Kumbukumbu ya miaka 47 ya uhuru wa Visiwa vya Comoro kutoka Ufaransa
Wakati ambapo visiwa vilidhibitiwa kamili na Ufaransa mnamo 1913 na vilikuwa rasmi koloni la Ufaransa. Na ifikapo 1972, Mapambano kwa ajili ya uhuru yakaanza kuongezeka sana pamoja na kuwepo kwa vyama vya Upinzani, vilivyoanza harakati zake kwa nguvu dhidi ya Ukoloni.
Baada ya mazungumzo pamoja na Ufaransa, kura ya maoni ilifanyika mnamo 1974, katika visiwa vikuu vinne vya nchi (Anjouan, Moheli, Mayotte, na Kisiwa kikibwa cha Comoro), wakati ambapo visiwa vitatu vilipiga kura kwa uhuru kwa asilimia 95, wakati kisiwa cha Mayotte kilipiga kura dhidi ya uhuru na asilimia 63.8, na kilipenda kubaki Chini ya utawala wa Ufaransa, na hivyo kwa sababu ya kuwepo kwa kiasi kikubwa cha wageni ndani yake.
Mnamo Julai 6, 1975, Bunge la Visiwa vya Comoro lilitoa uamuzi wa upande mmoja tu kutangaza uhuru wa nchi hiyo, na Visiwa vya Comoro vilipata uhuru wake, isipokuwa Kisiwa cha Mayotte, kilichobaki chini ya utawala wa Ufaransa.