Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu..Na maadhimisho ya miaka 65 ya Umoja wa Misri na Syria

Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu..Na maadhimisho ya miaka 65 ya Umoja wa Misri na Syria

Imefasiriwa na / Osama Mostafa Mahmoud

Siku kama ya leo, Februari 22, 1958, Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser na mwenzake wa Syria, Shukri Al-Qawatli, walitia saini mkataba wa Umoja kati ya Misri na Syria, nao ni Umoja mkubwa zaidi katika historia ya Waarabu, ulioanza kuwaunganisha nchi za kiarabu, na "Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu" ni matokeo ya Umoja huo kati ya pande hizo mbili Misri na Syria, na Kairo ilichaguliwa kuwa mji mkuu wake, na kuamua kupatikana kwake  mfumo kidemokrasia wa urais, na kura ya maoni ilipigwa ; kwa suala la Umoja huo na Gamal Abdel Nasser alichaguliwa kwa Rais wa Jamhuri na ikawa na Katiba mpya.


Mnamo 1960, mabunge ya nchi hizo mbili yaliunganishwa katika Bunge la Kitaifa mjini Kairo, na Wizara za kikanda zilifutwa kwa ajili ya serikali ya Umoja, na Misri na Syria zilikubali kuunda uongozi wa kijeshi wa pamoja, ukiwa na kituo kikuu huko Damascus, ambapo Umoja wa Kisovieti ulianza kampeni kubwa ya kupatia nchi za Mashariki ya Kati kwa upande wake, na Misri na Syria zilikubali mikataba ya silaha ya Soviet.

Wakati wa kutangazwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, Rais Abdel Nasser alitoa hotuba yake maarufu, akisema:

"Enyi Wananchi.. Matumaini mapya yamepambazuka katika upeo wa Mashariki hii. Nchi mpya inazuka moyoni mwake. Imezuka dola kubwa katika Mashariki hii isiyo ya nje wala si mnyang'anyi. Haina uadui nayo wala haina wivu hata, nchi inayolinda na kutotishia, inahifadhi na haifujai, inatia nguvu haidhoofishi, inaunganisha na haitenganishi, inafanya amani na haikati tamaa, inaimarisha usaidizi wa rafiki, inafukuza vitimbi vya adui, haina upendeleo, hakengeuka wala kuegemea upande wowote, anathibitisha haki, inaunga mkono amani, inajipatia ustawi wake, kwa wale wanaoizunguka, kwa wanadamu wote, kwa kadiri inavyovumilia na kustahimili".

Hata hivyo, Umoja huo haukudumu kwa muda mrefu, na ulimalizika kwa mapinduzi ya kijeshi huko Damascus mnamo Septemba 1961, na Syria ikabaki ikijulikana kama "Jamhuri ya Kiarabu ya Syria", huko Misri ikilibakisha jina la "Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu" hadi 1971. na ilibadilishwa jina lake la kisasa, Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.

Wengi wanaamini kuwa wito wa kuwepo Umoja umekuja kwa ajili ya kuitikia matakwa ya wananchi wa Misri na Syria kwa kuzingatia hali ya kimataifa iliyoshinikizwa na matukio ambayo ulimwengu wa Kiarabu ulishuhudia wakati huo.

Licha ya kukosekana kwa muendelezo wa Umoja huo, ila Wamisri na Wasyria bado wanaiona kumbukumbu hii kuwa ni tukio la kukumbuka zama ambazo mataifa haya mawili yalishiriki mapambano, maumivu na matumaini kwa pamoja.