Sambamba na maadhimisho ya Misri kwa Siku ya Diplomasia.... Wahitimu wa Udhamini wa Nasser wazindua jukwaa la kwanza la majadiliano kwa vijana waarabu
Imefasiriwa na / Aya Nabil
Mpalestina na Myemeni waunganisha vijana wa ulimwengu wa Kiarabu nchini Misri.. Sambamba na kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Sambamba na shughuli za mwaka wa Vijana waarabu 2023... Vijana wa Harakati ya Nasser wazindua jukwaa la mazungumzo la kiarabu

Kikundi cha wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kutoka mataifa mbalimbali ya Kiarabu, ikiwa ni pamoja na Yemen, Algeria na Palestina, ambao ni wanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, walizindua "Klabu ya Vijana wa Kiarabu" kama jukwaa la kwanza la majadiliano kwa vijana waarabu kutoka wana wa jamii za Kiarabu, na wageni nchini Misri, katika Kituo cha Ubunifu wa Vijana na kujifunza huko Al-Jazeera, pamoja na uangalifu wa Baraza la Mawaziri wa Vijana na Michezo wa Kiarabu, Kwa msaada na udhibiti wa Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri miongoni mwa shughuli za Mwaka wa Vijana wa Kiarabu 2023,na Kufuatia mapendekezo ya Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi wakati wa mikutano yake na viongozi wa Kiarabu pembezoni mwa Mikutano ya kikao cha 45 cha Baraza la Mawaziri wa Vijana na Michezo wa Kiarabu huko Kairo, kinachoongozwa na Dkt, Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri.

Katika muktadha unaohusika, jukumu la kusimamia la “Klabu ya Vijana Waarabu” lilikabidhiwa kwa Balozi Muhammad Al-Orabi, Waziri wa zamani sana wa Mambo ya Nje, ambaye kwa upande wake aliashiria kwamba vizazi wa sasa wa Vijana wana changamoto ambazo hatujawahi nazo katika historia yote , akisisitiza umuhimu wa kusaidia na kuwawezesha vijana na kuzingatia masuala yao, haswa suala la ufahamu, utambulisho na utaifa.

Mwanaharakati kijana wa Yemen, Muhammad Al-Jabri, mwanachama mwanzilishi wa Klabu ya Vijana wa Kiarabu, aliashiria kuwa shughuli za Klabu ya Vijana wa Kiarabu zitafanyika kila mwezi katika Mwaka wa Vijana wa Kiarabu 2023,kwa lengo la kuwekeza katika uwezo wa vijana waarabu na kusikiliza mawazo, mahitaji na matarajio yao, na kujenga madaraja ya mawasiliano na mazungumzo baina ya vijana wa nchi za Kiarabu; kuimarisha mafungamano ya mahusiano na kubadilishana uzoefu, tamaduni, mawazo na utaalamu kati yao.

Kwa upande wake mwanaharakati wa Palestina Rami Aman, mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na mwanachama mwanzilishi wa Klabu ya Vijana wa Kiarabu, alieleza kuwa wazo la kuanzisha klabu hiyo linakuja kutekeleza mapendekezo ya Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi na tangazo lake la 2023 kama Mwaka wa Vijana wa Kiarabu, ili kuunda kada za vijana wa Kiarabu katika nyanja kadhaa kama vile uchumi, utalii, kujenga uwezo, elimu, diplomasia ya vijana na vyombo vya habari, ili kufaidika na uzoefu wa kimisri katika nyanja hizo na kujenga jukwaa linalojumuisha watu wote wa kada muhimu zaidi za Kiarabu kwenye meza moja ya mazungumzo.

Hassan Ghazali, Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana alisema: “Tunashughulikia mbegu za vijana na miradi ya maendeleo tunataka kuwa endelevu kwa kutegemea haki ya kuchagua tunayofuata wakati wa mchakato wa kuchagua viongozi wa vijana wanaoshiriki katika programu zetu mbalimbali. ," akiashiria kwamba imani yake kubwa kwenye uwezo wa kada za vijana walioanzisha Klabu ya Vijana wa Kiarabu. Akisisitiza kwamba aliwawasiliana nao karibu kupitia Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na akawakuta watu wenye ufahamu,na ujumbe wa kweli wa kibinadamu, na asili mbalimbali za kiutamaduni.

Hivyo, na Shughuli za uzinduzi huo zilifanyika kwa mahudhurio ya Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri, Dkt. Ashraf Sobhy, na kundi la wanadiplomasia wa Kiarabu na viongozi vijana wa Kiarabu.