Siku ya Ujuzi wa Vijana Duniani

Siku ya Ujuzi wa Vijana Duniani

"Ushindi ni Mwenendo, Mwenendo huo ni Kazi, Kazi ni mawazo, mawazo ni kuelewa na imani, na hivyo kila kitu kinaanzia binadamu."

Kiongozi Gamal Abdel Nasser (1918 - 1970)

Mnamo  2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe ya Julai 15 iwe siku ya Ujuzi wa Vijana Duniani;  kusherehekea umuhimu wa mikakati ya kuandaa vijana kwa ujuzi unaohitajiwa; ili kuwaajiri na kuwawezesha kupata kazi nzuri, licha ya kuwawezesha kwa Ujasiriamali. 

Tangu wakati huo, Siku ya Ujuzi wa Vijana Duniani iliwapa fursa pekee kwa mawasiliano kati ya vijana na taasisi za elimu, uzoefu wa makanika na kifundi, makampuni, mashirika ya waajiri na wafanyakazi, watengeneza sera, na washirika wa maendeleo.