Ziara ya Jiji la Utoaji wa Vyombo vya Habari

Wizara ya Vijana na Michezo iliandaa ziara ka Jiji la Utoaji wa Vyombo vya Habari kwa vijana wanaoshiriki matukio ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" miongoni mwa matukio ya siku ya pili ya Udhamini huo, ambapo wakati wa ziara hiyo vijana waafrika walikagua studio za Jiji la Utoaji wa Vyombo vya Habari, zikiwemo Al-Mehwar TV, Sada Al-Balad, CBC na chaneli za satelaiti, vyumba vingine vya udhibiti na studio zilizo na teknolojia zao na uwezo wa juu wa kiufundi uliounganishwa moja kwa moja kwenye satelaiti.

Pia, ziara hiyo ilijumuisha kutembelea vituo mbalimbali vya studio ambavyo kwa njia yake maonesho makubwa zaidi ya televisheni, tamthilia na sinema hufanywa, ikichukua muda mwingi wa matangazo ya televisheni kwenye chaneli mbalimbali za Waarabu za Misri, pamoja na kutembelea maeneo wazi ya upigaji picha yanayojumuisha vitongoji tofauti kama vile Fukwe, Jangwa, Mito, Miji na Mazingira mingi yanayofanana na miji mingi ya kimataifa.

Pia, ziara hiyo ilijumuisha kutembelea maeneo ya upigaji picha yanayojumuisha  eneo la Kiislamu, eneo la vijijini, eneo la kifarao, eneo la Alexandria, eneo la vitongoji maarufu, eneo la kiakiolojia, eneo la bedui na jangwa, eneo la pwani na eneo la burudani. Na ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutembelea kituo cha mafunzo cha jiji hilo, kinachotoa kozi za hivi punde kwa wanafunzi na wahitimu wa nyanja mbalimbali za utengenezaji, uhandisi na usimamizi wa vyombo vya habari.