Wizara ya kimisri kwa vijana na michezo, "inatangaza udhamini wa Gamal Abd El Nasser kwa Uongozi wa kiafrika. "

Wizara ya kimisri kwa vijana na michezo, "inatangaza udhamini wa Gamal Abd El Nasser kwa Uongozi wa kiafrika. "
منحة ناصر
Wizara ya kimisri kwa vijana na michezo ( Idara kuu ya bunge na elimu ya kiraia na ofisi ya vijana wa kiafrika) inatangaza udhamini wa Gamal Abd Elnaser wa kiafrika,mnamo kipindi cha tarehe ya 8 mpaka tarehe ya 22 toka mwezi wa Juni ujao katika Kairo.
Na udhamini huo unawalenga vijana mia moja (100) toka viongozi maarufu wa nchi wanachama za Umoja wa kiafrika kama waanzishi wa maamuzi ndani ya sekta ya kiserikali, viongozi watendaji, katika sekta binafsi, vijana wa kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa kwa vijana, wataalamu wa vyuo vikuu, watafiti wa vituo vya tafiti za kimikakati na kimawazo, wanachama wa vyama vya kiufundi, na waandishi wa vyombo vya habari.
Kulingana na matukio ya Mkutano wa Vijana wa Pili wa kiafrika iliyofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia (Addis Ababa), katika kipindi cha 24 hadi 26 Aprili, 2019 . Kwa lengo la kuwatolea vijana wa kiafrika kwa njia nzuri.
Udhamini wa Gamal Abd Elnaser ni mmoja wa vyombo vikuu vya kutekeleza mpango wa (Vijana milioni 1 kwa mwaka 2021), Ambao ilizinduliwa kuwa kuwezesha na kuendeleza vijana barani Afrika Kupitia Kufundisha vijana milioni moja wa kiafrika Katika nyanja za Elimu, Ajira , Ujasiriamali na ushirikiano (4 E’s), kwa kufikia mwaka 2021 , na hayo yote yanayolengwa kwa udhamini wa Gamal Abd Elnaser katika sekta ya Elimu .
Na udhamini huo unalenga kuhamisha majaribio ya kimisri ya kale katika kuunda taasisi za kitaifa, pia kupatikana kizazi kipya cha vijana waongozi wa kiafrika, wenye mtazamo unaowafikiana na mielekeo ya Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika, ambao unaita kwa huduma ya malengo ya Umoja wa kiafrika kupitia kushirikiana pamoja.
Na hayo yanaenda sawa sawa na Kuangalia kwa wizara ya vijana na michezo kwa uongozi wa Dokta Ashraf Sobhi ili; kufanya mchango wake unaohusiana na kuimarisha jukumu la vijana wa kiafrika ; kupitia kutoa aina zote za msaada na mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika vyeo vya uongozi na kunufaisha toka uwezo wao na mawazo yao; kulingana na yaliyotangazwa na rais Abd Elfatah Elsisi kupitia matukio ya mkutano wa vijana wa Ulimwengu, pia kutekleza uamuzi wake ili kufanya mwaka wa 2019 uwe mwaka wa Elimu.
Na kwa upande wa masharti, yanawakilisha katika:
1. Mshiriki lazima awe mwafrika asiye mmisri na asiyeishi nchini Misri.
2. lazima pasipoti iendelee kwa miezi 6 baada ya kuishia udhamini.
3. lazima awe mwenye lugha ya kiingereza nzuri sana ( kuizungumza-kuisoma- kuiandika).
4. lazima awe na uzoefu wa shughuli ya kiraia.
5. lazima awe mwenye umri toka miaka20 hadi miaka 35.
6. lazima mshiriki awe na Utambulisho wa nchi toka za Umoja wa kiafrika au Ughaibuni wa kiafrika.
Inatajwa kwamba Udhamini wa Abd Elnaser ni Udhamini wa kwanza wa ( kiafrika -kiafrika), unalenga vijana waongozi watendaji wa kiafrika, wenye vitengo tofauti ndani ya jamii zao, Nao ni mmoja toka vyombo vikuu vya kuwezesha kwa mabadiliko ya kiafrika, vilivyoainishwa na ajenda ya 2063; ili kuyaimarisha maadili ya kiafrika, kupitia kujitegemea, mshikamano, kazi kwa bidii, ustawi wa pamoja, na kujenga juu ya mafanikio ya kiafrika na ujuzi, na vitendo vizuri zaidi ili kuunda mfumo wa kiafrika, kwa mabadiliko na maendeleo. Pia Udhamini huo unazingatiwa mmoja wa vyombo vya" unyonyaji wa marejeo ya idadi ya watu kupitia Uwekezaji wa vijana " sawa sawa na Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika mwaka wa 2019.