Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa atangaza sherehe ya Ubalozi wa kimisri huko Sudan wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Mapinduzi matukufu ya Julai
Ubalozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Khartoum, Sudan, ulisherehekea kumbukumbu ya miaka 70 ya Mapinduzi matukufu ya Julai 23, kwa ushiriki na utangazaji wa mtangazaji wa Sudan "Reem Al-Mamoun", mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na mwanachama wa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana, na hivyo kwa mahudhurio ya mgeni rasmi na mwakilishi wa Baraza Kuu la Sudan, Waziri wa Madini "Mohamed Bashir Abu Namou", na kundi la maafisa wa Sudan wakiongozwa na mawaziri walioteuliwa, akiwemo Gavana wa Darfur, Gavana wa Khartoum na Gavana wa Benki Kuu, pamoja na wakuu wa vyama vyote vya Sudan, maafisa wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na mabalozi walioidhinishwa nchini Sudan, wanachama wa uwanja wa kidiplomasia, na wakurugenzi wa ofisi za UN na wakurugenzi ya mashirika ya kimataifa na ya kikanda, na wasimamizi wa matawi ya makampuni makubwa ya Misri yanayofanya kazi nchini Sudan, pamoja na wakuu wa jamii ya Misri huko Sudan.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Hossam Issa, Balozi wa Misri nchini Sudan, alitoa hotuba katika hafla hiyo, ambapo alielezea undani wa viunganishi vya kihistoria kati ya nchi hizo mbili, akiashiria kiunganishi wa milele kinachowakilishwa na Mto Nile, akipitia masuala muhimu zaidi ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, akisisitiza endelevu na kina ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili ndugu, na umuhimu wa kuendelea Kazi ya kuimarisha na kuboresha mahusiano hayo.
Katika muktadha huo, mgeni rasmi Mhandisi. Mohamed Bashir Abu Nammo, Waziri wa Madini alisisitiza kina na nguvu ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili, na akashukuru serikali na wananchi wa Misri kwa misimamo yao ya kuiunga mkono Sudan katika masuala ya kisiasa, kiuchumi , viwango vya maendeleo na kibinadamu.
Ikumbukwe kwamba, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulikuja kama moja ya njia za kiutekelezaji za kuwasilisha uzoefu wa Misri katika kujenga taasisi za kitaifa, kisha Toleo lake la pili lilijumuisha mabara matatu ya Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, pamoja na kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" na likapata Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi mnamo Juni 2021, kisha toleo lake la tatu likafanyika, Juni 2022, pamoja na Ufadhili wa Rais wa Jamhuri kwa mara ya pili mfululizo, ukiwa na kauli mbiu "Vijana wa Kutofungamana kwa upande wowote, ushirikiano wa Kusini - Kusini»