma Uzoefu wake katika vita vyake dhidi ya Wabulgaria, na njia ya vita vya msituni aliyovumbua katika maeneo ya milimani, katikati ya jangwa, na misitu ya Libya dhidi ya Waitaliano. Shujaa huyo (Aziz Al-Masry) alibaki uhamishoni kutoka nchi yake hadi aliporejea Misri mwaka wa 1924, baada ya chama cha Wafd kuingia madarakani, na miezi michache baada ya kurejea alipokea barua kutoka kwa rafiki yake na mwenzake katika jeshi huko Iraq, Afisa Yassin Al-Hashimi, aliyekuja kuwa Waziri Mkuu wa Iraq, akimtaka aende kwake haraka, akakubali mwaliko huo, ambapo alikutana na watu wengi wa Jumuiya ya Maagano waliokuwa maafisa wa Iraqi katika jeshi la Ottoman, kisha wakaja ili kufanya kazi kwenye jeshi la Iraq.
Al-Hashimi alimwambia kuwa anafikiria kufanya mapinduzi ya kijeshi nchini Iraq na kutimiza ndoto yake ya zamani ya kuifanya Baghdad kuwa mahali pa kuanzia kuwa nchi huru ya Kiarabu itakayokuwa mwanzo wa kuzikomboa nchi nyingine. Alimwomba amsaidie kuandaa mpango ufaao, na Waingereza hawakuridhika na uwepo wa Aziz Al-Masry huko Iraq, kwa hivyo Balozi Mkuu wa Uingereza akamwita na kumuuliza juu ya siri ya Uwepo wake. Aziz akajibu kuhusu anachofanya Iraq, na alikuwa Mwingereza mgeni, huku Aziz akiona uwepo wake huko Iraq, nchi yake ya Waarabu, kuwa ni jambo la asili ambalo asingeulizwa. Walimpa nafasi ya kuteuliwa kuwa rais wa Kampuni ya Mafuta ya Iraq, na mshahara wa watu pauni elfu tano, na nyumba ya kifahari huko London, lakini alikataa, hivyo amri zilitolewa kwa kumfukuza kutoka Iraq.
Katika mwaka wa 1926, Aziz Al-Masry alirudi Kairo, na kwa kuthamini jukumu lake la kizalendo na kitaifa na kwa kutambua fikra zake za kijeshi, Muhammad Mahmoud Pasha, Waziri Mkuu wa Misri mnamo wa mwaka wa 1928, alimchagua kama mkurugenzi wa Chuo cha Polisi. Alianzisha mbinu mpya za ufundishaji na elimu na akachagua washiriki wa kitivo kutoka miongoni mwa maafisa waliobobea nchini Misri na akawa chuo hiki. Alikuwa na sifa pana kutokana na juhudi za wazi za Aziz Al-Masry na kile alichokuwa anajulikana kwa kuwa na msimamo, Umakini, na kipaji cha Uandalizi na Usimamizi, na maarifa ya encyclopedic, yaliyomvutia Mfalme Fouad, Mfalme wa Misri, na kile alichokiunda katika Chuo cha Polisi, hivyo akamchagua kuwa mkuu wa kwanza wa Prince Farouk, Mfalme wa Taji.
Alipandishwa cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Jeshi la Misri na hivyo kumfanya kuwa Mmisri wa kwanza kushika wadhifa huu, lakini Aziz Al-Masry alijaaliwa kuwa mwanamapinduzi wa mara kwa mara baada ya Waingereza kumuondoa katika nafasi yake ambayo hakuwa alitumia zaidi ya mwaka mmoja ndani.
Katika tarehe ya 16, mwezi wa Mei, mwaka wa 1941, Aziz Al-Masry alipanda ndege ya Usambazaji kutoka Uwanja wa ndege wa kijeshi huko Almaza, pamoja na Hussein Zulfikar Sabry na Abd el-Moneim Abd el-Raouf, na injini iliharibika na ndege ilitua kwenye shamba karibu na Kalyoub. Na katika saa nne asubuhi, Aziz aligonga mlango wa afisa wa polisi wa Misri anayemfahamu na kumpa salamu ya kijeshi, hakujua juu ya kutoroka, akaweka gari la kituo cha polisi lililompeleka kwenye uwanja wa Opera. Hilo lilikuwa katika enzi za wizara ya Hussein Siri Pasha.
Kisha habari zikatangazwa, na polisi hawakupata mahali alipo Aziz Al-Masry, hadi uchunguzi wa polisi ulipobaini kuwa Muhammad Hussein (baba yake Ahmed Hussein, kiongozi wa Chama cha Misri ya vijana), alikimbia na alitaka kukamatwa, alitembelea mara kwa mara nyumba fulani huko Imbaba, hivyo ofisa huyo (Ibrahim Imam), ofisa wa polisi wa kisiasa, alivamia nyumba yake, aliyefungwa tarehe ya 4, mwezi wa Juni, mwaka wa 1941, hadi serikali ya Al-Nahhas Pasha ilipomwachilia huru mwaka uliofuata. Alikamatwa tena tarehe 13, mwezi wa Agosti, mwaka wa 1942, na kutuhumiwa kuwasiliana na Wajerumani, kwa mujibu wa maelezo ya Anwar El-Sadat, itakayotolewa tarehe 20, mwezi wa Novemba, mwaka wa 1944.
Kisha Vita vya Palestina vya 1948 vilikuwa vita kabla ya mwisho, vilivyofurahia shughuli, kutiwa moyo na mipango ya Aziz Al-Masry, kama alivyofanya jitihada kubwa katika kuandaa vita vya kujitolea katika vita hivi, na wengi wa watu hao wa kujitolea walikuwa wanafunzi wake wa karibu, aliojichagua mwenyewe, na kuwahimiza wajiuzulu kutoka kwa majeshi ya kawaida ya kijeshi. Na kujiunga na vikosi vya kujitolea vya Misri vilivyopewa sifa ya kuhifadhi sehemu kubwa ya ardhi ya Palestina na kuwazuia Israeli kula zaidi ya ilivyokuwa tayari kula.
Aziz Al-Masry alichangia katika vita vya wapiganaji wa msituni wa Kimisri kwenye Mfereji mwaka wa 1951. Aziz Al-Masry alifanya juhudi kubwa katika kupanga vikosi vya Wamisri katika upinzani huu, na kama ilivyokuwa kawaida katika matukio yake ya kimahesabu na ya werevu, alichukua fursa hiyo ya uhusiano wake na Mkoa wa Kairo wakati huo, Fouad Shirin Pasha, na kutoweka nyumbani kwake, ni mahali ambapo mamlaka hakuwa na nia ya kumtafuta.
Kituo cha mwisho katika maisha ya kijeshi na kisiasa ya Aziz Al-Masry kilikuwa ni kushirikiana kwake na maafisa huru. Anwar El-Sadat alikuwa wa kwanza wa maafisa huru kukutana naye, kwani angemtembelea nyumbani kwake miongoni mwa vijana wengine wa Misri waliokuwa wakijadiliana naye mambo ya kisiasa ya nchi. Alifahamu kuwepo kwa shirika changa katika jeshi linalofanya kazi kuondoa nchi ya mfalme na Waingereza, na kuwa Sadat alikuwa sehemu ya shirika hili.
Anwar El-Sadat akawa afisa wa Uhusiano kati ya Aziz Al-Masry na maafisa huru na akaamua kuwa baba yao wa kiroho. Na baada ya mafanikio ya mapinduzi hayo, alimshauri Gamal Abdel Nasser kutompeleka Farouk mahakamani na aridhike na kitendo chake cha kutekwa nyara kiti cha enzi.
Kwenye kitabu chake, "Siri za Mapinduzi ya Misri", Sadat anafichua siri ya Upendo wake na wenzake wa Al-Masry, akisema: "Tulijua anachokitaka kwa jeshi la Misri katika suala la nguvu na nguvu, na tukaanza ili kufurahia Ufufuo halisi alioanzisha jeshini, na tulikuwa tukisikia mengi kuhusu hadithi zilizosimuliwa kuhusu majaribio yake ya mageuzi, na matatizo na vikwazo vinavyowekwa mbele yake".
Sadat anaongeza: "Wakati majenerali walipomsaliti, na yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wao, na wakawaeleza yale yaliyokuwa moyoni mwake kwa Waingereza, Uamuzi ulitolewa wa kumweka chini ya kizuizi cha nyumbani, jambo lililokuja kama kengele kubwa inayogonga masikioni mwetu. Tulizungumza juu yake kwa muda mrefu, na hamu yangu kubwa katika mada hii ikawa wazi kwangu, na nilionesha hamu kubwa ya Ulazima wa kukutana na mtu huyu aliyekuwa msimamo wake unashughulikia mawazo yetu".
Mahojiano kati ya Al-Masry na Sadat yalifanyika baada ya hayo katika moja ya kliniki za kibinafsi za daktari, na kutoka hapa ulikuwa mwanzo halisi na mawazo mazito kuhusu mapinduzi dhidi ya Ufalme, kulingana na Sadat, anayesema: "Nilipoondoka kutoka kwake, Ujumbe wetu ulikuwa umefafanuliwa kuwa lengo la mbali tunaloweza kuona kwa macho yetu wenyewe, hata kama hatunge, tutagundua njia yake".
Al-Masry mwenyewe anasimulia undani wa tukio hilo kama ilivyonukuliwa katika kitabu "Abu Al-Tha’erin Aziz Al-Masry", akisema: "Mwanzo wa kukutana na Gamal Abdel Nasser ulikuwa wa kusisimua na wa ajabu, utu wake wa mapigano kupitia hali ya kuchekesha iliyosababisha mshangao na vicheko kwa wakati mmoja. Jioni moja nilikuwa nimekaa chumbani, chumba changu katika nyumba yangu huko Ezbet El Nakhl katika eneo la Ain Shams, na mjakazi wangu, Zainab Khairallah, alikuja niligonga mlango kimya kimya na aliomba ruhusa ya kuingia, na akaniambia kuwa kulikuwa na kundi la vijana waliovaa kiraia waliotaka kunilaki na kuketi nami".
Luteni Jenerali anaendelea kusimulia undani wa tukio hilo: "Jioni hii nilikuwa nilichoka, na hivyo uamuzi wangu ulikuwa ni kukaa peke yangu na kutokutana na wageni wowote, isipokuwa ni polisi, na wakapewa amri ya kunikamata na kunikamta, nipelekwe gerezani kuchunguza chochote. Basi nikamwambia Zainabu na anasubiri jibu kutoka kwangu ili akutane nao: Nimechoka, nilitamani unaomba msamaha mara moja kwa kuugua, akatoka na kufunga mlango nyuma yake, na baada ya dakika moja au zaidi, nilisikia sauti kubwa, sauti tulivu ya Zainabu ilikuwa ya nguvu na ya kunguruma, ikiwataka wageni waondoke na waje wakati mwingine, kwa sababu hali yangu ya kiafya haikuwa nzuri".
Jambo Halikuishia kiwango hicho.
Al-Masry anasema: "Kulikuwa kimya kwa muda, kisha nikasikia sauti yake kubwa ikimwita mpishi kuleta fimbo kubwa (shoma), na kelele zikaongezeka kwenye ukumbi wa nyumba, na miguu mingi ilikuwa ikitembea na kugongana, nikiwa na sakafu ya ukumbi, hivyo nilitoka nje kwenda kuchunguza suala hilo, na nilipofungua mlango wa chumba changu, nilipiga hatua chache kuingia ndani ya ukumbi". Nilimkuta Zainabu akiwa ameshika fimbo na kuelekea kwa kijana mrefu, mwenye ngozi nyeusi. mtu akiwa na nia ya kumshambulia kwa nguvu mbele ya mgongo na begani. Nikamuuliza kwa mshangao maelezo ya kile nilichokiona mbele yangu. Yule kijana akapiga hatua mbele, kisha akapiga hatua nyingine, aibu ikaonekana wazi usoni mwake, huku akisema: "Tunasikitika kwa kilichotokea, sisi ni watoto wako, Pasha. Sisi ni wanafunzi wako, Luteni Jenerali, tunasikitika kwa yaliyotokea tena, tunajua historia yako na misimamo yako. Tulikuja kuketi na nyinyi badala yake tunatamani kuketi nanyi, sisi ni maafisa wa jeshi. Anwar El-Sadat alitakiwa atutangulie kwenu ili apate taarifa za ujio wetu. Lakini kwa bahati mbaya hatukumpata hapa ili kumtambulisha nasi kwako... nami nina hakika kuwa yuko njiani kuja kwetu sasa hivi".
Japokuwa mwanaume huyo alikuwa alichoka na hakutaka kukutana na mtu muda mchache uliopita, alipuuza kila kitu alipowaona vijana hao. Hivi ndivyo alivyoeleza jambo hilo kwa kusema: "Mbele ya maneno haya, nilipoteza kisingizio chochote cha kuomba msamaha na kutoketi nao, na nilisahau uchovu wangu wote, na wasiwasi wangu wote ulipungua ndani yangu, na nilihisi kuburudishwa.... Nilihisi uhai ukinitiririka mwili mzima, nikasahau kila kitu huku nikiwakaribisha kuketi. Niliwaonea huruma kwa kutoelewana, na nilicheka kutoka ndani ya moyo wangu, kwa sababu Zainabu alikuwa mzito na mwenye maamuzi katika alichukua uamuzi wa kumpiga yule kijana mrefu na mweusi ambaye macho yake yalikuwa yalimeta kuashiria akili na Ufahamu, na kijana huyu mweusi hakuwa mwingine ila Gamal Abdel Nasser, na sikumbuki majina mengine isipokuwa Abd el-Hakim Amer na Gamal Salem, na labda Hassan Ibrahim.
Al-Masry alihisi furaha baada ya kukutana na maofisa hao, kama athibitishavyo, akisema katika kitabu "Abu Al-Thareen, Aziz Al-Masry": "Kuketi pamoja nao kulinipa hisia ya uchangamfu wa kihisia moyo, faraja ya kiakili, na utulivu wa kibinafsi pamoja na upendo. Nilihisi mapinduzi yangu yakichanganyika ndani ya mapinduzi yao, na nilikuwa na hakika kuwa badiliko bila shaka lingekuja mradi tu yangekuwa mbele yangu wanaume kama hao".
"Sikutaka kuwanyang'anya uongozi, na siku baada ya hapo ilithibitisha busara ya uamuzi wangu, wakati Muhammad Naguib alikuja kuongoza mapinduzi mwanzoni mwake kama mtu wa ngazi ya juu, na jinsi mzozo ulitokea uliosababisha kumzuia kufanya kazi yake ya Urais wa Jamhuri, kisha kufukuzwa kwake na kuamulia Ukazi wake" Aziz Al-Masry aliyewasaidia maafisa huru kwa Uzoefu na Ushauri wake.”
Baada ya mkutano huu wa kwanza, mwingine alikuja na Abdel Nasser. "Anwar El-Sadat, Abdel Moneim Abdel Raouf, na mimi tulikuwa tukimsubiri, na nakumbuka kuwa mazungumzo yalidumu kwa takriban masaa 3, na alikuwa mzungumzaji pekee katika kikao hiki". Kwa mujibu wa Al-Masry, aliyesimulia kuhusu mkutano huo, akisema: "Niliona baada ya hapo katika mazungumzo yao kuwa walirudia neno mapinduzi zaidi ya mapinduzi. Nilikuwa nikiwaambia kuwa mapinduzi hayo yanaweza kufuatwa na mengine, kama yalivyokuwa yakitokea Syria wakati huo, nikawaomba wainue kauli mbiu ya mapinduzi, kwa sababu mapinduzi ni nguvu zaidi na ya kina zaidi, na wakati watu wa Misri wanaunga mkono mapinduzi ya jeshi, kwao ni mapinduzi kutoka ndani, kwa sababu wanakataa mfalme, vyama, na Ukoloni, na anataka mabadiliko ya kina".
Hatua muhimu zaidi baada ya mikutano hii ilikuwa kuchagua kiongozi kwa ajili ya kundi la maafisa. Kutokana na kile walichokiona na walichokijua kuhusu Al-Masry, walimtaka awe kiongozi, lakini alikataa, na akaridhika na kuwa “baba yao wa kiroho.”
Abdel Majeed anasema katika kitabu chake "Abu Al-Tha'reen, Aziz Al-Masry": "Baada ya hapo, kulikuwa na mkutano wa maamuzi katika nyumba ya Aziz Al-Masry, ambao mashujaa wake walikuwa Gamal Abdel Nasser, Anwar Sadat, Salah Salem, na Abdel Hakim Amer Gamal aliianzisha kwa kusema: 'Unajua mengi kuhusu sisi, na unajua mambo yetu ya kufurahisha na mipango yetu yote kuwa kusimama katika ngazi ya Al-Bakbashi, na wachache sana kushika cheo cha Kaim Makam, hivyo tuliamua kuwa na mwandamizi, na kuwa na kiongozi anaye kadri yake, thamani yake, Umuhimu, na historia inayojulikana ili watu ridhika naye, hivyo tumeamua kukuchagua kuwa kiongozi wa mapinduzi yetu'".
Al-Masry aliyekuwa wakati huo na umri wa karibu miaka 70, alishangaa na kujibu akisema: "Sitaki uongozi huu kuutoroka, lakini nasitasita kuuongoza na kuukataa, labda kwa sababu mimi sio mtu sahihi, au sifai kwa kazi hii. Tafuta mtu mwingine, lakini ikiwa ungependa niwe mtu wa maoni na ushauri, au msaidizi katika kufanya Uamuzi wowote, ninakaribisha hii na nina furaha fanya kazi hii kama baba yako wa kiroho".
Al-Masry anasisitiza kuwa hajutii kukataa huku kwa kinamna, akihalalisha hilo kwa kusema: "Sikutaka kuwanyang’anya Uongozi, na siku baada ya hapo ilithibitisha hekima ya Uamuzi wangu, wakati Muhammad Naguib alipokuja kuongoza mapinduzi mwanzoni kama mtu wa ngazi ya juu. Halafu mzozo ulitokeaje uliopelekea Kumzuia asifanye kazi yake ya Urais wa Jamhuri, kisha kumfukuza na kuamua makazi yake, na mimi sikutaka niwe katika hali yake".
Baada ya Mapinduzi ya 23, mwezi wa Julai, mwaka wa 1952 yalifanikiwa, na Abdel Nasser aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu, alikutana na Zainab, mjakazi wa Al-Masry, tena. Rais Nasser anasimulia kilichotokea katika mkutano huo kwa kusema: "Nakumbuka kuwa alimwambia Zainab katika moja ya ziara zake baada ya mapinduzi alipokuwa bado waziri mkuu: 'Nashangaa, Bibi Zainab, ni nini kingesemwa na kurekodiwa katika historia lau kweli ungenipiga na fimbo? Wangesema: Zainab alimpiga mtumwa Al-Nasser kwa fimbo katika nyumba ya Aziz Al-Masry'. Siku hiyo tulicheka mpaka mishipa ikatutoka. Miongoni mwao waliokuwepo Muhammad Naguib, Anwar Sadat, Abdel Hakim Amer, na Salah Salem".
Kwa shukrani kwa wema wake na Ubaba wake wa kiroho kwake, mapinduzi yalimchagua Luteni Jenerali (Aziz Al-Masry) kuwa balozi wake wa kwanza katika Umoja wa Kisovieti kufanya kazi ya kulipatia tena silaha jeshi la Misri.
Katika mwaka wa 1960, Rais Gamal Abdel Nasser alimtunuku nishani ya Nili kwa kutambua huduma zake kubwa na historia yake tajiri ya uzalendo na kupigania kwa ajili nchi.
Licha ya Umri wake mkubwa, aliendelea kufuata mambo ya nchi hadi kifo chake tarehe 15, mwezi wa Juni, mwaka wa 1965.
Vyanzo:
Kitabu cha "Aziz Al-Masry Pasha", Fouad Nashi
Kitabu cha "Abu Al-Tha'reen Aziz Al-Masry", Muhammad Abdel Hamid
Kitabu cha "Siri ya mapinduzi ya Misiri" Muhammad Anwar Sadat
Tovuti ya Mamlaka Kuu ya Habari
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy