Kumbukumbu ya miaka uhuru wa Jamhuri ya Watu wa Angola

Kumbukumbu ya miaka uhuru wa Jamhuri ya Watu wa Angola

Angola imeshapata uhuru  wake kutoka kwa Ureno mnamo Novemba 11, 1975. kuwepo kwa kwanza kwa Kireno nchini Angola kulianza mnamo 1448 kupitia ziara ya Mtafiti wa kwanza wa Ureno, na hatua kwa hatua Wareno walianza kuenea kufikia majimbo ya ndani ya Angola, na wakaanzisha makazi na vituo vya biashara kando ya pwani ya Angola mpaka walipoitawala nchi kabisa mnamo karne ya 20.

Watu wa Angola walianza kupambana na kupinga kuwepo kwa ukoloni tangu mwanzo wake, na aina za kupambana kwa ajili ya kupata uhuru ziliongezeka mnamo miaka ya hamsini ya karne ya ishirini. Lakini, wakati huo,utawala wa Ureno ulikataa kukubali hatua zozote za makoloni yake kuelekea uhuru, na ulifanya ukandamizaji wa harakati za uhuru huko Angola, iliyosababisha kuibuka kwa upinzani wa kijeshi na vita vya genge, na uzinduzi wa Harakati ya Watu ya Uhuru wa Angola (MPLA) mnamo 1961.

Baada ya mapinduzi mnamo 1974 huko Ureno, serikali ya Ureno ilipitisha hatima ya makoloni yake kwa kura ya maoni ya watu. Mnamo Januari 1975, vikundi vikuu vya ukombozi huko Angola viliunda serikali ya mpito, Harakati ya Watu ya Uhuru wa Angola (MPLA) ilifanikiwa kuutawala wa mji mkuu, Luanda, na ilitangaza uhuru wa Jamhuri ya Watu wa Angola mnamo Novemba 11, 1975.

Ikumbukwe kuwa mahusiano ya Misri na Angola yanajulikana kwa mshikamano na utulivu kupitia historia, ambapo Misri iliisaidia Angola katika mapambano yake ya kupata uhuru, na ofisi ya kwanza ya kikanda ya Chama cha Watu wa Ukombozi wa Angola (MPLA) ilifunguliwa mjini Kairo ikiongozwa na Bwana Paulo George, Waziri wa zamani sana wa Mambo ya nje, kwa ajili ya kuongeza msaada wa kimisri kwa harakati za ukombozi  za Angola dhidi ya ukoloni wa Ureno.