Leo ni kumbukumbu ya miaka 45 ya uhuru wa Jamhuri ya Djibouti

Leo ni kumbukumbu ya miaka 45 ya uhuru wa Jamhuri ya Djibouti

Djibouti  ilikuwa moja wapo ya makoloni ya Ufaransa na inajulikana tangu 1896 kama " Somalia ya kifaransa", na mnamo 1958 ilifanyika kura ya maoni  kwa ajili ya kuamua kubaki Djibouti  kama koloni la Ufaransa au uhuru na kujiunga kwa Somali, na matokeo ya kupiga kura yalikuwa kwa upande wa kuendelea kama sehemu ya Ufaransa, pamoja na kuwepo shaka ya  kudanganya kwa kupigiwa kura kwa upande wa kifaransa.

Na matokeo ya msukumo  wa watu wa Djibouti na mapigano ya silaha dhidi ya wafaransa, mnamo 1967, serikali ya Ufaransa iliruhusu kushikilia kura nyingine ya kuamua hatima ya nchi, na tija ya kura ilikuwa kwa asilimia 60% kuendelea  kuweka Djibouti chini ya utawala wa Ufaransa (kulingana na madai ya serikali ya Ufaransa), na jina la Djibouti lilibadilishwa kutoka kwa  "Somalia ya kifaransa" na kuwa "Kanda la Afars na Issas ya kifaransa." 

Watu wa Djibouti waliendelea katika upinzani huo na wakiomba  haki yake ya uhuru hadi Ufaransa ililazimishwa kushikilia kura nyingine mnamo Mei 8, 1977, ambapo watu wa Djibouti waliunga mkono uhuru kwa idadi kubwa sana ya 98.8%, na Djibouti ilipata uhuru mnamo Juni 27, 1977 kama koloni la mwisho la Ufaransa barani Afrika lililopata uhuru.

Inatajwa kuwa Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na Jamuhuri ya Djibouti baada ya uhuru mnamo 1977, na kwa wepesi  imeanzisha ubalozi wa kimisri huko.