Kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo…. Mavuno ya Mapambano ya Lumomba na uungaji mkono wa kudumu wa Nasser

Siku kama hii mnamo 1960, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipata uhuru  wake kutoka kwa Ubelgiji,  wakati ambapo Leipold wa pili , mfalme wa Ubelgiji alikuwa amepata haki ya kumiliki Congo baada ya Mkutano wa Berlin mnamo mwaka 1885, na nchi hizo zikawa koloni maalum kwa Leipold mwenyewe sio kwa Ubelgiji, na aliiita "Congo huru." 

Watu wa nchi hiyo waliteseka kwa miaka kadhaa kutokana na kutendeana vibaya chini ya utawala wa Leipold hadi bunge la Ubelgiji liliingilia, na Ubelgiji ilichukua utawala wa Kongo huru mnamo mwaka 1908 na iliiita " Congo ya Ubelgiji", hali haikuwa nzuri zaidi na machafuko  ya Ukoloni kama kuiba haki, kutumia rasilimali za nchi vibaya yaliendelea, na wakazi wa Kongo ya Ubelgiji walianza kuomba Uhuru kwa miaka kadhaa, na kuzuka mapinduzi na vuguvugu dhidi ya utawala wa Ubelgiji, na harakati ya kitaifa ya Kongo ilizinduliwa mnamo mwaka 1958 ikiongozwa na kiongozi Patrice Lumumba kupinga ukoloni na kuasi dhidi yake, hadi Ubelgiji ilipewa uhuru kwa koloni  hilo mnamo tarehe Juni 30, 1960, na ikaitwa Jamhuri ya Congo, na Patrice Lumumba  alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri na Jossef Kasavubu ni Rais wa Jamhuri. 

Mnamo enzi ya Rais Gamal Abd El Nasser, Misri ilitoa njia zote za misaada kwa harakati za ukombozi na vita vya uhuru vinavyohusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupambana na ukoloni, na Vyombo vya habari vya kimisri vilionyesha hila zote za ukoloni wa Ubelgiji  zinazolenga kutengana pamoja na kuunda na kusaidia harakati za umoja kwa ajili ya kuendelea kutumia rasilimali za nchi vibaya, na Rais Gamal Abd El Nasser alimsaidia kiongozi Patrice Lumumba, na haki yake ya kuiwakilisha serikali kuu hadi Kongo itakapopata uhuru wake.

Baada ya uhuru, Misri iliunga mkono Umoja wa Congo kupambana na njama za kujitenga, wakati ambapo Congo haikufurahi kwa muda mrefu kwa uhuru na mgongano ulitokea kati ya Lumumba na Kasavubu (aliyejulikana kwa uaminifu wake kwa Wabelgiji), na alimwondoa Lumumba kutoka serikali nanchi  zilianza vita vya wenyewe kwa wenyewe, na mnamo wakati huo Misri ilikaribisha familia ya Lumumba huko Kairo kulingana na utashi wake wa kuwahamisha na kuwapeleka kwa Gamal Abd El Nasser baada ya kuhisi hatari kwao, na Lumumba aliuawa mnamo tarehe Januari 1961, na Misri iliendelea kutoa misaada yote ya kila namna kusaidia Congo na kuunga mkono Usalama na Utulivu  wake wa ndani.