Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa ni mhadhiri katika mpango wa uongozi wa kiuchumi kwa wanawake kwa ajili ya ukuaji endelevu

Bebom Jean-Francois Nicolas, mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, toleo la tatu, Mratibu wa kitaifa wa timu ya Mustakabali nchini Cameroon, na mwenyekiti ofisi ya kiutendaji kwa timu ya mustakabali Barani Afrika (Future Team in Africa), alishiriki kama mhadhiri katika mpango wa "Uongozi wa kiuchumi kwa wanawake kwa ukuaji endelevu", unaoandaliwa na taasisi ya Asongwe Asongwe (Asongwe's Virtues Home Foundation); kuwawezesha wanawake vijana hamsini wawe viongozi wa wanawake wa Afrika huko Jamhuri ya Cameroon.
Wakati wa mkutano wake, Nicolas alielezea Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, na uzoefu wake huko Misri wakati wa shughuli za Udhamini zilizoendelea kwa muda wa wiki mbili katika Mji mkuu wa Misri Kairo, pamoja na ziara yake kwa miji ya Aleskandaria na Ismailia.
Na mwishoni mwa mkutano huo, Beibom alipendekeza Misri kwa washiriki kama akiisifu kwa "Nchi ya Fursa" kama walitaka uzoefu mkubwa na washirika wanastahili.
Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri imekamilisha shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, mnamo kipindi kutoka Mei 31 hadi Juni 17 iliyopita, katika jumba la mamlaka ya uhandisi jijini Kairo.
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa Misri katika kuanzisha na kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kujenga kizazi cha viongozi vijana kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote wenye maoni yanayoendana na Ushirikiano wa Kusini- Kusini, kuongeza ufahamu wa jukumu la harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote ya kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la mtandao wa vijana wa nchi wanachama wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote (NAM), na kuunganisha viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi katika ngazi ya nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki.
Pamoja na kutoa nafasi sawa kwa jinsia zote mbili kama lengo la tano la malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 linavyoashiria, pia unawezesha vijana na kuwapa nafasi kwa watendaji kutoka nchi mbalimbali za Dunia kuchanganyikana na kufanya ushirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu Barani, bali kimataifa pia kama lengo la kumi na saba ya malengo ya Maendeleo Endelevu linavyoonesha.