Kumbukumbu ya miaka 62 ya uhuru wa Niger
Mnamo siku kama hii, Agosti 3, 1960, kwa njia rasmi Niger ilipata uhuru kutoka kwa Ukoloni wa Ufaransa. Ufaransa ilianza majaribio yake ya kuvamia Niger mwishoni mwa 1980, na Wafaransa walikabiliwa na upinzani mkali na uasi kutoka kwa makabila nchini Niger , wakikataa vikali uvamizi huo, iliyosababisha kushindwa udhibiti wa Ufaransa kwa nchi hiyo kwa miaka kadhaa.
Mnamo 1922, Niger ikawa sehemu inayoitwa Afrika Magharibi ya Ufaransa. Na ifikapo 1946, Niger imeanza hatua kwa hatua kuelekea kujitawala, hadi Desemba 1958 ikawa inajitawala ndani ya jamii ya kifaransa, na Niger ilipata uhuru wake kamili mnamo Agosti 3, 1960.
Kati ya Misri na Niger kuna mahusiano ya kina, wakati ambapo Misri iliisaidia Niger katika mapambano yake na kuiunga mkono kwa uhuru wake , Rais wa kwanza wa Niger na kiongozi wake wa ukombozi, Hamani Diori, alikuwa rafiki wa karibu kwa kiongozi Gamal Abd El Nasser. Diori amefanya ziara ya kihistoria kwenda Misri baada ya uhuru wa nchi yake, wakati ambapo alielezea kiburi na furaha ya nchi yake kwa mahusiano ya zamani ya kihistoria pamoja na Misri, na hamu ya kuyarudisha tena baada ya kutengana Niger kwa miaka kadhaa mbali na watu wengine wa bara hilo kwa sababu ya Ukoloni wa Ufaransa, na wakati huo marais wawili wale walisisitiza uungaji mkono wao kwa nchi zote za kiafrika zinazopambana kwa ajili ya Uhuru.