Sikukuu ya Mkulima Mmisri Pamoja na Kiongozi Gamal Abdel Nasser na Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi
Imetafsiriwa na/ Enas Abd El-Basset
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Maadhimisho ya miaka 70 ya Sikukuu ya Mkulima Mmisri yanayoingiliana na maadhimisho ya kuanzishwa kwa Sheria ya mageuzi ya Kilimo mnamo Septemba 9, 2023, Sikukuu ya Mkulima iliadhimishwa baada ya Mapinduzi ya Julai 1952,wakati kiongozi wa hayati Gamal Abdel Nasser alipotekeleza sheria ya mageuzi ya kilimo iliyotoa usambazaji wa umiliki wa ardhi ya kilimo kutoka kwa mabwana wa maliki kwa wakulima wadogo.
Sheria hiyo ina vifungu 6 vinavyojumuisha mada 40, Kifungu chake cha kwanza kiliweka kiwango cha juu cha umiliki wa kilimo kwa ekari 200 kwa mtu, na kifungu cha nne kilimruhusu mmiliki kuwapa watoto wake ekari mia moja,sheria iliwaruhusu wamiliki wa ardhi kuuza ardhi yao ya ziada kwa mtu yeyote waliyemtaka, na iliwapa haki ya kuepuka ardhi inayouzwa ya watu wengine , kama sheria iliamua kutoa malipo kwa wamiliki wa ardhi,thamani za ardhi ilipimwa kwa mara kumi ya thamani yake ya kodi, na kuongeza mali na vifaa vingine (miti na mashine) vilivyowekwa kwenye ardhi kwa thamani kubwa, aidha Tume ya Mabadiliko ya Kilimo ilianzishwa, pamoja na Mashirika ya Mabadiliko ya Kilimo, ili kuchukua ardhi kutoka kwa wamiliki wa ardhi baada ya kuondoka kwa kiwango kilichowekwa na sheria, kuanzia ekari 50 hadi ekari 200, na kugawanya ardhi iliyobaki kwa wakulima wa kukodisha wa maskini wanaofanya kazi kwenye ardhi ileile kwa kiwango cha 2 hadi 5 ya hekta, ili wabadilishwe kutoka kuwa wapangaji na kuwa wamiliki, na kulipa malipo ya ardhi hii kwa awamu kwa miaka 30, kwa riba ya 3% kwa mwaka, ikiongezwa 1.5% ya thamani ya jumla ya ardhi; Kwa mujibu wa mali zilizokuwa kwenye ardhi, jumla ya ardhi ambayo sheria ya Septemba ya 1952 inatumika ilikuwa 653.736 elfu ya ekari inayomilikiwa na wamiliki wa 1789 wakubwa, lakini ardhi ambayo sheria hiyo ilitumika kwa kweli ilikuwa 372.305 elfu ya ekari, na iliyobaki ni karibu na nusu iliuzwa na wamiliki kwa njia zao wenyewe hadi Oktoba ya 1953, wakati serikali ilipofuta kifungu ambacho kiliwawezesha wamiliki kuiuza kwa njia zao wenyewe, takwimu rasmi zilionyesha kuwa hadi mwaka 1969, 989,184 ya ekari ziligawanywa kwa wakulima, kati ya hizo 775,018 ya ekari zilikuwa zimechukuliwa kwa mujibu wa sheria za mageuzi ya kilimo, Kukomesha wa umiliki wa kilimo chini ya mipango ya jumla ya kilimo kupitia mzunguko wa kilimo, ulisaidia kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira, na kuongeza kiwango cha kiuchumi cha wakulima wa Misri katika mfumo sambamba na mpango wa kiuchumi wa serikali kwa kufikia kujitegemea kwa mazao ya kilimo, pamoja na mabadiliko mazuri ambayo yametokea katika maisha ya mkulima wa Misri, ambapo shule na vitengo vya afya vimeingia vijijini, kiwango cha ufahamu, kiwango cha elimu, hali ya afya na uchumi viliboreshwa vijijini kwa sababu ya mapinduzi, na tangu wakati huo, siku ya mkulima wa Misri imekuwa ikiadhimishwa mnamo Septemba 9 kila mwaka, ili kuishi na kichwa chake juu, kumiliki nguvu ya siku yake, kuishi kwa upendo katika nchi yake, na kuchangia ujenzi wa nchi yake.
Hivi karibuni, katika muktadha unaohusiana, uongozi wa kisiasa nchini Misri umetilia manani mkulima mmisri na nyanja ya mageuzi ya kilimo, ambapo Mhe. Rais Abdel Fattah El-Sisi aliamua idadi ya vifaa kwa mkulima mmisri, kama zawadi kutoka kwake na kwa shukrani na utambuzi wa mkulima mmisri hakuachaia jukumu lake hata katika misiba ya dhiki na majanga ambayo nchi ilipitia na mapinduzi, vita na magonjwa ya milipuko kwa muda mrefu, kutambua jukumu la mkulima wa Misri katika kufikia Usalama wa Chakula, na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi, maamuzi haya yanafuatiana na maadhimisho ya Siku ya Mkulima mwaka huu, maamuzi haya ni pamoja na kusimamisha kodi ya udongo wa kilimo kwa kipindi cha miaka 6, na kuzindua mradi wa kuingiza ndani ya mfereji uliosababisha ongezeko la maeneo ya barabara, ardhi za kilimo, na kufanya kazi ya Kuendeleza vijijini vya Misri kupitia mpango wa “Maisha Mema” unaosaidia utoaji wa mtandao wa barabara na usafi wa afya kwa wakulima, pamoja na kutoa huduma na bima ya afya kwa mkulima, na pia kupanuza sehemu ya ardhi ya kilimo katika miradi ya kitaifa kwa kugeuza ekari milioni nne, K.m, mradi wa “Mustakabali wa Misri” una lengo la kurudisha hekta 350 kama hatua ya kwanza na kutekeleza sheria ya kilimo cha mkataba kwa mazao fulani.
Mhe. Rais pia alizindua mradi wa kitaifa wa kuhifadhi mazao ambayo imesababisha kupunguza upotezaji wa ngano na kuwezesha kazi ya utoaji wa mazao, pamoja na mradi wa kitaifa wa uzalishaji wa mbegu ambayo itatoa kiasi kikubwa kwa wakulima katika thamani ya mbegu yaliyoingizwa, Pamoja na kazi ya serikali ya kutoa mkopo wa “Pitlu” ambayo ilisaidia wakulima na wafugaji kutoa mtaji kwao na kununua kulisha na mifugo, pia ni muhimu kutaja kwamba uamuzi wa utukufu wake wa kuwaondolea watu maskini zaidi ya pauni 25,000 na kufuta madeni ya wakulima na kupunguza mzigo,
Utaratibu wa ardhi kwa watu wenye haki ya uhamisho wa umiliki wa ardhi ni sehemu ya juhudi kubwa za serikali ya Misri za kukomesha umaskini na uhitaji, kuleta haki ya kijamii na kutoa maisha ya heshima kwa raia wa Misri katika maeneo yote ya jamhuri.
Vyanzo:
• Wakulima: Dr. Baba Henry Eyrot, Mjesuiti
• Farouk na kuanguka kwa ufalme wa Misri 1936-1952, kwa Dk. Latifa Salem
• Ripoti ya Benki ya Dunia namba [870 - A] kuhusu Misri iliyotolewa huko Washington mnamo Januari 5, 1976 baada ya kifo cha Rais Gamal Abdel Nasser kwa miaka mitano na miezi minne.
• Kitabu “Kuanguka Baada ya Nasser Kwa Nini?” na Adel Hussein.
• Majaribio ya Othman: Abdullah Imam.
• Mustakabali wa kilimo nchini Misri: Dk. Mansour Abdel Fatta.
• Ushuhuda wa Magdy Hassanein katika kitabu "Mashahidi wa Julai": Ahmed Hamroush.
• Maandishi ya/Kumbukumbu za Sayed Merhi – Sehemu ya Pili.
• Amr Sobeh: Kilimo cha Misri kati ya enzi ya kifalme na enzi ya Nasser.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy