Kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Rwanda
Mnamo mwaka 1884, Rwanda ikawa sehemu ya koloni la Afrika Mashariki la Ujerumani. Baada ya kushindwa kwa Ujerumani katika Vita vya Kwanza vya Dunia, sehemu hii ilipewa kwa Ubelgiji, na eneo la Rwanda-Urundi likawa mamlaka inayohusiana na Ubelgiji mnamo mwaka 1924, na kuwepo kwa Ulaya kupitia miaka kadhaa hakukuathiri mabadiliko ya muundo wa kijamii wa Rwanda .
Migogoro na mizozo ilioongezeka kutokea kati ya vikundi viwili vya kikabila vya HUTU na TUTSI kuhusu kuwezesha kila kundi liwe na utawala zaidi, na hiyo ndiyo iliyosababisha kuzuka kwa mapinduzi ya Rwanda mnamo mwaka 1959.
Mnamo mwaka 1961, kura ya maoni ya watu ilitokea na ilisababisha mabadiliko ya Rwanda kutoka koloni la Ubelgiji na ikitawaliwa na ufalme wa TUTSI, mpaka kuwa Jamuhuri inayoongozwa na HUTU . Mnamo Julai Mosi, 1962, Rwanda ilitangazwa kama Jamhuri huru inayowakilisha nusu ya kaskazini ya eneo hilo lililokuwa likijulikana kama Rwanda-Urundi, wakati ambapo nchi ya Burundi ya kisasa inawakilisha nusu ya kusini kwa eneo hilo.
Misri inazingatiwa mojawapo ya nchi za kwanza za kutambua uhuru wa Rwanda na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja nayo baada ya uhuru, na ilikuwa moja ya nchi za kwanza kufungua ubalozi huko mji mkuu Kigali mnamo mwaka 1976.
Licha ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda mnamo mwaka 1994, Misri ndio nchi ya kipekee isiyofunga milango ya Ubalozi wake au kuomba kuondoka kwa ujumbe wake wa kidiplomasia mnamo kipindi kizima cha vita nchini Rwanda.