Sikukuu ya Wafanyikazi yamaanisha nini kwa Wakenya?

Sikukuu ya Wafanyikazi, pia ikijulikana kama Siku ya Wafanyikazi Duniani au Siku ya Wafanyikazi, ni Likizo rasmi inayotambuliwa katika nchi mbalimbali Duniani kote; Kuthamini mapambano ya watu wanaofanya kazi.
Nchini Kenya, Siku ya Wafanyikazi huadhimishwa mnamo Mei mosi kila mwaka.
Siku hiyo, Wakenya wengi hawaendi kazini lakini badala yake, huhudhuria hafla ya umma ambayo kawaida huandaliwa kwa Chama cha Wafanyikazi.
Wafanyikazi Wakenya wengi kwa kawaida huwa na matarajio mengi kutoka kwa serikali katika siku hiyo. Katika siku nyingi za Sikukuu ya Wafanyikazi, ambayo mara nyingi hufanyikwa kwenye bustani ya Uhuru, Nairobi, tena kwa kawaida humwona Rais wa Kenya au Rais wa Chama cha Wafanyikazi akitoa hotuba akiwahutubia wafanyikazi.
Siku hiyo inaeleza maswala yanayomzunguka mfanyikazi, ambapo kuna mambo matatu ambayo kwa kawaida hushughulikiwa katika siku hiyo.
1. Ongezeko la mishahara: - Watu wote wanaofanya kazi wanapaswa kupokea ongezeko la mishahara kulingana na ongezeko la gharama za maisha na hali ya kiuchumi.
2. Afya na Amani ya Wafanyikazi:- Kila mwajiri nchini Kenya lazima ahakikishe kwamba wafanyikazi wake wanafanya kazi katika mazingira yanayofaa ambayo yanaafiki viwango vya afya vilivyoainishwa katika Katiba.
3. Haki za Kikatiba za Wafanyikazi:- Siku hiyo, wafanyikazi wote wanatakiwa kupokea uangalizi na heshima ya hali ya juu. Pia wapate sifa stahiki kwa kazi wanayoifanya kwa kuboresha Nchi.