Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashiriki katika Kongamano la Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini
"Godfrey Juner Malongo", Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana,kama mwakilishi wa vijana kutoka eneo la Afrika Kusini na Malawi, alihudhuria mkutano wa kikanda wa Kongamano la Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika kusini unaojulikana kama "SADC",kuhusu ushiriki wa wanawake katika siasa na kuimarisha usawa wa kijinsia, mkutano huo ulijumuisha wajumbe wa Bunge, wawakilishi wa kamati za uchaguzi za nchi za Jumuiya ya maendeleo ya Afrika kusini, wanawake na sheria huko Afrika Kusini, Shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake, mashirika ya kiraia, na vijana.

Kwa upande wake “Godfrey” alieleza kwamba Kongamano hilo linazingatiwa fursa kwa vijana ; kushughulikia na kujadili masuala muhimu zaidi katika eneo hilo , haswa kuhusisna na ushiriki wa vijana katika siasa na maendeleo, haswa kuchunguza juhudi zinazofanywa kwa usawa wa kijinsia, ili kuharakisha uwezeshaji wa vijana kushiriki katika siasa na uongozi, akisisitiza kwamba Kongamano la Bunge limefanya maendeleo makubwa yamesababisha mifumo kadhaa ya kuhakikisha uwezeshaji wa vijana na kuwazingatia kwao kama sehemu muhimu ya vyombo vya kuunda maamuzi, michakato ya kisiasa na njia za maendeleo.
Katika muktadha unaoendelea, "Hassan Ghazali" Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana alisisitiza kuwa, Harakati hiyo inawasaidia vijana kwa kushiriki katika michakato ya kuunda maamuzi, iwe katika kiwango cha kitaifa ndani ya nchi zao, bara au hata kimataifa. akiashiria kwamba ni lazima kuunda nafasi ili kujali nguvu za vijana, kusikiliza mawazo na matarajio yao, na kuimarisha ushiriki wao na kutetea Haki na sauti zao katika makundi ya kuunda maamuzi katika viwango vyote na katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande mwingine, fursa ilipatikana kwa vijana kupitia Kongamano hilo ili kuchangia katika kuweka mikakati huko eneo,na kutoa hatua zitakazoharakisha ushiriki wa kisiasa wa vijana wa kike na usawa wa kijinsia katika eneo la Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini, na katika nchi zote za eneo hilo; ambapo wastani wa uwakilishi wa kisiasa wa wanawake katika eneo hauzidi 23.2% katika nafasi za uongozi na uchaguzi katika nchi zote za Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini, pamoja na ukosefu wa eneo kwa majukwaa ya maendeleo ya Uongozi yanayoweza kuongeza ushiriki wa vijana katika sera za siasa.
