Hiyo Ni Njia ya Uhuru, Twende Pamoja Ndani Yake
Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled Eid
Ndugu mpendwa Mhe: Rais Houari Boumédiène ..
Eeh Ndugu na Marafiki :
Ninaposikia salamu yenu kwake pamoja na mamilioni ya watu wa nchi yetu , na hisia zenu wazi za kuelezea uaminifu wake , na kila Mmoja kwetu hana cha kufanya _na moyo yake unaojaa ushikamanifu na tathmini _ isipokuwa kujua vizuri historia hii kubwa ambapo matukio yake yaliwaunganisha watu wa Jamuhuri ya Muungano wa Kiarabu na watu wa Algeria, pamoja na kuonesha mahusiano yao yenye undugu halisi , kama kuwa damu zinazo mishipani mwa mamilioni niliowakutana huko Port Said mpaka Aswan , ni zile zile zinazo mishipani mwa ndugu zao huko Algeria ; kutoka vilele vya milima huko Aurès hadi Mabonde ya Wahran.
Siku hizo, ambazo umekaa pamoja nasi zilipitia, na aghlabu ya siku hizo ulizitumia ziara zake ulipojaribu kuwakutana na raia hawa, walipokuwa katika kazi zao ili kuhakikisha ujenzi uliovutia amali na maslahi yao , kiasi kwamba waliona kuwa ujenzi huo ni njia bora ya kuhakikisha maendeleo makuu ya pamoja , na tukiweza kutumia baadhi ya muda wako ili kuonesha mazungumzo yako nasi , ingawa hilo mimi nahisi kuwa mikutano yako na watu hawa ilikuwa ushahidi kwa mazungumzo hayo ; kwa sababu ndani ya maisha ya kweli na maisha ya kikazi watu waliweka mipaka kwa urahisi njia tuliyokwenda mbele, na sina shaka yoyote kuwa njia iliyochaguliwa na watu wa Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu ni njia ile ile iliyochaguliwa na watu wa Algeria.
Na hii ni njia ya uhuru ; Twende pamoja ndani yake kwa utashi na azimia na tumejua kuwa njia hiyo ni njia ndefu, na hayo yote kwa sababu uhuru unawakilishwa na upande wa uhuru wa kisiasa, uhuru wa kijamii, na katika kipindi cha kabla ya mapinduzi watu wetu walikuwa na matumaini ya kuondolewa kwa ukoloni wa Uingereza pamoja na nchi zinazouunga mkono ukoloni huo.
Na mapinduzi yaliyofanyika mnamo tarehe 23, mwezi wa Julai, mwaka wa 1952 , pamoja na kumalizisha kipindi cha ukoloni wa Uingereza na mamlaka zake za kifalme na kutangazwa kwa sera ya serikali ya jamuhuri na raia wa Misri waliweza kumiliki tena Mfereji wa Suez mikononi mwa ubepari wa kimataifa , pamoja na kulishinda shambulio la pande tatu mwaka wa 1956 , na haya yote yalikuwa mwanzo wa njia tu , njia ya uhuru.. uhuru wa kijamii, na hatua zilisonga mbele, na hatua yoyote tunaichukuwa inatulazimisha kufanya mengi zaidi ya tuliyofanya, kiasi kwamba maana za uhuru ziliongezeka sana katika akili za watu hawa , uhuru umebadilika sio mgogoro dhidi ya ukoloni ndani ya taifa dogo , lakini sasa ni mgogoro dhidi ya ukoloni ndani ya ulimwengu mkubwa, ambapo hakuna watu wowote wanaweza kuishi kiusalama pamoja na upatikanaji wa nguvu mkubwa inayopanga kila siku ili kupanua utawala wake , na uhuru sasa haumaanishi uhuru wa watu tu lakini ni uhuru wa mtu binafsi ndani ya wigo la watu hawa , na kuondoa chochote kinachomsukuma nyuma , kama vile utumiaji mbaya , ukabaila ubepari, na uhuru umebadilika kuwa ujamaa , kutosheleza na uadilifu
Ndugu mpendwa:
Ukoloni haujakuwa kama zamani , lakini umekuwa na njia mbalimbali za kujificha nyuma zake , unajificha nyuma ya ujinga ambapo ni chanzo kikuu cha ukoloni , na pia unajificha nyuma ya uyahudi ulioshambulia utawala wa Palastina na kuzitishia nchi zote za kiarabu, na kujificha nyuma ya ubaguzi uliopenyeza ndani ya Rhodesia na Afrika kusini kutishia ulimwengu huru wa kiafrika, na pia midororo ya kiuchumi , kudhibiti masoko ya kimataifa, maendeleo makubwa ya kisayansi, yanayosababisha tofauti kubwa kati yake na nchi zingine, na kuzifanya kama mhitaji wa maendeleo hayo , na migogoro hiyo yote inatoa mbinu mpya zinazoelewekwa na watu wetu wanaoenda mbele njiani mwao na kubeba mizigo yake.
Ndugu yangu nilikuambia kuwa ziara yako ilikuja kwetu katika wakati mzuri zaidi, kwa hiyo nasema kwamba mazungumzo yetu yalihakikisha jambo linalolengwa ; kwa maana kuwa mazungumzo haya hayajachukuwa muda mrefu ili kufahamiana na kuwa na mawazo yanayofanana, kwani tuna mawazo hayo hayo ili kuhakikisha lengo letu kuu , lakini kutafuta mipango ijayo lilikuwa jambo la muhimu zaidi, na hakuna shaka ya kuwepo changamoto mpya zinazokwamisha maendeleo yetu , ushirikiano wa ukoloni na kupinga maendeleo haukubali kuwa kimya mbele ya ongezeko la ujamaa katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu na katika Algeria, na maeneo mengine kwenye Ulimwengu wa Kiarabu , na sisi pia hatutakubali kuwa kimya dhidi ya matendo ya ushirikiano huo wa ukoloni na kupinga maendeleo.
Eeh Ndugu na rafiki yangu mpendwa!
Mkirudi kesho kwa watu wa ndugu wa Algeria, nawapelekea hisia zote za upendo na undugu, na pia kwa niaba ya wamisri , hawa ndio wanaowafikiri kuwa ndugu wa kupambana, na mfano wa kuigwa katika mapambano, ujasiri na kutoa mhanga, hadi inakuwa ngumu kuwalinganisha na wengine, pamoja na uwezekano uliotayarishwa na mazingira.
Na hebu sisi tutoe salamu yetu kwa rafiki na ndugu mpendwa Mhe Rais Houari Boumédiène .. na ujumbe wake mzuri zaidi waliomfuatia , na pia kwa mahusiano ya kipekee kati ya Mapinduzi ya kimisri na Mapinduzi ya Algeria , kwa ajili ya jukumu lake lililo muhimu mno katika historia ya kibinadamu.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy