Siku ya Vijana Duniani... Mshikamano wa Kizazi waunda ulimwengu kwa kila kizazi

Imetafsiriwa na:Fatma Ibrahim Saleh
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Mawaziri wa Dunia unaowajibika kwa Vijana, ulioandaliwa na Serikali ya Ureno kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, na uliofanyika katika mji mkuu wa Ureno Lisbon kutoka nane hadi kumi na mbili ya Agosti 1998, azimio lilipitishwa kutangaza Agosti 12 kama Siku ya Vijana ya Kimataifa, na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha pendekezo hilo mnamo tarehe Desemba 17, 1999, katika kikao chake cha hamsini na nne, katika azimio Na. (54/120) chini ya kichwa "Sera na mipango inayohusiana na vijana".
Maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kufikisha ujumbe kwamba kuna haja ya kufanya kazi katika vizazi vyote ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na kuepuka kuacha mtu nyuma. Tukio hilo pia lina lengo la kuongeza uelewa wa baadhi ya vikwazo vya mshikamano wa kizazi, hasa ubaguzi dhidi ya wazee, ambao kwa hivyo huathiri vijana na wazee, pamoja na athari mbaya kwa jamii kwa ujumla.
Kuzeeka ni suala tata na mara nyingi hupuuzwa katika afya, haki za binadamu na maendeleo, na pia kuathiri watu wazee na vijana duniani kote. Kwa kuongezea, upendeleo wa umri unaingiliana na aina zingine za chuki (kama vile ubaguzi wa rangi na ngono), ambayo huathiri watu kwa njia ambazo zinawazuia kutambua uwezo wao kamili na kutoa mchango kamili kwa jamii yao.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ubaguzi wa Umri, iliyotolewa mnamo Machi 2021, inaonesha kuwa vijana wanaendelea kuripoti vikwazo vinavyohusiana na umri katika maeneo mbalimbali ya maisha yao kama vile ajira, ushiriki wa kisiasa, afya na haki. Ripoti hiyo pia inabainisha mwingiliano wa kizazi kama moja ya mikakati mitatu muhimu ya kushughulikia upendeleo wa umri.
Shughuli za kizazi zinaweza pia kusababisha hisia kubwa ya mshikamano wa kijamii na kuimarisha mshikamano wa kizazi.
Mshikamano wa kizazi ni ufunguo wa maendeleo endelevu. Tunapokaribia mwaka wa tatu wa janga, ni muhimu sana kutambua na kushughulikia vizuizi hivi vinavyohusiana na umri ili kufikia "kujenga nyuma bora" kwa njia ambayo huongeza nguvu na maarifa ya vizazi vyote.
Siku ya Vijana Duniani ni fursa ya kuongeza juhudi katika nyanja ya kuelimisha vijana, kuwawezesha kushiriki, yenye ufumbuzi wa ujasiriamali wanaoutoa na kisha kufanya kazi ili kuyatekeleza.