Gamal Abdel Nasser na Mapinduzi ya Afrika Kusini

Gamal Abdel Nasser na Mapinduzi ya Afrika Kusini
Siku kama ya leo mwaka 1994 Nelson Mandela alikula kiapo kama raisi mweusi wa kwanaza wa nchi ya Afrika kusini, baada ya nchi yake kupata uhuru wake kutoka Apart-heid aliekataliwa na baba wa waafrika kiongozi Hayati Jamal Abd-Elanser aliyezungumzia kuhusu Apart-heid “haukuwa ubaguzi wa rangi kati ya watu isipokuwa ni utangulizi wa ubaguzi katika haki kati wao”. Na kutokana na jambo hili Misri ilikatisha mahusiano yake na serikali ya ubaguzi ya Afrika kusini mwaka 61.Na pia Misri ilishirikiana na nchi 28 zingine kwa kupeleka mashtaka ya Apart-heid ndani ya baraza la usalama kwa mara ya kwanza mwaka 62, ikizingatia siasa ya ubaguzi ni siasa inayotishia amani na usalama wa kimataifa. Pia Misri ilikataa Bantostanas “ Mipaka ya kiubaguzi iliowekwa na watu weupe ili kuainisha makazi ya wakazi wa waafrika ndani ya maeneo yao ya kikabila na waliyaita Banto na wanawazuia kuingia maeneo ya weupe). Na pia palikuwa mawasiliano ya Misri na raia wa Afrika kusini kupitia vipindi vya idhaa elekezi (regional radio) ima kwa lugha ya kiengereza au kizulu.
Na kuna suala muhimu tunaliashiria hapa, nalo ni mkutano wa kitaifa wa kiafrika uliisaidia Misri kwa nguvu kipindi cha uvamizi wa nchi tatu juu ya Misri, na baada ya uvamizi huo Raisi Jamal Abd-Elnaser alianza kuzisaidia harakati za uhuru wa kitaifa
( ambazo miongoni mwao ni mkutano wa kitaifa wa kiafrika na mkutano wa umoja wa kiafrika) dhidi ya ubaguzi.
Mwenyezi Mungu Azirehemu roho zilizoondoka miili yake na zikabaki alama zake zikiwa ni shahidi juu ya athari yake.