Ghazali akutana na timu ya Tovuti rasmi ya Harakati ya Nasser kama sehemu ya maandalizi ya toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Jana jioni,Mwanaanthropolojia Hassan Ghazali, Mwanzilishi wa Harakati ya Naseer kwa Vijana, alikutana na vikundi na sehemu za timu ya Tovuti ya Nasser, inayojumuisha makada kadhaa wa wanafunzi na vijana kutoka nyanja na taaluma mbalimbali;kujadili changamoto muhimu, mipango, mapendekezo na maswali yanayoulizwa na vijana hao kama maandalizi ya maendeleo ya mfumo wa Tovuti na ufafanuzi wa mpango wake mpya mnamo kipindi kijacho kwa maandalizi ya kupokea Udhamini wa Nasser katika toleo lake la nne.
Tovuti rasmi ya Harakati ya Naseer kwa Vijana inatoa kwa wanafunzi na wasomi lugha fursa ya kufundisha kitaaluma kwa kutafsiri maudhui zake tofauti, inayotolewa katika lugha tano rasmi: Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kihispania, pia Tovuti hiyo iko na lango maalum la «Makala na Maoni» kama jukwaa jumuishi kwa vijana ili kutoa mawazo yao na kuchapisha michango yao ya kiakili, maandishi na uchambuzi kwa uhuru kamili katika lugha wanayoipenda.