" Hapana Upendeleo wala Mgawanyiko, pia hapana Chuki "
Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
Enyi Wananchi:
Kwa moyo huu wa hali ya juu, na kwa Umoja wa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, - Mwenyezi Mungu akipenda na kwa msaada wake kwetu- tutaweza kuendeleza nchi yetu na kufanya kazi ili kufikia jamii ya Ujamaa ya Demokrasia ya pamoja, inayoelezea matumaini ya raia hawa kwa maisha huru na mazuri, yanayotegemea usawa na fursa sawa. Na Umoja niliogusa leo ndani ya mioyo ya raia hawa; unaonesha tumaini kubwa kwamba tutashinda - kwa uweza wa Mwenyezi Mungu - katika kufikia lengo hili, hapana upendeleo, mgawanyiko, wala chuki, bali taifa ambalo limeweka nia yake ya kufuata njia yake ili kuunda jamii ambayo ustawi unapepea. , jamii inayounganishwa na upendo na udugu, jamii inayojengwa kwa ushirikiano wa kweli; ambapo kila mtu ni tegemeo la ndugu yake, na kila mtu ni ngao ya ulinzi kwa ndugu yake, na kila mmoja wa raia wa jamhuri hii anahisi kuwa jamhuri hii ni yake yeye na watoto wake baada kifo chake , na si miliki tu kwa watu wachache. ; Kwa sababu jamhuri hii imeshaondoa ukoloni, kisha ikaondoa utumiaji vibaya kwa maana zake zote na kwa aina zake zote; Iwe ni unyonyaji wa kisiasa, kijamii au kiuchumi, iliendelea njia yake ili kufidia kile kilichopotea, kujenga ili kukuza nguvu zake kisha kuongeza uzalishaji wake, kisha kuunda kwa kila raia wake,maisha yenye uhuru na utulivu .
Hiyo ndiyo jamii yetu tunayoishi , na siyo Jamhuri hii kwa kanuni hizi mlizozitangaza nasi pia tulizitangaza na mlizipandisheni kauli mbiu zake bali ni Jamhuri inayotegemea usawa na haki ya kijamii; Kanuni ambazo tulitangaza zilikuwa za kukomesha ukabaila, kukomesha udhabiti wa tajiri kwa utawala , kutekeleza haki ya kijamii, jeshi imara la taifa, na demokrasia ya kweli na yenye msimamo. Hilo enyi ndugu, lilikuwa onesho kwa kile ambacho kilichomo rohoni mwa kila mtu mmoja-mmoja wa Jamhuri, kutoka kusini hadi kaskazini.
Sisi sasa hivi - Enyi wananchi wenzetu - tunatekeleza hili , ambapo tunafanya kazi ya kuanzisha demokrasia imara.. maisha mazuri ya kidemokrasia, basi ni demokrasia ya raia na siyo demokrasia ya bandia ambayo ukoloni ulituletea huko kipindi kilichopita ili kuwatenganisha watu wa nchi yetu na kuwageuza kuwa madhehebu na vyama; kwa lengo la Wapingane, watengeishane na wasikubaliane, kisha wapiganie utawala, ufahari, mamlaka na utajiri.Hii si demokrasia tunayoiona, au ambayo kila mmoja miongoni mwenu anaihisi moyoni mwake .
Kila mmoja wa raia wa Jamhuri hii anataka maisha kweli ya kidemokrasia yanayomwondolea unyonyaji wa kisiasa na kijamii, na wakati tulipokomesha uchama na tulipoondoa mgawanyiko na chuki, na tulipoondoa mbinu za unyonyaji kwa namna zake zote; huo - Enyi ndugu-, ndio ulikuwa mwanzo wa demokrasia kweli .
Leo - Enyi wananchi wenzetu - tuko njiani ili kujenga kwa ajili yetu, taifa letu, na Jamhuri yetu ya kidemokrasia ambayo inakidhi mahitaji na malengo yetu , demokrasia sahihi inayotegemea upendo , ushirikiano na mshikamano , inayotegemea demokrasia ya kisiasa , kidemokrasia ya kijamii , inayotegemea kiwa raia wanaazimia kujiunganisha na kushikamana; wakajiunganisha basi wamekuwa pamoja na wakatembea katika njia ya nguvu ili kuiendeleza na kuijenga nchi yake, na akaiendea njia ya utaifa ili kuipandisha bendera yake na kuinyanyua, na akatembea katika njia ya umoja kwa ajili ya ulimwengu wa Kiarabu upate usalama. , na ili kulinda nchi zote za Kiarabu , na wakatembea kwenye njia ya mshikamano. Hii - enyi ndugu - ni njia ambayo sisi tumeitembea.
Leo, baada ya miaka miwili ya Umoja, ambayo ni kielelezo cha Mapinduzi Makuu ya kiarabu, tunahisi kwamba tumemaliza hatua kubwa, na sehemu ngumu zaidi njiani , ambayo ni sehemu ya kwanza ya njia hii. Leo, baada ya kuachana na uchama, migawanyiko na chuki, na baada ya kuhisi kuwa nchi hii ni kwetu sote, na baada ya kuamini kwamba lazima tujenge jamii ya kidemokrasia, ya ushirikiano na ya ujamaa isiyo na unyonyaji wa kisiasa, kijamii na kiuchumi. ; Njia ya mustakabali siyo njia rahisi, lakini pia - kwa azimio hili ambalo niliona kwenu katika kila nchi niliyotembelea - siyo njia ngumu.
Sisi - kwa msaada wa Mwenyezi Mungu - licha ya njama hizo na licha ya vitisho vya wafuasi wa ukoloni na ukoloni binafsi , tutaendelea kuijenga nchi yetu kulingana na matakwa yetu na kwa utashi wetu, na kujenga jamii yetu ili iwe jamii ambayo ustawi unaipepea , jamii inayo uhuru, haki na usawa, na nilisema hapo zamani: Mbwa wanapiga kelele karibu nasi lakini msafara unaendelea Na nimeona -Enyi ndugu - kwamba msafara unatembea katika kila sehemu za Jamhuri ili kufikia malengo makuu mliyokubaliana nayo, nasi tutaendelea na njia yetu huku tukimtegemea Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atufanikishe.
Waasalam Alaikum warahmat Allah.
__________________
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika jumba la wageni mjini Aleppo
Kwa tarehe ya Februari 17, 1960.