Nafasi ya Uwekezaji Barani Afrika ni la kujadiliwa katika Udhamini wa Nasser Kwa Uongozi wa Kiafrika

Mhandisi Amany khuder, Mkuu wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa miradi ya Afrika katika kampuni ya (Al mokawloon Al Arab), ameeleza Utunzaji wa Misri ikiongozwa na Rais Abd El Fatah El Sisi katika kuwekeza kupitia uanzishaji wa miradi kadhaa ya maendeleo Barani Afrika, miongoni mwao ni inayohusiana na Barabara,majengo na ujenzi na mingine ya maendeleo,
akisisitiza mchango mkubwa wa Misri katika kuboresha Mahusiano na nchi za Afrika katika nyanja zote.
Hayo yametokea wakati wa mkutano wa "Fursa za Uwekezaji Barani Afrika, kama sehemu ya shughuli za siku ya tisa ya "Udhamini wa Nasser Kwa Uongozi wa Kiafrika" uliozunduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo ( Ofisi ya Vijana ya Afrika na Idara kuu wa Ubunge na Elimu ya kiraia) kwa Ufadhili wa Dkt.Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu mnamo kipindi Cha 8 hadi Juni 22,2019, Kwa ushirikiano na Umoja wa vijana wa Afrika.
Kudher alisisitiza umuhimu wa kuhimiza Uwekezaji na kukabiliana na changamoto za Maendeleo katika nchi za Afrika na kukuza fursa za Ushirikiano kati yao, akiashiria nia ya serikali ya Misri ya kuboresha na kujenga miundombinu na kuendeleza Rasiliamali kwa ajili ya kupatikana fursa ya Uwekezaji katika nyanja zote na nchi nyingine kufanya kazi ili kufikia Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063,
Pia kuongeza nafasi ya Mikusanyiko ya kiuchumi katika nyanja za maendeleo ya Kiafrika,
Khuder aliashiria umuhimu wa kuwasiliana na nchi za Kiafrika na kuunganisha yanayohusu faili ya Kiafrika katika uwanja wa miundombinu, iwe katika huduma za afya na elimu kupitia miradi muhimu zaidi ya kitaifa inayotekelezwa na ( Al mkawloon Al Arab) kupitia maeneo kadhaa ya ushirikiano ambayo ni pamoja na ujenzi wa Barabara, ujenzi wa madaraja, na Majengo ya Elimu na ya Afya katika nchi za Kiafrika.