Tunatoa Wito Kwa Wananchi Kuwa Kufikiri Na Ufahamu
Imetafsiriwa na/ Amira Mohamed
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Assalamu Alaikum warahmat Allah
watu wenye uhuru wa Jamaliya:
Kwanza napenda kutoa shukrani kwa Bw.Abdelaziz Khedr na Bw. Mohamed Ibrahim; kwa ujenzi walizozianza kwa Halamashauri ya Uhariri katika eneo hilo, na vilevile nawashukuru ndugu wengine kwa juhudi walizozifanya katika njia hii, na nazingatia kuweka jiwe la msingi leo kama ishara nzuri kwa Halamshauri ya Uhuru katika Al-Jamaliya.
Halamashauri ya Uhariri iliyoanzishwa baada ya mapinduzi linalenga kutakasa mioyo, kuwapatanisha hali za matajiri na maskini, na kushirikiana kati ya mwenye nguvu na dhaifu. Hii ni misingi ya awali ambayo Halamashauri ya Uhariri iliyoanzishwa, hatukuiunda kwa malengo ya kibinafsi au faida za kibinafsi, sote tunaenda, na haishi milele duniani na katika nchi hii isipokuwa matendo mema.
Na kuzungumzia malengo na faida kunisukuma nizungumzie hali ya jeshi kabla ya mapinduzi, ni kwa kiasi gani walijaribu kuiridhisha, ili jeshi haizingatii -ni chanzo cha nguvu- hali ya wananchi, jeshi imekuwa nguvu ambayo dhuluma inategemea, kwa hivyo, kila mara waliulizia maombi ya jeshi ni nini, matakwa ya jeshi ni nini, kwa sababu walihisi hisia za kina kuwa ikiwa jeshi itawaacha, watakuwa wenye udhaifu bila nguvu yoyote, kwa hivyo sisi katika jeshi walihisi ambacho kila mwananchi anahisi, na hali zetu za kibinafsi hazijawahi kutukengeusha kutoka kwa hali za wananchi wengine. Tuliona kwamba tuna wajibu na majukumu, na tumekataa kuridhika au kutembea na Shetani na tunaomba chochote tunachotaka na kila kitu tulichoomba kilijibiwa. Lakini tulikuwa na bado tumehisi kwamba nguvu ya nchi sio nguvu ya sehemu yake lakini ni nguvu ya wananchi wote, hali zetu za kibinafsi hazijawahi kutukengeusha -na hapa nakusudia uhalisia- kutoka kwa wananchi wote wanateseka, kila mara tunafikri hali inatuchukua wapi.
Na mojawapo ya njia mbili ilikuwa mbele yetu: kutembea pamoja na nguvu, kunafiki na kudanganya ili kufikia faida zote kwa watu wetu, au kutembea na Mungu na katika njia ya Mungu. Maafisa huru walichukua njia ya pili kwa sababu wanaiamini nchi na wananchi hawa walioweza kuondoa dhuluma na utumwa, kamwe hawafi na ni lazima wafufuliwa wenye nguvu, na wananchi hawa ni ndugu zetu, lazima tushirikiane nao na tunakesha kuwalinda. Kamwe hawakuwa kama mjeledi unaoumia migongo yao. bali tuwe kama nguvu inawaangazia njia ya kujenga nchi yenye huru, na furaha.
Tulichagua njia hii, tulielekea njia ya Mungu, Tunaomba msaada wake, tuliungana na tulishirikiana, na upendo ulikuwa kiongozi wetu, kwa hiyo hii ilikuwa njia ya ushindi. Naweza kukuambia kwa uwazi kwamba upepo wa uhuru ulipovuma na mapinduzi yalipofanikiwa, hatukujua kamwe kwamba tungekumbana na magumu haya, matatizo haya, na majukumu haya. Tulitoka nje katika usiku wa kwanza wa mapinduzi tukiwa na lengo moja na nia moja ambayo ni ukombozi, ni kufanya kazi kwa Misri, ni kuwakomboa raia wote kutoka kwa ukoloni na dhuluma, Wadhalimnawenyewe wamehisi nguvu ya jeshi, na kwamba ikiwa wananchi walipinga dhuluma, jeshi litawalinda, tukaamua kuunganisha jeshi na wwananchi, basi mapinduzi yalifanikiwa.
Ukandamizaji wao kwa watu haukuwa wa kiholela, bali ulikuwa ni mpango.. Muhamed Aly alianza utawala kwa jina la ukombozi kutoka kwa utawala wa Waturuki, lakini yeye mwenyewe aliifanya nchi hii kuwa mtumwa, hivyo akateka mali yote ya kilimo na kujimilikisha mwenyewe. kisha akaigawanya watumishi wake, wafuasi wake, familia yake na wasaidizi wake ili waweze kutawala kugawanya riziki pamoja naye, na wote waliokuwa na sera ya kudhibiti riziki ya mtu.
Wakati huo huo, miongoni mwetu kuna watu waliokuwa wakidai uhuru, na walikuwa wakiwapotosha watu kwa maneno mazuri na ahadi tamu, na wakachagua kuinua kiwango chao na kiwango cha familia zao, na kuondoka nchi ikipiga magoti katika unyonge na utumwa, sisi tulio yakini na upotofu wao na sisi tulioukubali udanganyifu wao. Na watarejea tena kwenye hadaa hii na udanganyifu huu, ikiwa hatutatambua, na ikiwa hatujui nini maana yetu, na kuzingatia kila tunaloambiwa, na sio kutoa amana yetu isipokuwa kwa wale, wanaostahili. Tukikengeuka kutoka katika haki, tunapata ndani yetu ujasiri wa kutosha ambao tunaweza kuondoa hili. Tumaini, suala si kama ibada ya sanamu, kwani ibada ya sanamu ilikuwa njia ya nchi hii kuanguka shimoni.
Ujumbe wa Bodi ya Wahariri uko hapa kukujulisha hili; Haijui kutia chumvi kuhusu majukumu yake, lakini inajua jinsi ya wananchi wote wanafanya kazi kwa vitendo, na kila mtu anayekosea atawajibika. Katika Bodi hiyo, tunafanya kazi kulingana na imani huria na wazo la pamoja.
Sambamba na hilo, tunatoa wito kwa wananchi kuwa na ufahamu na ufahamu, kwa sababu katika nchi hii wapo watu wataokutumikia kwa jina la uhuru, kwa jina la katiba, na kwa jina la kuinua kiwango cha uchumi, hivyo. usisikilize upotofu na udanganyifu huu. Walikupotosha huko wakati wa nyuma na watakupotosha siku za usoni. Wajibu wa ubinafsi hawatakaa kimya, bali watajaribu kukuhadaa ili ushirikiane na ukoloni. Lakini leo tuko katika mapinduzi ya kiuchumi na ya kijamii, na wakati huo huo ni mapinduzi ya ukombozi ambayo yaliibuka kupambana na ufisadi wa kisiasa na athari za kiuchumi, na yaliibuka kuikomboa nchi kutoka kwa utumwa wote. Mapinduzi ya ujenzi na ujenzi lazima yaishi. bega kwa bega na mapinduzi ya uhuru na ukombozi.
Nataka awe mkweli kwa mantiki mbali na mtindo wa hotuba na maneno mazuri ambayo huchochea shauku. Leo tuko kwenye shida kubwa katika nchi yetu, Nchi hii iliyo pendwa, waliopoteza na kuiacha kuwa magofu, na sisi. tumejenga upya ili nchi yetu ichukue nafasi inayostahili, nitakuwa mkweli kwako kwa kusema tusipojitegemea, hatuwezi kufanya jambo.
Nchi hii imekuwa na bado ni lengo la wakoloni kutokana na umuhimu wake wa kijiografia na wa kiuchumi. Tukiitazama historia tutaikuta imejaa ushahidi wa haya tunayoyasema. Na hapa tuko leo katika nchi inayokaliwa, na hii ndiyo kazi ambayo tunakabiliana nayo nyumbani na ambayo ilipata udhibiti wa ardhi yetu shukrani kwa ushirikiano na watoa maoni hapo awali. Mpango wetu ulikuwa ni kuwaondoa wasaliti hawa ili mkoloni asipate miongoni mwetu watu wanaoshirikiana naye, lakini mkoloni wakati huo huo anaikalia sehemu ya nchi yetu, anafanya kazi kwa kila namna ya kutudhoofisha. ... Vipi?
Misri ni nchi ya kilimo, huagiza ngano kwa kiasi pauni milioni arobaini kila mwaka, na siku moja tunaambiwa: Hamna ngano, waliweza kudhibiti maisha yetu, kwa hiyo ni lazima tujitegemee katika kujenga nchi yetu mpya.
Idadi ya Wamisri ni milioni 22, na mapato yao ya kitaifa ni pauni milioni 660, kwa hivyo inamaanisha kuwa mapato ya kila mtu kwa mwaka ni pauni 30 na pauni mbili na nusu kwa mwezi, na kila mwaka tunaongeza watu elfu 350, na baada ya miaka 50 tutakuwa milioni 44, na anga hainyeshi dhahabu au fedha, kwa hivyo ikiwa tunataka Ili kuinua kiwango chetu cha maisha, lazima tukumbuke ukweli huu: kiwango cha maisha kinapungua, idadi ya watu inaongezeka. na utajiri kama unavyojua unaongezeka.
Je, hali ikiendelea kama ilivyokuwa huko kama wakati wa nyuma, je, mustakabli ya watoto wetu itakuwaje? Bila shaka watakabili ugumu na uchovu, na hivyo tutakuwa watu wataoanguka shimoni. Ikiwa tunataka kuepuka uovu wa shimo hili, msingi lazima uwe na nguvu na imara, na hili haliwezi kufikiriwa kutoka kwa maoni ya mtu binafsi, bali lazima fikra yetu ya pamoja itakuwa msingi yetu ili kutatua tazizo hilo kubwa.
Tatizo hili kubwa haliwezi kutatuliwa, isipokuwa nchi yetu iwe ya kilimo na ya viwanda, lakini hatupati fedha iliyo kutosha kwa miradi yetu ya uzalishaji. Miradi hii inahitaji fedha za kigeni, lakini ukoloni – Eeh wananchi - inapigana na sisi huko. Itafanya kazi kwa njia zote ili kuzuia misaada yoyote inayokuja kwetu kutoka nje. Kwa sababu kila jiwe tutakaloweka katika kujenga viwanda litakuwa njia ya kutuimarisha, na kupitia hilo tutakuwa taifa hatari, na nchi yenye nguvu.
Msisubiri miradi yetu ipate misaada kutoka hapa na pale, na msiweke matumaini kwa Benki ya Dunia kujenga Bwawa la Juu, na msifikiri kwamba mtu yeyote atakuja kwetu na mkopo isipokuwa bei yake haijajulikana mapema. na isipokuwa wahakikishe angalau kuwa nchi yetu itakuwa soko la viwanda na bidhaa zake. Kila mtu anayetukopesha anafikiria kwanza katika masilahi yake ya kibinafsi , na maslahi hiyo haiendani hata kwa kidogo na maslahi ya Misri.
Ushauri wangu kwenu ni kwamba tukitaka tukutane na kujipatia sisi na watoto wetu maisha adhimu na yenye heshima, basi tushiriki sote kujenga, na wananchi wote wawe imara, ili tabaka la wasomi lisibembelezwe kwa gharama. ya wafanyakazi na wakulima. Nilikupa mfano wa sisi maafisa mwanzoni mwa hotuba yangu ili ujue kuwa fikra za mtu binafsi kuliangusha taifa shimoni.
Tuna ardhi ya kilimo iliyo kutosha ili kulima ngano, mpunga na pamba, na kila tunachotakia ni kazi ya kitaifa ya kujenga msingi, na tujitegemee kwa miaka mitano tu, ambayo ni muda wa ujenzi wa Bwawa la Juu, kwa hivyo nchi yako itakuwa nguvu, na raia wote watakuwa watu wanaopata uhuru wa kisiasa na uhuru wa kiuchumi kwa nchi zao.
Hatutakudanganya, wala hatutakulaumu.Bali kila wakati tutakukabili na ukweli, Ukweli ndio njia pekee ya kushinda vita...vita vya kumiliki mali, ama vita ya ukombozi tunafanyia kazi. kila wakati kupigana nayo kwa kila njia na uwezo.Hatua si kuingia vitani, bali ni kuibuka mshindi.
Waalsalamu Alaikum warahmat Allah.
Hotuba ya Mheshimiwa Gamal AbdelNasser, Naibu Mkuu, katika Bodi ya Uhariri katika Al-Jamaliya
Mnamo Februari 18, 1953
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy