Siku ya kimataifa ya Kupambana na majaribio ya Nyuklia "

Hapo mwanzo , wazo la kumiliki silaha za nyuklia lilikuwa mojawapo ya vigezo muhimu zaidi vya maendeleo ya kisayansi na nguvu ya kijeshi ulimwenguni, bila ya kuzingatia athari hasi za majaribio zinazoharibu maisha ya binadamu, pamoja na hatari na a matokeo ya nyuklia na majanga ya kibinadamu na ya mazingira yanayotokana na majaribio ya angahewa, kwa hivyo umuhimu wa kuadhimisha siku ya kimataifa hiyo unakuja ili Kupambana na majaribio ya Nyuklia, ambapo mnamo kipindi kilichopita , mwakani 1996, Umoja wa Kimataifa ulizindua mkataba wa kimataifa unaokiri kwa kupiga marufuku kwa majaribio ya nyuklia, na kusisitiza kuweka mipaka na kukomesha aina zote za majaribio ya nyuklia japo nchi 185 zilitia saini mkataba huo na nchi zingine 170 ziliidhinisha ila hazijaanza bado kuutekelezwa hadi sasa.
Na mnamo 2009, Umoja wa Mataifa ulitangaza tarehe Agosti 29 kuwa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Majaribio ya Nyuklia, kwa mujibu wa azimio la 64/35 linalokiri kuwa "inapaswa kufanya juu chini ili kukomesha majaribio ya nyuklia ili kuepusha athari hasi na zinazoharibu maisha na afya ya watu.vilvile , Azimio hilo linaomba Kuzinduliwa kwa shughuli na matukio ya kuelimisha ili kuongeza ufahamu wa athari za majaribio ya milipuko ya silaha za nyuklia au milipuko ya nyuklia yoyote mingine, na kusisitiza dharura ya kuyakomeshwa kama ni njia mojawapo ya mbinu na mifumo inayolenga kufikia lengo la kuunda ulimwengu usio na silaha za nyuklia.
Mnamo Agosti 29, 2012, Kazakhstan ilizindua mpango wa kimataifa wa "ATOM" katika uwanja wa ukomeshaji wa silaha za nyuklia na diplomasia ya umma. Hayo yalitajwa katika Kongamano la kimataifa "Kutoka kupiga marufuku kwa majaribio ya nyuklia Kuelekea ulimwengu usio na silaha za nyuklia" katika Siku ya Kimataifa ya kupambana na Majaribio ya Nyuklia, na zaidi ya watu 316000 ulimwenguni kote walitia saini mkataba wa mtandao unaohusisha mradi wa " ATOM" ambao unaiomba serikali kuthibitisha mwanzo wa kutumika kwa Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia kwa ajili ya kukiri jukumu na umuhimu wa viongozi na mashirika ya kisiasa na ya umma na kuwahimiza, kisha mnamo 2016, ilizindua tuzo " kwa ajili ya ulimwengu usio na Silaha za Nyuklia na Usalama wa Dunia", lengo lake kuu lilikuwa kufahamisha ulimwengu kwa viongozi, mashirika, wasimamizi na watu wasio wa serikali, ambao walitoa juhudi na michango mikubwa katika uwanja wa kutekeleza utulivu wa kikanda, kuimarisha usalama wa kimataifa na kusimama kwa nguvu dhidi ya vita, ugaidi na upanuzi wa silaha za maangamizi makubwa.